On Point: Bunge Lisiposimamiwa na Chombo Chochote Linakuwa La Kiimla

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,498
40,047
Kuna mambo ya hatari ambayo tumeanza kuyakubali kwa sababu tuna hasira, tumechoshwa na tumekata tamaa na ufisadi nchini. Katika hasira zetu tumeanza kukubali "liwalo na liwe" ilimradi tuonekane tuna ukali dhidi ya ufisadi. Inanikumbusha matukio ya watu kuchoma moto vibaka kwa sababu wanaamini polisi wameshindwa na kuwa wakipelekwa mahakamani "kesho yake wametoka". Ni katika hasira hizi ndio watu wanajichukulia sheria mikononi; yaani hakuna mtu wa kuwasimamia.

Nadharia ya mgawanyo wa madaraka (separation of powers) na mfumo wa kusimamiana (checks and balances) katika demokratia una lengo jambo moja kubwa - kuhakikisha hakuna chombo ambacho kinakuwa na nguvu kubwa mno dhidi ya vingine au juu ya vingine.

Baadhi yetu hatuna tatizo la ripoti ya PAC kujadiliwa Bungeni kwani kama tunavyojua hiyo siyo mara ya kwanza kwa ripoti za Kamati za Kudumu za Bunge kujadiliwa au kuletwa Bungeni. Tatizo letu baadhi yetu katika hasira hii ya kuchukia ufisadi tumeanza kuwa na mwelekeo (proclivity) ya kutaka tufanye lolote ilimradi tuonekane tumefanya kitu.

Kwamba Spika wa Jamhuri ya Muungano akitambua uwepo wa zuio la mahakama anaamua kupuuzia zuio hilo akidai kuwa sheria iko upande wao na wengine wabunge na raia wakinukuu Ibara ya 100 ya Katiba wanafanya kitu ambacho ni cha hatari. Kazi ya Bunge ni Kutunga Sheria (Legislate). Kazi ya kutafsiri Sheria hizo na Katiba ni jukumu lililoko kwenye Mahakama peke yake. Lakini, magenius wetu wametaka tukubali kuwa Spika anaweza kusimama na kutafsiri Katiba kutetea Mhimili wake na wote tunatakiwa tukubali tafsiri yake kuwa ni sahihi.

Wabunge wote waliapa kuilinda na kuitetea Katiba ya JMT lakini cha kushangaza hakuna aliyethubutu kufanya hivyo kwa sababu ni wakati wa kumwekea mtu tairi, kummwagia mafuta na kumtia kiberiti; tumechoshwa. Tumechoshwa kiasi kwamba sheria huwa zinafaa zinapokuwa upande wetu. Hili ni jambo la hatari katika demokrasia na ni jambo la hatari sana kwa nchi inayojaribu kujenga utawala wa kidemokrasia.

Isipokuwa kama hilo zuio halikuwa zuio kweli; ila kama kweli lilikuwa zuio halali limetoka mahakama kuu basi jukumu la Bunge lilikuwa ni kuchallenge uhalali wa kisheria(legality) na uhalali wake wa Kikatiba (constitutionality) badala ya kulipuuzia. Lakini kwa vile tumechoshwa haya mambo si ya maana tena; matokeo yake tunaweza kujikuta tunashabikia drama za Bungeni ili tuone tu nani anazungumza kwa ukali, nani anajenga hoja hadi tunashangilia na nani anaonekana kuinamisha kichwa hata kama katika hayo yote mabadiliko ya kweli dhidi ya ufisadi hayatokei au hayafanyiki.

NImewahi kusema huko nyuma kuwa haki ni haki hata ya adui yako nayo ni haki. Haiki haiwi haki kwa vile tu anayeidai humpendi au humjali. Sasa huko mbeleni watu wakionekana wanaandamwa na Bunge wakimbilie wapi? Kama Mbunge anatambua kuwa tafsiri ya Ibara ya 100 ni kuweza kusema lolote, juu ya mtu yeyote, wakati wowote bila kujali haki za mtu huyo basi tutakuwa tumewapa wabunge uwezo mkubwa sana juu ya wananchi, taasisi na watu mbalimbali.

Tutakuwa tumewapa wabunge haki ya watu mitaani kushambulia vibaka bila kujali nani anaweza kuwauliza au kuwawajibisha (with absolute impunity).

Tunapotaka demokrasia ni lazima tuwe tayari kufuata mapigo yake hata kama hatuyapendi. Na mojawapo ni kuhakikisha mihimili inasimamiana.

NB: Binafsi ningependa kujua Jaji Mkuu wa Tanzania Chande Othman yuko upande gani na kama anakubaliana na hili lililofanywa. Na zaidi kama kweli Bunge limepuuzia amri halali ya Mahakama Kuu basi Jaji Othman awe wa kwanza kujiuzulu kupinga (to resign in protest).
 
Ajiuzuru? ndio mdudu gani huyo kwa miungu ya Tanzania? Labda anaweza ngoja tumsubiri huyo jaji mkuu wa kijiuzuru
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji na Pasco mna lenu jambo watu wanatetea maslahi ya umma nyie mnaleta mzaha Mzaha

Nakumbuka kipindi cha nyuma SYSTEM( CAPITAL LETTER) ilikuwa unawatumia kugeuze mambo yanapokuwa yameenda kombo serikalini

Nina UHAKIKA(CAPITAL LETTER) NA kwa hili Mzee Mwanakijiji na Pasco Wako MNATUMIKA

WATANGANYIKA HATUDANGANYIKI

Mzee Mwanakijiji Inawezekana siku hizi nae tissue kama https://www.jamiiforums.com/member.php?u=12004Pasco anavyorembua macho kwa fisadi lowassa na kukubali kuwa tissue ya Lowassa.

Chezea pesa za mafisadi
 
Mzee Mwanakijiji, you are on the wrong ship!
I suppose youve heard of the sans culottes , they will want nothing short of blood!
They can sniff it in the air , and so long as they have been wronged they will bray for more blood to flow!
 
Mzee Mwanakijiji sikubalini na hoja yako. Mahakama ndiyo iliingilia Bunge na sio kinyume chake.

Mjadala wa Escrow bungeni ulianza miezi kadhaa iliyopita, na bunge likagaagiza kamati ya PAC kuangalia hilo swala. Kwa maana hiyo mjadala wa sasa bungeni unatokana na mrejesho wa kamati ya PAC. Kwa Mahakama kujitokeza katikati ya mjadala wa Bunge (mjadala ulianza wakati wa vikao vya nyuma) ni kinyume na Ibara ya 100 ya Katiba, ambayo wewe Mwanakijiji unaonekana kuisoma kivyako.

Hata hivyo, wakati wa bunge maalum la Katiba, mahakama ilikataa kusitisha mjadala kwa madai kuwa haina mamlaka ya kufanya hivyo (precedence). Na kwa upande mwingine kuna kitu kinaitwa 'public interest'. Kwenye issue ya Escrow, kitendo cha Mahakama kutoa amri ya kusitisha mjadala ambao nchi nzima wanausubiri ni kutojali public interest ukizingatia kuwa tayari baadhi ya majaji ni watuhumiwa kwenye issue yenyewe.
 
Kuna mambo ya hatari ambayo tumeanza kuyakubali kwa sababu tuna hasira, tumechoshwa na tumekata tamaa na ufisadi nchini. Katika hasira zetu tumeanza kukubali "liwalo na liwe" ilimradi tuonekane tuna ukali dhidi ya ufisadi. Inanikumbusha matukio ya watu kuchoma moto vibaka kwa sababu wanaamini polisi wameshindwa na kuwa wakipelekwa mahakamani "kesho yake wametoka". Ni katika hasira hizi ndio watu wanajichukulia sheria mikononi; yaani hakuna mtu wa kuwasimamia.

Nadharia ya mgawanyo wa madaraka (separation of powers) na mfumo wa kusimamiana (checks and balances) katika demokratia una lengo jambo moja kubwa - kuhakikisha hakuna chombo ambacho kinakuwa na nguvu kubwa mno dhidi ya vingine au juu ya vingine.

Baadhi yetu hatuna tatizo la ripoti ya PAC kujadiliwa Bungeni kwani kama tunavyojua hiyo siyo mara ya kwanza kwa ripoti za Kamati za Kudumu za Bunge kujadiliwa au kuletwa Bungeni. Tatizo letu baadhi yetu katika hasira hii ya kuchukia ufisadi tumeanza kuwa na mwelekeo (proclivity) ya kutaka tufanye lolote ilimradi tuonekane tumefanya kitu.

Kwamba Spika wa Jamhuri ya Muungano akitambua uwepo wa zuio la mahakama anaamua kupuuzia zuio hilo akidai kuwa sheria iko upande wao na wengine wabunge na raia wakinukuu Ibara ya 100 ya Katiba wanafanya kitu ambacho ni cha hatari. Kazi ya Bunge ni Kutunga Sheria (Legislate). Kazi ya kutafsiri Sheria hizo na Katiba ni jukumu lililoko kwenye Mahakama peke yake. Lakini, magenius wetu wametaka tukubali kuwa Spika anaweza kusimama na kutafsiri Katiba kutetea Mhimili wake na wote tunatakiwa tukubali tafsiri yake kuwa ni sahihi.

Wabunge wote waliapa kuilinda na kuitetea Katiba ya JMT lakini cha kushangaza hakuna aliyethubutu kufanya hivyo kwa sababu ni wakati wa kumwekea mtu tairi, kummwagia mafuta na kumtia kiberiti; tumechoshwa. Tumechoshwa kiasi kwamba sheria huwa zinafaa zinapokuwa upande wetu. Hili ni jambo la hatari katika demokrasia na ni jambo la hatari sana kwa nchi inayojaribu kujenga utawala wa kidemokrasia.

Isipokuwa kama hilo zuio halikuwa zuio kweli; ila kama kweli lilikuwa zuio halali limetoka mahakama kuu basi jukumu la Bunge lilikuwa ni kuchallenge uhalali wa kisheria(legality) na uhalali wake wa Kikatiba (constitutionality) badala ya kulipuuzia. Lakini kwa vile tumechoshwa haya mambo si ya maana tena; matokeo yake tunaweza kujikuta tunashabikia drama za Bungeni ili tuone tu nani anazungumza kwa ukali, nani anajenga hoja hadi tunashangilia na nani anaonekana kuinamisha kichwa hata kama katika hayo yote mabadiliko ya kweli dhidi ya ufisadi hayatokei au hayafanyiki.

NImewahi kusema huko nyuma kuwa haki ni haki hata ya adui yako nayo ni haki. Haiki haiwi haki kwa vile tu anayeidai humpendi au humjali. Sasa huko mbeleni watu wakionekana wanaandamwa na Bunge wakimbilie wapi? Kama Mbunge anatambua kuwa tafsiri ya Ibara ya 100 ni kuweza kusema lolote, juu ya mtu yeyote, wakati wowote bila kujali haki za mtu huyo basi tutakuwa tumewapa wabunge uwezo mkubwa sana juu ya wananchi, taasisi na watu mbalimbali.

Tutakuwa tumewapa wabunge haki ya watu mitaani kushambulia vibaka bila kujali nani anaweza kuwauliza au kuwawajibisha (with absolute impunity).

Tunapotaka demokrasia ni lazima tuwe tayari kufuata mapigo yake hata kama hatuyapendi. Na mojawapo ni kuhakikisha mihimili inasimamiana.

NB: Binafsi ningependa kujua Jaji Mkuu wa Tanzania Chande Othman yuko upande gani na kama anakubaliana na hili lililofanywa. Na zaidi kama kweli Bunge limepuuzia amri halali ya Mahakama Kuu basi Jaji Othman awe wa kwanza kujiuzulu kupinga (to resign in protest).

Mahakama kuu ni mateka bunge kutii ile amri ingekuwa kama kulipa ransom kwa wateka nyara. Mbona waziri wa sheria alifafanua hili jambo vizuri au wewe unajifanya unajua kuliko ile authority ya sheria ?
 
Mzee Mwanakijiji sikubalini na hoja yako. Mahakama ndiyo iliingilia Bunge na sio kinyume chake.

Mjadala wa Escrow bungeni miezi kadhaa iliyopita, na bunge likagaagiza kamati ya PAC kuangalia hilo swala. Kwa maana hiyo mjadala wa sasa bungeni unatokana na mrejesho wa kamati ya PAC. Kwa Mahakama kujitokeza katikati ya mjadala wa Bunge (mjadala ulianza wakati wa vikao vya nyuma) ni kinyume na Ibara ya 100 ya Katiba, ambayo wewe Mwanakijiji unaonekana kuisoma kivyako.

Hata hivyo, wakati wa bunge maalum la Katiba, mahakama ilikataa kusitisha mjadala kwa madai kuwa haina mamlaka ya kufanya hivyo (precedence). Na kwa upande mwingine kuna kitu kinaitwa 'public interest'. Kwenye issue ya Escrow, kitendo cha Mahakama kutoa amri ya kusitisha mjadala ambao nchi nzima wanausubiri ni kutojali public interest ukizingatia kuwa tayari baadhi ya majaji ni watuhumiwa kwenye issue yenyewe.

Naona siku hizi busara za Mzee Mwanakijiji zinapungua kadri siku zinavyosogea
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji na Pasco mna lenu jambo watu wanatetea maslahi ya umma nyie mnaleta mzaha Mzaha

Nakumbuka kipindi cha nyuma SYSTEM( CAPITAL LETTER) ilikuwa unawatumia kugeuze mambo yanapokuwa yameenda kombo serikalini

Nina UHAKIKA(CAPITAL LETTER) NA kwa hili Mzee Mwanakijiji na Pasco Wako MNATUMIKA

WATANGANYIKA HATUDANGANYIKI

Mwanakijiji na Pasco,kuna wakati hata mahakama haitiliwa maanani kutokana na maamuzi yake hasa ikitiliwa maanani kuwa mahakama zimekosa imani kutoka kwa wananchi kwa kuzingatia mahakama hizo hizo kutotenda haki pale haki inapotaka ifanyike hasa kwa mtu ambaye ni hohe hahe,nawezakuthubutu kusema kwamba mahakama ya hapa Tanzania imekuwa na maamuzi ambayo yamekuwa ya kuangalia nani anahitaji haki.Kifupi mahakama yetu haiminiwi tena kutokana na maamuzi yake tata.
Mtakumbuka sakata la mwanamuziki wa kinaijeria Davido,kuna pingamizi kutoka mahakama kuwa asifanye show ,lakini yeye akafanya show pamoja na pingamizi kuwekwa mahakamani,je mahakama ilifanya nini?
 
Mwanakijiji naona unapotoka na. Wewe...... Sawa mahakama ndo inatafsri sheria lakin ikumbukwe kwamba wabunge au ss wenyewe tunanukuu katiba ibara ya 100 siyo vusheria ile ni quote ya katiba..that means mahakama kuweka zuio kwa Bunge ni uvunjwaji wa katiba.UTAKUWA NAWE UMEPATA MGAO LABDA
 
Naona kwa makusudi kabisa Mwanakijiji hutaki kuangalia haki ya Bunge kuingiliwa. Unajenga hoja kwamba kuingiliwa kwa Bunge na mahakama ni sawa kwa sababu bunge limevuka mipaka. Mipaka ipi bunge limevuka, sheria gani bunge limevunja?

Kama mahakama ilikuwa inajua na kuheshimu Bunge na katiba isingefanya jambo lile. Sasa kosa lao mahakama lisiwe kosa la Bunge. Kama kujivunjia heshima wamejivunjia wao sio Bunge. Swali la msingi jiulize kwa nini Bunge wana ile ibara ya 100?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Katika jambo hili ni vizuri ungejenga HOJA kwa kutuelekeza katika ibara za katiba zilizovunjwa na BUNGE kwa maamuzi yake ya kuedelea na mjadala. Lakini kwa jinsi ulivyojenga hoja yako inaonekana ni ya jumla mno.
Wanasheria wana msemo wao usemao, ''Sio tu haki itendeke bali pia ionekane imetendeka''. Tujiuliza je, katika kutoa uamuzi wa jambo hili HAKI imeonekana kutendeka?
Sakata hili ni mithili ya vita, Vita kati ya Wavuna jasho na wavuja jasho, kati ya wala rushwa na wapinga rushwa. Tayari kuna baadhi ya huduma za jamii na miradi ya maendeleo inazorota kwa kukosa ufadhiri tulioahidiwa kwenye BAJETI. Je, nchi inatokaje hapa?
 
unadhani haya mazuio toka mahakamani yanakimbizwa haraka haraka usiku wa manane/alfajiri yana nia njema?

Mbona hii si mara ya kwanza watu kukimbilia mahakamani kuweka zuio... zipo kesi nyingi tu hata za raia wa kawaida kukimbilia kutaka mahakama iweke zuio.
 
Huyu lengo lake anataka kubadili mwelekeo wa mjadala, ambao ungesaidia wananchi kuelewa kwa undani kwa nini pesa za escrow zilitolewa BoT wakati maamuzi ya msingi hayajafikiwa, kwa nini watendaji wa serikali na wasitaafu wa nafasi za serikali walipewa ela na VIP +PAP kwa utaratibu ambao unatiliwa mashaka,
Pia wananchi tunataka kujua kwa nini ili amriwa na AG PAP wasilipe kodi za serikali na kwa nini 'mkulu kulu' kama taasisi alishidwa kujiridhisha na ushauri wa AG ni sahihi , kabla ya kutoa maagizo BoT ilipe na kufunga akaunti ya Tegeta Escrow!

La mwisho, watu wa Tanzania wanataka kujua kwa nini Waziri wa Nishati anazidi kutoa kauli na nyaraka za kidanganyifu (rejea maelezo ya Mh.Lissu na Mh.Mbowe ,Mh. Nassare leo).

Mwanakijiji anajua anacho kifanya... Hataki watanzania wajue kwa undani mambo yote niliyoeleza hapo juu. Ndiyo maana hoja zake nyingi ziko kwenye technicalities za nguvu za mihimili badala ya kutafuta ukweli juu ya maamuzi yakutiluwa shaka yanayofanywa na watawala wa nchi hii juu ya rasilimali zetu.

Ndivyo ninavyo dadisi malengo ya Mzee Mwanakijiji
 
Kuna mambo ya hatari ambayo tumeanza kuyakubali kwa sababu tuna hasira, tumechoshwa na tumekata tamaa na ufisadi nchini. Katika hasira zetu tumeanza kukubali "liwalo na liwe" ilimradi tuonekane tuna ukali dhidi ya ufisadi. Inanikumbusha matukio ya watu kuchoma moto vibaka kwa sababu wanaamini polisi wameshindwa na kuwa wakipelekwa mahakamani "kesho yake wametoka". Ni katika hasira hizi ndio watu wanajichukulia sheria mikononi; yaani hakuna mtu wa kuwasimamia.

Nadharia ya mgawanyo wa madaraka (separation of powers) na mfumo wa kusimamiana (checks and balances) katika demokratia una lengo jambo moja kubwa - kuhakikisha hakuna chombo ambacho kinakuwa na nguvu kubwa mno dhidi ya vingine au juu ya vingine.

Baadhi yetu hatuna tatizo la ripoti ya PAC kujadiliwa Bungeni kwani kama tunavyojua hiyo siyo mara ya kwanza kwa ripoti za Kamati za Kudumu za Bunge kujadiliwa au kuletwa Bungeni. Tatizo letu baadhi yetu katika hasira hii ya kuchukia ufisadi tumeanza kuwa na mwelekeo (proclivity) ya kutaka tufanye lolote ilimradi tuonekane tumefanya kitu.

Kwamba Spika wa Jamhuri ya Muungano akitambua uwepo wa zuio la mahakama anaamua kupuuzia zuio hilo akidai kuwa sheria iko upande wao na wengine wabunge na raia wakinukuu Ibara ya 100 ya Katiba wanafanya kitu ambacho ni cha hatari. Kazi ya Bunge ni Kutunga Sheria (Legislate). Kazi ya kutafsiri Sheria hizo na Katiba ni jukumu lililoko kwenye Mahakama peke yake. Lakini, magenius wetu wametaka tukubali kuwa Spika anaweza kusimama na kutafsiri Katiba kutetea Mhimili wake na wote tunatakiwa tukubali tafsiri yake kuwa ni sahihi.

Wabunge wote waliapa kuilinda na kuitetea Katiba ya JMT lakini cha kushangaza hakuna aliyethubutu kufanya hivyo kwa sababu ni wakati wa kumwekea mtu tairi, kummwagia mafuta na kumtia kiberiti; tumechoshwa. Tumechoshwa kiasi kwamba sheria huwa zinafaa zinapokuwa upande wetu. Hili ni jambo la hatari katika demokrasia na ni jambo la hatari sana kwa nchi inayojaribu kujenga utawala wa kidemokrasia.

Isipokuwa kama hilo zuio halikuwa zuio kweli; ila kama kweli lilikuwa zuio halali limetoka mahakama kuu basi jukumu la Bunge lilikuwa ni kuchallenge uhalali wa kisheria(legality) na uhalali wake wa Kikatiba (constitutionality) badala ya kulipuuzia. Lakini kwa vile tumechoshwa haya mambo si ya maana tena; matokeo yake tunaweza kujikuta tunashabikia drama za Bungeni ili tuone tu nani anazungumza kwa ukali, nani anajenga hoja hadi tunashangilia na nani anaonekana kuinamisha kichwa hata kama katika hayo yote mabadiliko ya kweli dhidi ya ufisadi hayatokei au hayafanyiki.

NImewahi kusema huko nyuma kuwa haki ni haki hata ya adui yako nayo ni haki. Haiki haiwi haki kwa vile tu anayeidai humpendi au humjali. Sasa huko mbeleni watu wakionekana wanaandamwa na Bunge wakimbilie wapi? Kama Mbunge anatambua kuwa tafsiri ya Ibara ya 100 ni kuweza kusema lolote, juu ya mtu yeyote, wakati wowote bila kujali haki za mtu huyo basi tutakuwa tumewapa wabunge uwezo mkubwa sana juu ya wananchi, taasisi na watu mbalimbali.

Tutakuwa tumewapa wabunge haki ya watu mitaani kushambulia vibaka bila kujali nani anaweza kuwauliza au kuwawajibisha (with absolute impunity).

Tunapotaka demokrasia ni lazima tuwe tayari kufuata mapigo yake hata kama hatuyapendi. Na mojawapo ni kuhakikisha mihimili inasimamiana.

NB: Binafsi ningependa kujua Jaji Mkuu wa Tanzania Chande Othman yuko upande gani na kama anakubaliana na hili lililofanywa. Na zaidi kama kweli Bunge limepuuzia amri halali ya Mahakama Kuu basi Jaji Othman awe wa kwanza kujiuzulu kupinga (to resign in protest).
Mzee Mwanakijiji Ina maana kwako kuvunjwa kwa katiba si jambo kubwa ?
Majaji Kama walimaanisha kuzuia bunge basi walivunja katiba.
Bahati nzuri majaji wanaouhuru mpana zaidi wa kutumia lugha ambayo itamsaidia likibuma.
Bunge lingesimama kwa ile iitwayo Amri ya mahakama kuu na watu wangehoji uvunjaji wa katiba majaji wanfeikana hukumu kwamba haikumaanisha kusitisha shughuli za bunge...
Ni kwanini mjadala usigusue na kujikita juu ya uhalali wa zuio hilo tukizingatia bunge na mahakama ni sehemu ya mihimili mikuu ya dola ambapo inapewa nguvu ya kuendesha mambo yake kwa kurejea katiba ya nchi ?
 
Last edited by a moderator:
Mahakama kuu ni mateka bunge kutii ile amri ingekuwa kama kulipa ransom kwa wateka nyara. Mbona waziri wa sheria alifafanua hili jambo vizuri au wewe unajifanya unajua kuliko ile authority ya sheria ?

Unafanya kosa lile lile la Makinda. Sasa Waziri wa Sheria ndiye mwenye kutafsiri maana ya sheria au Katiba?
 
Back
Top Bottom