William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
- Nimeona Mkurugenzi wa CHADEMA leo akidai maelezo kuhusiana na safari ya hivi karibuni ya Waziri wa CCM Magufuli huko Kenya na kuhusika na mikutano ya kampeni za Urais huko,
- Now kwenye hilo this time CHADEMA wapo on the right side of the coin, CCM itoe maelezo ya kina as to how and why Magufuli didi that, kwa sababu ieleweke kwamba Waziri wa Jamhuri anakuwa On Duty 24 hours akiwakilisha Jamhuri sasa alikwenda huko kuwakilisha Jamhuri au CCM?
- Ni muhimu Serikali ya CCM ikatoa maelezo sasa kabla haijageuka kuwa a big deal ni ishu ndogo sana ila ikiachwa itageuka kuwa kubwa na kutuumiza CCM, so CCM let's get the facts out now!
Es!
- Now kwenye hilo this time CHADEMA wapo on the right side of the coin, CCM itoe maelezo ya kina as to how and why Magufuli didi that, kwa sababu ieleweke kwamba Waziri wa Jamhuri anakuwa On Duty 24 hours akiwakilisha Jamhuri sasa alikwenda huko kuwakilisha Jamhuri au CCM?
- Ni muhimu Serikali ya CCM ikatoa maelezo sasa kabla haijageuka kuwa a big deal ni ishu ndogo sana ila ikiachwa itageuka kuwa kubwa na kutuumiza CCM, so CCM let's get the facts out now!
Es!
Mwananchi - Dec 13 said:CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemtaka Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kueleza kama msimamo alioutoa katika kampeni za Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga ni wa Serikali au wake.
Chama hicho kimesema kuwa msimamo alioutoa Magufuli wa kuunga mkono Chama cha ODM ni hatari kwa Tanzania hasa katika uhusiano na nchi hiyo na ni kinyume na mkataba wa kimataifa wa Rome.
Pia kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kueleza kama alimtuma Magufuli katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika Desemba 7 mwaka huu, uwanja wa Kasarani na kusema Watanzania wanaunga mkono ODM au la.
Msimamo huo wa Chadema ulitolewa jana na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa chama hicho, Ezekieah Wenje.
"Hatujui kama Magufuli alikwenda Kenya kama Serikali au alikuwa amekwenda kama rafiki. Hilo linatupa wasiwasi kwa kuwa hotuba yake ilionekana kama ametumwa na Serikali," alisema Wenje na kuongeza;
"Alichukua upande katika siasa za Kenya, alimsifia sana Odinga kwamba Tanzania wanampenda wakati kuna mikataba ya kimataifa inayokataza nchi nyingine kuingilia siasa za nchi nyingine kama ilivyoelezwa kwenye Rome Statute."
Wenje alisema kutokana na hilo ambalo Magufuli amefanya itakuwa mbaya kama mgombea wa chama kingine atashinda nchini Kenya kwa kuwa imeshajionyesha kuwa Tanzania inamuunga mkono Odinga.
"Waziri kuchukua upande kwenye siasa za Kenya ni hatari kwa taifa letu na Watanzania wanaishi nchini Kenya.
Itakuwa ni matatizo kwao na hata machafuko yakitokea Tanzania inaweza kuonekana ni chanzo," alisema Wenje.
Alisema ni muhimu Rais Kikwete akaeleza umma kama alimtuma Magufuli Kenya au la ili ujumbe alioutoa ujulikane ni wa nani kwa sababu kama alichokisema ni msimamo wa Serikali basi alitumwa na Rais Kikwete.
Alisema ni muhimu ikajulikana alitumwa na nani kwani taarifa ambazo Chadema inazo ni kwamba CCM hawakualikwa kwenye mkutano huo."Kama Kenyatta(Uhuru) akishinda humuoni kama italeta shida hapo baadaye? alihoji Wenje.
Alisema ni muhimu Serikali ikajua kwamba Rais wa Kenya atachaguliwa na Wakenya wenyewe na si vinginevyo.
Magufuli alipotafutwa kuzungumzia suala hilo hakupatikana kwa simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe ili atoe ufafanuzi hakujibu chochote.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, baada ya simu yake ya mkononi kutoita na taarifa zilizopatikana baadaye kutoka kwa mwandishi wake msaidizi, Irene Bwire, zilieleza kuwa alikuwa kwenye kikao cha baraza la Mawaziri.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape aling'aka akitaka waulizwe ODM ili waeleze walimwalika Magufuli kwa wadhifa upo.
"Sikiliza siwezi kuzungumzia suala la ... kama Wenje, kwani itakuwa tunafanya majibizano, we waeleze alipopigiwa Nape alisema waulizwe ODM walimwalika nani," alisema Nnauye na kuongeza;
Desemba 7 mwaka huu, Magufuli aliungana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsavangirai kumpigia debe Odinga, huku akieleza kuwa mwasiasa huyo mkongwe nchini Kenya ndiye anayestahili kuwa Rais wa nchi hiyo.
Alisema hakuna sababu zozote za zitakazowafanya Wakenya wasimchague Odinga kwa kuwa ni mcha mungu, hivyo wanatakiwa kujua hilo.
"Nataka kuwaambia Wakenya kwamba Odinga ni mcha Mungu, mnatakiwa kujua hilo. Kama mimi ningekuwa Mkenya ningempigia Odinga kura ili aongoze nchi. Lakini siruhusiwi hata kupiga kura basi nawambia msiache kumchagua huyu atawaongozeni vizuri,"alisema Magufuli.
Magufuli alisema katika wagombea wote waliojitokeza kuwania kiti cha urais nchini Kenya, hakuna anayemfikia Odinga na hiyo inaonyesha kuwa wakimchagua atawasaidia bila ubaguzi.
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia CHADEMA kimeitaka Serikali kutolea ufafanuzi suala la WazirI wa ujenzi Dr. John Magufuli kuhudhuria Sherehe za kutambulishwa kwa mgombea urais chama cha ODM Kenya Raila Odinga endapo suala hilo lina uhusiano wowote wa Kiserikali.
Mkurugenzi wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Ezekiel Wenje amesema kitendo cha waziri huyo kuhudhuria sherehe za kutambulishwa wa Raila kinatoa picha mbaya ya serikali ya Tanzania na Serikali ya Kenya iliyopo Madarakani kutokana na ushirikiano wa muda mrefu kati ya serikali hizo.
kwenye sentensi nyingine Wenje amesema Magufuli kupanda jukwaani kuanza kumnadi kiongozi wa ODM ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu za kimataifa ambapo amedai kwa mujibu wa kanuni za Umoja wa mataifa ni kosa kubwa Taifa moja kuingilia siasa za Taifa jingine hata kama hayo mataifa yanaushirikiano wowote.