Ommy Dimpoz ni msanii bora zaidi ya Alikiba

Hi kwa wanaburudani wote.

Nakumbuka nikiwa mdogo baba aliwahi kuniambia. Mafanikio ya binadamu yoyote yanategemea vitu vikubwa vitatu:-
1. Bahati
2. Kipaji
3. Elimu
Akaniambia kati ya vyote bahati ndio inabeba vyote. Kama huna bahati hata uwe na kipaji vipi bado hutofanikiwa ipasavyo, hata uwe na elimu gani bado hutofanikiwa kulingana na elimu yako. Leo nikifikiria naona majibu kwa ukaribu.

Tuje katika mada. Hii ni opinion yangu na wala sio fact. Nawe unaweza kuwa na yako. Nimemfuatilia msanii Ommy Dimpoz kwa muda mrefu nimegundua jamaa yuko talented enough katika Bongoflava ila naona amekosa bahati. Jamaa anajua sana na hata anajua kubadilika kwendana na wakati, nikajaribu kuangalia sifa na ukubwa anaopewa msanii Alikiba nikaona hastahili alipaswa kuwa chini ya Dimpoz. Mwisho nikapata jibu Alikiba amepata bahati ya kushindanishwa na Diamond Platnumz, hii ni bahati ya mtende vinginevyo saa hizi tungemuongelea Sawa na Marlow.

Hebu angalia kwa mfano wimbo kata wa Dimpoz, ule wimbo angeupata Alikiba Dunia ingejuta, Clouds tungewakoma. Hata angeupata Diamond huu wimbo ungefikisha views 50m, ila mwenyewe sijui kafikisha 6m, hata sijui. Kabla hujabisha kaanze kusikiliza hits songs za Dimpoz zote, sikiliza zote za Alikiba halafu rudi na comment.

Sent using Jamii Forums mobile app

Yaani akili za kibongo unapokosea tu ninkufananisha, kulinganisha .. sijui nani kawaroga?

Amba ruttu, giggy money wana washabili wao damu hata useme nini wako tayari kufa ka ajili yao

Ali kiba ana nini mpaka umweke kundi moja au kimlinganisha na yule au huyu? He is simple ila influential sana.... Ali kiba kushindanishwa na diamond ni ujinga pia, tena umeuweka humu bila haya, ni kwa sababu ya akili ndogo

kiba wa nakshi nakshi mpaka mshumaa ni kiba yule yule, tabia ile ile ya kiswahili.. sio msanii yule ni mwanamuziki! Kwake kuimba ni furaha na faraja tu..huyu ataimba mpaka uzee wake

Ushawahi kwenda kwenye mgahawa ukakuta jamaa anauza maandazi 20kila siku na anaridhika na hajiongezi wala hapapariki na wengine KAMA UTAKAVYO

Wako wengi tu kwa kipaji wanampita kiba (kama unawaza kushindana) wako akina onesix, aten, benson, cheed, barnaba, n.k lakini pia ndani ya moyo wako unajua kuna kiki, kupumbazwa na wengi kama kipaji wamemzidi diamond bya far million times better. dunia haiko hivyo... Kutoboa kunahitaji ujanja mwingi na jitihada za kudumu kama afanyavyo diamond

Labda utueleze kilichofanya umseme kiba kati ya wengi ni kipi? Nini hasa kimekuvuta? Kwa nini haikuwa rahisi kumu ignore tu?
 
Nakuunga mkono kwasasa ommy dimpoz anafanya mziki unaopendwa na wengi na ngoma zake zinafanya vizuri kuliko za alikiba ila kwa maana ya kipaji kiba ana kipaji kikubwa kushinda ommy dimpoz

Ommy dimpoz anafanya vizuri kuliko hata diamond
 
Huu Mshumaa umeuonaje sokoni? Alikiba yuko static sana. Huu wakati nyimbo zinazotoboa ni za kuchezeka zaidi ila Alikiba alitambui kubalance nyimbo zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni shabiki wa Kiba? Kama jibu ni hapana basi ungenyamaza tu sababu mashabiki wake tunapenda hizo nyimbo zake zisizochezeka usilazimishe nyekundu kua njano,
Hizo nyimbo za kwioo kwioo tunawaachia nyie wakata viuno.

The best Medicine of Corona is to Stay Home.
 
Ommy dimpoz anafanya vizuri kuliko hata diamond
Anzisha Uzi wake alafu uone Kama Kuna mtu atakuunga mkono hapa hatupo kwaajili ya ushabiki hapa tunaongea facts nikikuuliza vigezo ulivyotumia kusema ngoma za ommy dimpoz zinafanya vizuri hutanipa jibu.
 
Huyo dimpoz mwemyew ukimuuliza kati yake na kiba nan yuko vzuri atakuambia...

Acheni stry za kahawa, ifike kipindi muwape wa2 heshima zao sio mpk wafe... ku mantain kufanya mziki kwa miaka zaidi ya 15 sio kazi rahs.

Tz hii wakumfikia kiba ni wachache sana... na mziki umegawanyika sehemu nyingi sio kila mziki uwe na vibes kama za platnumz yan za kuchezeka..

Mbn akina ben pol na jux hamsemi waimbe nyimbo kama *kata*!

Kila mtu ana radha yake... mimi binafsi nikitaka nyimbo za kuchezeka nitamskiliza platnumz, pia nikitaka nyimbo za hisia, za kufunza na pia kuchezeka basi nitaenda kwa kiba.

Muzik ni mood, na hakuna anaefanya aina zote za mziki hvyo basi kila m2 mzuri sehemu yake.... siku ukijua hili utaacha ku generalise aina za mzki na kushindanisha wanamzk kipuuz

...
Nadhani mpaka hapa Thread ingefungwa na mtoa mada amuombe radhi King Kiba.

The best Medicine of Corona is to Stay Home.
 
Yaani akili za kibongo unapokosea tu ninkufananisha, kulinganisha .. sijui nani kawaroga?

Amba ruttu, giggy money wana washabili wao damu hata useme nini wako tayari kufa ka ajili yao

Ali kiba ana nini mpaka umweke kundi moja au kimlinganisha na yule au huyu? He is simple ila influential sana.... Ali kiba kushindanishwa na diamond ni ujinga pia, tena umeuweka humu bila haya, ni kwa sababu ya akili ndogo

kiba wa nakshi nakshi mpaka mshumaa ni kiba yule yule, tabia ile ile ya kiswahili.. sio msanii yule ni mwanamuziki! Kwake kuimba ni furaha na faraja tu..huyu ataimba mpaka uzee wake

Ushawahi kwenda kwenye mgahawa ukakuta jamaa anauza maandazi 20kila siku na anaridhika na hajiongezi wala hapapariki na wengine KAMA UTAKAVYO

Wako wengi tu kwa kipaji wanampita kiba (kama unawaza kushindana) wako akina onesix, aten, benson, cheed, barnaba, n.k lakini pia ndani ya moyo wako unajua kuna kiki, kupumbazwa na wengi kama kipaji wamemzidi diamond bya far million times better. dunia haiko hivyo... Kutoboa kunahitaji ujanja mwingi na jitihada za kudumu kama afanyavyo diamond

Labda utueleze kilichofanya umseme kiba kati ya wengi ni kipi? Nini hasa kimekuvuta? Kwa nini haikuwa rahisi kumu ignore tu?
Hapa umeongea point Sana.
 
Niwe mkweli tu.
Dimpoz anajitahidi mnoo kwa sasa..
Kizuri zaidi anabadilika badilika..

Alikiba mpka aje atoe nyimbo ni mpka harmonize avae shat kwenye video
 
Yaani akili za kibongo unapokosea tu ninkufananisha, kulinganisha .. sijui nani kawaroga?

Amba ruttu, giggy money wana washabili wao damu hata useme nini wako tayari kufa ka ajili yao

Ali kiba ana nini mpaka umweke kundi moja au kimlinganisha na yule au huyu? He is simple ila influential sana.... Ali kiba kushindanishwa na diamond ni ujinga pia, tena umeuweka humu bila haya, ni kwa sababu ya akili ndogo

kiba wa nakshi nakshi mpaka mshumaa ni kiba yule yule, tabia ile ile ya kiswahili.. sio msanii yule ni mwanamuziki! Kwake kuimba ni furaha na faraja tu..huyu ataimba mpaka uzee wake

Ushawahi kwenda kwenye mgahawa ukakuta jamaa anauza maandazi 20kila siku na anaridhika na hajiongezi wala hapapariki na wengine KAMA UTAKAVYO

Wako wengi tu kwa kipaji wanampita kiba (kama unawaza kushindana) wako akina onesix, aten, benson, cheed, barnaba, n.k lakini pia ndani ya moyo wako unajua kuna kiki, kupumbazwa na wengi kama kipaji wamemzidi diamond bya far million times better. dunia haiko hivyo... Kutoboa kunahitaji ujanja mwingi na jitihada za kudumu kama afanyavyo diamond

Labda utueleze kilichofanya umseme kiba kati ya wengi ni kipi? Nini hasa kimekuvuta? Kwa nini haikuwa rahisi kumu ignore tu?
Pole mkuu Waberoya Mimi nimesema ni opinion yangu, sikujua kama Alikiba incomparable. Huwa napenda ubishe kwa evidence. Pole ila kama unaamini yeye music kwake ni hobby na sio professional unajidanganya au unakwepa tatizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom