On a Serious Note: Waziri wa Sheria anapokuwa hajui Katiba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

On a Serious Note: Waziri wa Sheria anapokuwa hajui Katiba!

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Pascal Mayalla, Apr 8, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 22,988
  Likes Received: 12,505
  Trophy Points: 280
  Kwa mlio na access,
  Watch TBC sasa, Waziri wa Sheria na Katiba, Mhe. Selina Kombani yuko live hewani, akiutetea Muswada wa Kuunda Tume ya Kukusanya Maoni ya katiba mpya!.

  Ameutetea kwa nguvu zake zote huo muswada jinsi ulivyo, ila pia amekubali, kuyapokeo maoni na mapendekezo yote yanayotolewa, ndio maana wametoa nafasi kwa wananchi kutoa maoni.

  Update:
  Wanabodi,

  Leo ndio mara yangu ya kwanza kumuona Waziri wetu wa Sheria, Mhe. Selina Kombani akihojiwa live kwenye kipindi cha Jambo, kinachorushwa na TBC-1 asubuhi hii.

  Alipokuwa akitetea mamlaka kubwa za rais kwenye utungaji wa katiba, Mhe. Kombani amesema, Tangu kutungwa kwa katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, Tanzania tumekuwa na katiba nyingine zaidi ya 5 ambazo zote process ndio hiyo hiyo kwa rais kuwa na mamlaka kubwa hivyo na zote zimesainiwa na rais, kitu ambacho sio kweli!.

  Mhe. Kombani wakati akizungumzia katiba hizo tano, alimaanisha marekebisho zaidi ya matano ya katiba, yaliyofanywa kwenye katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, na sio katiba tano kama alivyoeleza Mhe. Waziri.

  Usahihi ni kuwa Ile katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, ndio hiyo hiyo katiba iliyopo mpaka sasa, licha ya kufanyiwa marekebisho zaidi ya mara 5!. Marekebisho hayo hayabadilishi katiba na kuwa na katiba tano, katiba inabaki ni ile ile moja ya Mwaka 1977!.

  Mhe. Kombani, hakuishia hapo, katika utetezi wake kwa mamlaka ya rais pale aliposema, katiba hizo zote 5!, zimesainiwa na rais, kitu ambacho pia sio kweli!. Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, ilitokana na Bunge la Katiba 'Constituent Assembly' (Japo ni Bunge lile lile la chama kimoja lilijigeuza), ambalo ndilo liliipitisha katiba. Katiba ikishapitishwa na Bunge la Katiba, haisainiwi na rais, rais mwenyewe, anapata mamlaka toka kwenye katiba hiyo, ila kinachosainiwa na rais, ni yale marekebisho ya katiba!.

  Hivyo mpaka ninapoandika hapa, Waziri wetu wa Sheria, anaamini yuko right kabisa kutoa mamlaka kubwa zile kwa rais katika marekebisho ya katiba, kwa vile anaamini kinachofanyika sasa, ni marekebisho mengine ya katiba ile ile ya Tanzania ya Mwaka 1977 na sio process ya Uundwaji wa katiba mpya!.

  Waziri wa Sheria, anajua kuwa ni rais ndiye ameisaini Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, kitu ambacho sio kweli!.

  Japo sio kosa kubwa kwa mtu wa kawaida kuyaita marekebisho ya katiba kuwa ni katiba nyingine, lakini kwa Waziri wa Sheria, Live kwenye TV ya Taifa, kusema Tumekuwa na katiba 5 baada ya Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, ni uthibitisho kuwa tunaye Waziri wa Sheria Asiyejua Katiba!.

  Wasalaam.

  Pasco.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 22,988
  Likes Received: 12,505
  Trophy Points: 280
  Mhe Kombani, amekiri ni kweli rais amepewa madaraka makubwa sana kwenye muswada huo, lakini akasema madaraka hayo, yametokana na katiba yetu ya Tanzania ya mwaka 1977.
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,780
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo hii ni "vicious circle"?

  Nimesikia Mathias Chikawe BBC leo asubuhi anatetea pia muswada huu kwa "nguvu" zake zote!
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 9,810
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280
  watetee kwa nguvu zote, hata kwa nguvu ya risasi.

  all we need is Katiba. Katiba yetu, siyo yao.

  vinginevyo patachimbika.

  kama hawaamini, basi waendelee kucheza danadana na sheria mama ya vizazi vyetu.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,071
  Likes Received: 5,209
  Trophy Points: 280
  These people really don't get IT! the are incapable of getting it, and they would never get it even if you were to hammer it with a six inches nail in their heads. It is not about them, it is not about cosmetic change; it is about the fact that the people want to exercise their sovereignty by writing a new constitution. I mean, what is so hard to understand in that?
   
 6. markach

  markach Senior Member

  #6
  Apr 8, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Watanzania sasa wameamka na hawataki longo longo. nafikiri siku ya jana Tambwe hizi alijionea mwenyewe, kwa hiyo ngoja wapindishe tu, wataona mwisho wake. Hatukubali kwa nguzu zoteeeeeeeee
   
 7. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  Kuna lawyer jana kaniboa sana STAR TV.......ati Marekani wana katiba ya miaka 250 na hawabadili katiba iweje sisi tubadili yetu yenye miaka 34 tu?
   
 8. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2011
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,264
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  lakini pia kaelezea kuwa yale maeneo yaliyotajwa kama muungano, urais nk yanapaswa kutolewa maoni katika kuboresha tu na si kufifisha!
  maoni kwamba muungano ufe hayatapokelewa
  maoni kwamba uraisi ufe na tuweke usultani/ufalme pia hayatapokelewa

  nafikiri hayajafafanuliwa vizuri kwenye mswada ule
   
 9. B

  Bobby JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,673
  Likes Received: 171
  Trophy Points: 160
  Ni lawyer gani huyo anaboa kiasi hicho? Ni lazima awe zao la chuo cha kata kwani anachoongea ni upupu usio na mfano? Ni nani amemwambia ugomvi wetu ni umri wa katiba? Marekani hawabadili kwa kuwa yao iko valid kulingana na matakwa yao kama nchi? Sisi si copy ya Marekani kwamba wanachofanya wao ni lazima kiwe sahihi kwetu pia. Yetu haitufai kulingana na kilichomo kwenye sheria hiyo mama period. So kwake yeye kilichomo kwenye katiba yetu ni sahihi? Hivi wajinga kama hawa wanapataje audience kwenye hizi TV au ndio wametumwa? Inakera sana kwa kweli kwa the so called "msomi" kuongea utumbo kama huo on air.
   
 10. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 425
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Issue ni approach waliotumia wamarekani kupata katiba .....wao hawakuangalia katiba iwafae watu wa wakati wao tu bali walifikiria vizazi na vizazi. Sisi hapa watanzania naona walioko madarakani wana mkakati wa kuhakikisha katiba italinda maslahi yao badala ya kulinda maslahi ya watanzania wote. Kama katiba itajengwa kwa misingi mibovu si ajabu ikabadilishwa hata ndani ya muda mfupi.
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 9,810
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280
  hao ndio wanaitwa wasomi-uchwara.
   
 12. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  Tambwe jana kaumbuka sana.....sijui atamwabia nini Baba yake Makamba
   
 13. L

  LAT JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  mkuu... hivi ccm wanafanya makusudi au ni nini...? hivi hakuna mtu mwingine anayeweza kuwakilisha ccm katika masuala muhimu ya taifa pasipo Tambwe Hiza .... huu ni mzaha na dharau katika kuleta maendeleo ya nchi yetu
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Apr 8, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 22,988
  Likes Received: 12,505
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Leo ndio mara yangu ya kwanza kumuona Waziri wetu wa Sheria, Mhe. Selina Kombani akihojiwa live kwenye kipindi cha Jambo, kinachorushwa na TBC-1 asubuhi hii.

  Alipokuwa akitetea mamlaka kubwa za rais kwenye utungaji wa katiba, Mhe. Kombani amesema, Tangu kutungwa kwa katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, Tanzania tumekuwa na katiba nyingine5 ambazo zote process ndio hiyo hiyo kwa rais kuwa na mamlaka kubwa hivyo na zote zimesainiwa na rais, kitu ambacho sio kweli.

  Mhe. Kombani wakati akizungunzia katiba hizo tano, alimaanisha marekebisho ya matano ya katiba, yaliyofanywa kwenye katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, na sio katiba tano kama alivyoeleza Mhe. Waziri.

  Usahihi ni kuwa Ile katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, ndio hiyo katiba katiba iliyopo mpaka sasa, licha ya kufanyiwa marekebisho mara 5, marekebisho hayo hayabadilishi katiba na kuwa na katiba tano, katiba inabaki ni ile ile moja ya Mwaka 1977!.

  Mhe. Kombani, hakuishia hapo, katika utetezi wake kwa mamlaka ya rais pale aliposema, katiba hizo zote 5, zimesainiwa na rais, kitu ambacho pia sio kweli. Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, ilitokana na Bunge la Katiba 'Constituent Assembly' (Japo ni Bunge lile lile la chama kimoja lilijigeuza), ambalo ndilo liliipitisha katiba. Katiba ikishapitishwa na Bunge la Katiba, haisainiwi na rais, rais mwenyewe, anapata mamlaka toka kwenye katiba hiyo, ila kinachosainiwa na rais, ni yale marekebisho ya katiba.

  Hivyo mpaka ninapoandika hapa, Waziri wetu wa Sheria, anaamini yuko right kabisa kutoa mamlaka kubwa zile kwa rais katika marekebisho ya katiba, kwa vile anaamini kinachofanyika sasa, ni marekebisho mengine ya katiba ile ile ya Tanzania ya Mwaka 1977 na sio process ya Uuundwaji wa katiba mpya.

  Waziri wa Sheria, anajua kuwa ni rais ndiye ameisaini Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, kitu ambacho sio kweli.

  Japo sio kosa kubwa kwa mtu wa kawaida kuyaita marekebisho ya katiba kuwa ni katiba nyingine, lakini kwa Waziri wa Sheria, Live kwenye TV ya Taifa, kusema Tumekuwa na katiba 5 baada ya Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, ni uthibitisho kuwa tunaye Waziri wa Sheria Asiyejua Katiba.

  Wasalaam.

  Pasco.

  NB.(Somo la Katiba, ndio somo la kwanza kwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria, anapufundishwa 'What is Law?').
   
 15. M

  Marytina JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  secretary and the boss On the red carpet ndio anachoweza Selina
   
 16. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #16
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  Huyu mama aombe kubadilishwa wizara........hii haiwezi.......I wish Sitta was in place
   
 17. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #17
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hahahahhaaaaaaaa.
  Mama selina rudi jimbon ukalime mpungaaaa,eeeeeh hayo mambo ya sheria ni KIZUNGUMKUT
   
 18. L

  LAT JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  yaani acha tuu...hata Robert Manumba aliulizwa kwamba katiba ya tanzania inasemaje kuhusu madaraka ya jeshi la polisi ..akajibu kuwa yeye sio mtaalam wa katiba .... najiuliza katiba hii nani anatakiwa aijue...?
   
 19. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #19
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
   
 20. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #20
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 9,810
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280
  samehe baba samehe. ndiyo mawaziri wachapakazi na waadilifu tulioahidiwa na m*k*w*e*r*e

  huyu mama si ndiyo yule alisema serikali haina pesa?
   
Loading...