On Star TV: Chaguzi ndani ya vyama vya siasa - Nafasi ya vijana kuelekea 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

On Star TV: Chaguzi ndani ya vyama vya siasa - Nafasi ya vijana kuelekea 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yahya Mohamed, Sep 2, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Salaam wakuu

  Kutokana na kuendelea kwa wimbi la kuwafungamanisha VIJANA wanaowania nafasi mbalimbali katika vyama vya siasa kuwa hawana nia ya dhati ya kuleta mabadiliko zaidi ya kutumiwa na kundi Fulani au kufanya siasa kwa malengo maalumu binafsi Leo tutajadilii nafasi Yao katika chaguzi za vyama.

  Wageni Mwanza:

  John Deya - mgombea mwenyekiti CCM Taifa
  Adam Chagulani - Diwani Igoma CDM

  Dar:

  David Kafulila (MB)
  William Malecela (tunamleta kwa lengo la kujibu mengi ambayo hayajapata majibu hapa JF akiwa Kama Moja wa Wanachama waliokuwa na changamoto za kutoa moyo tofauti na anavyotafsiriwa kwa sasaa)

  Karibuni kwa mjadala
   
 2. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Huyo William Malecela kama kijana amekaa Marekani miaka mingi ametuletea nini tujifunze? [Tunachoona kutoka kwake ni aibu tupu kutafuta madaraka ndani chama cha baba yake]
   
 3. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
 4. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Naomba umuulize bwana Deya, chaguzi nyingi ndani ya CCM hugubikwa na tuhuma za rushwa, na inavoonesha CCM wameshindwa kujipambanua katika suala la rushwa labda kutokana na kukosa dhamira ya dhati ya kushughulikia rushwa au kutoikana na faida itokanayo na rushwa kwa kikundi fulani cha watu.

  Ni nini mkakati wake yeye katika kupambana na rushwa katika chama chake?
   
 5. jobe ayoub

  jobe ayoub JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 206
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania itakombolewa na vijana na hali halisi ipo wazi.

  Angalia kwa mfano CHADEMA, vijana ndio wanaleta mabadiliko hapa nchini, ukiachana na Dr slaa, Mbowe na Tundu lissu - waliobakia wengi ni vijana.....
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Yahya M,

  Mie nina maswali matatu katika huu munakasha, swali la kwanza.

  1. Kwa Adam Chagulani, baada ya Madiwani wa Nyamagana kumuondoa Meya wa Jiji la Mwanza kwa ufisadi nasikia nyie kama vijana wa Mwanza mnamuaandaa Diwani wa Mirongo (CUF) Daudi Mkama, kuwa Meya wa Jiji la Mwanza.

  2. Kwa William Malecela, kwanini kawakimbia vijana JF katika harakati za kisiasa wakati bado watu wanamuitaji?

  3. Kwa Kafulila, vipi mgogoro wake na NCCR Mageuzi umekwisha au ameishajipanga kuondoka?
   
 7. M

  Mkono JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Itakuwa ngumu vijana kusaidia katika mabadiliko tunayohitaji maana vijana wengi wa sasa wanaingia kwenye siasa kwa ajili ya maslahi binafsi tofauti na wazee wetu waliongia kwenye siasa kwa kusukumwa na uzalendo wa nchi yao.
   
 8. jobe ayoub

  jobe ayoub JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 206
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Dhana ya kwamba vijana hawawezi au wanatumika, ni uvivu wa kufikiri kwa watu wasioona mbali.

  Mmabadiliko yoyote duniani si kwenye siasa tu chanzo hua ni vijana, iwe utamaduni, uchumi, burudani na michezo+siasa, bila vijana hakuna kitu.
   
 9. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Mkuu Yahya M,

  Mimi nina maswali kidogo

  1) Kwa Malecela: Ndugu Malecela unafikiri chama chako cha CCM kinawapa nafasi stahili vijana katika uongozi wa chama kwa ujumla? Je, unafikiri kwanini CCM inaonekana kukosa mvuto kwa vijana wengi nchini?

  2) Kwa wote wageni hapo: Je inawezekana hivi karibuni kuona chama kimoja cha siasa kinampa kijana nafasi ya juu kabisa ya utawala kama Mwenyekiti wa kitaifa? Wanafikiri kwanini vijana hawapati nafasi ya juu kama hiyo ndani ya vyama vya kisiasa?
   
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Huyu kijana wa CCM anampiga vijembe Dr Slaa, kuhusu bei ya saruji dogo anasema kusafirisha mfuko moja wa saruji kutoka Dar mpaka Mwanza Sh 3,000.
   
 11. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #11
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndugu William Malecela katika chaguzi nyingi za CCM zinatawaliwa na rushwa ni jinsi gani viongozi hao wanaweza kupambana na rushwa na ufisadi?
   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mwambie Wlliam kwanza hongera kwa kubuni jina changamfu la Le Mutuz.

  Pili akunjue moyo na kurudi JF, changamoto na vikwazo ni mambo ya kawaida kwenye siasa.

  Tatu afafanue vizuri jinsi rushwa ilivyotumika katika uchaguzi wa wabunge wa EA.

  Kafulila muulize akishauriwa au kuombwa kurudi CHADEMA atakubali au bado anaamini CHADEMA ina ubaguzi?
   
 13. ugolo wa bibi

  ugolo wa bibi JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 1,228
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Nchi hii itakombolewa na vijana!

  Tatizo ni CCM ambao walikua hawawapi fursa vijana, kwa sababu walikua wanajua wataumbuka! sasa moto wa M4C unawaleta vijana katika siasa, wakina Malecela kazi mnayo!!
   
 14. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Kutafuta uongozi ni sawa swali langu limejikitika jinsi unavyotafuta uongozi kwa tamaa, ina maana huna skill nyingine uliyojifunza ambayo unaweza kusaidia vijana?
   
 15. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,217
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Nafasi ya vjana ni kubwa ktk vyama vya siasa kwani huko ndiko chimbuko la viongozi wa nchi na pia chama ndicho kinasimamia serikali hvo bila kujitosa kwenye chaguzi ni kazi bure.

  Pili chaguzi nyingi hutawaliwa na rushwa hvo tunashindwa kupata vijana makini kwani vijana wengi hawana uwezo wa kifedha hii hupelekea watoto wa vigogo kupata nafasi hzo.

  Ushauri wangu kwa vijana tuache kutumiwa na Watu wanaosaka madaraka kwani hiyo hujenga makundi ndani ya vyama na pia tunaonekana kama vigeugeu mbele ya jamii.
   
 16. M

  Magesi JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nataka kujua kutoka kwa ndg Deya; kwanini chaguzi nyingi za CCM rushwa ndio inapewa kipaumbele?
   
 17. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Kwa William,

  Tunaomba atupe uzoefu wake wa uongozi kwanza kwa hapa nchini, na nini anadhani uongozi uliopo madarakani wanaweza kufanya kubadilisha hali ya maisha ya mtanzania?
   
 18. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Habari Mkuu Yahya, Nina maswali mawili

  1. Tunakubali kwamba raia yoyote ana haki ya kugombea uongozi; lakini William haoni kwamba kwa nchi yetu viongozi wanatumia uongozi wao kubeba either watoto wao au rafiki zao? Haoni kwamba tuna tatizo kubwa sana la nepotism katika nchi yetu kuliko sehemu nyingine?

  2. David Kafulila, unazungumziaje kashfa ya kutaka kumpindua mwenyekiti wako wa chama wa taifa na kumweka unaemtaka wewe, huoni hili ndio linafanya vijana msiaminiwe kwa kuwa mnaonekana kama mna tamaa.
   
 19. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,999
  Likes Received: 2,654
  Trophy Points: 280
  Swali kwa William Le Mutuz,

  Ni kwanini vijana wa CCM wamekuwa wanafiki kupindukia? Chama chenu kimekuwa mstari wa mbele kwa siasa chafu, fitna majungu, unafiki na magomvi unalizungumziaje hilo ukiwa kijana mmoja wapo ndani ya CCM?
   
 20. M

  Mkono JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Siasa za ki-baguzi kwa msingi wa dini na makabila inaonekana imekuwa sera ya Chama cha Mapinduzi, LE MUTUZ anatekeleza kwa vitendo sera hiyo kupitia mijadala mbalimbali mfano kule FACEBOOK. Je, ni kuwa hajui athari za hicho anachokifanya? ANGALIA MOJA YA POST YAKE
  [h=6]Nimepokea ujumbe huu kutoka +255713453929 unasema Wapendwa ktk bwana tumejipanga vyema kuchukua nchi 2015,Haleluyaa,operesheni vua gamba vaa gwanda itasaidia kuwatia mkononi waislam.Uingreza na Ujerumani zimeahidi kuwapa vijana wetu mafunzo ya uongozi na ya kivita,tusiache maandamano kwani yanajenga chama (CHADEMA) zaidi,mawakala wetu waliomo ndani ya CCM na CUF wanafanya kazi vyema tuliyowatuma, vyombo vya habari vimeahidi kutubeba hadi kieleweke, watangazie waumini wetu kuwa ule mpango wa KIC unaendele.(zindukeni jamani maelezo haya yanathibitishwa na Slaa ktk vyombo vya habari kuhusu Sita mguu 1 CCM na 1 CHADEMA au kwa njia yeyote ili mradi awe Rais)[/h]
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...