Ombwe/pengo kati ya vijana na historia ya nchi yetu; ni kwa manufaa ya nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombwe/pengo kati ya vijana na historia ya nchi yetu; ni kwa manufaa ya nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NewDawnTz, Mar 10, 2011.

 1. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Heshima na amani kwenu ndugu zangu wana-JF,

  Kwanza nitoe heshima zangu za pekee kwa watu wa rika lililosogea na wazee ndani ya JF ambao wamekuwa wakitufungua macho yetu vijana wengi katika kufahamu mambo mengi ambayo yamefichika juu ya ukweli na uwazi wa historia ya nchi yetu.
  Ni suala lisilopingika ya kuwa Vijana wengi wa Tanzania historia ya nchi yetu imetutupa mkono. Liko wazi, kaa nao waulize utagundua LIKO OMBWE KATI YAO NA HISTORIA SAHIHI YA NCHI YAO.

  Niweke wazi imani yangu juu ya historia SAHIHI na maendeleo. Imani yangu ni kuwa maendeleo ya taifa lolote huweza kuhamishwa na kupiga hatua kizazi hadi kizazi kulingana na historia sahihi za nchi husika kupitishwa kati ya kizazi hadi kizazi. Maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania ya leo na kesho yanategemea kwa asilimia kubwa historia ya maendeleo ya Tanganyika katika msingi wa falsafa, itikadi na maamuzi ya namna ya kukuza uchumi yaliyochukuliwa katika zama za Tanganyika (tuseme na Zanzibar pia). Hali ni hiyo hiyo pia katika maendeleo ya kisiasi, kijamii na katika nyanja nyingine.

  Naamini kama historia inawekwa wazi na kupasishwa kati ya kizazi hadi kizazi ni rahisi kwa jamii husika kupiga hatua. Nchi inayosahau au kuficha historia yake haiwezi kupiga hatua na badala yake inajichimbia kaburi la kupotea kifalsafa, kimkakati na hata kimipango na kisha kupoteza dira. Je, hii si sababu ya nchi yetu leo kuanza kupoteza Dira kwa kuwa na asilimia kubwa ya nguvu kazi yake (Vijana) ambao hawaijui historia ya nchi yao? Kutopasisha historia sahihi na makini kwa vizazi ni kuipoteza nchi kwa kukosa dira…………….Ndivyo ninavyoamini.

  Ukweli ulio wazi ni kuwa vijana wengi (sio wote tafadhali) hawaijui historia ya nchi yetu ilikotoka. Hawajui historia ya nchi katika maendeleo ya miundombinu ikiwamo barabara na reli, hawajui ukweli na uhalisi wa harakati za ukombozi wa nchi yetu, hawajui kwa undani historia ya mahusiano ya kijamii; wengi hawajui historia ya nchi hii katika falsafa na mikakati ya uendeshaji uchumi na dola/siasa. MADHARA YAKE yanaweza kuonekana sasa kwa wanaochunguza kwa undani, lakini naamini yataonekana zaidi hapo BAADAE KWA KUWA NA KIZAZI AMBACHO HAKIJAPASISHWA HISTORIA SAHIHI NA KAMILIFU KIUSAWIA na hata kuutupa uthamani wa utu wao pembeni....Historia hujenga kujithamini na kuutunza utu kwa falsafa sahihi zilizopasishwa kizazi kimoja hadi vizazi vingine.

  Kwa muda niliokaa hapa JF na kusoma mambo mengi yaliyofichwa juu ya historia ya Tanganyika na Zanzibar naweza kukiri ya kuwa VIJANA HATUTENDEWI HAKI KUFICHWA HISTORIA.

  Najua wako watakaosema ni uvivu na uzembe wa kutokufuatili. Lakini ni ukweli usiopingika ya kuwa ukweli wa HISTORIA YA TANGANYIKA YANGU KWA ASILIMIA KUBWA UMEFICHWA… ni mpaka uitafute kwa tochi kama unatafuta sindani iliyoanguka kwenye jumba lenye kiza kinene…HISTORIA HAITAFUTWI TU, HISTORIA HUPASISHWA NA WALIOISHUHUDIA NA KUISHIRIKI

  Shule gani utafundishwa juu ya Abdulwahid Sykes au John Okelo? SIJUI NI NANI AMEDHAMIRIA KUFICHA UKWELI HUU, ila ni wazi HAKUNA DHAMIRA NA NIA YA KUTAKA HISTORIA SAHIHI KUPASISHWA KATI YA VIZAZI HADI VIZAZI.


  Ninasikia viko vitabu vilivyoandikwa kuweka usahihi wa kumbukumbu za ukombozi wa taifa letu na harakati nyingine za kisiasa na kiuchumi, lakini ni kwa nini ni vigumu kuvipata vitabu hivi pengine kuliko vile vinavyoelezea historia na maisha binafsi ya Kikwete "Chaguo la Mungu na Ukombozi wa Tanzania"?

  Ni mengi ninayoweza kusema, kujiuliza au kutolea mifano, lakini maswali yangu makubwa ni haya:-

  • Je ni kwa manufaa ya nani historia ya nchi inafichwa na haiwekwi wazi kiusawia?

  • Tatizo ni nini katika kufundisha usahihi na uhalisi wa historia ya nchi yetu?

  • Ni nini tunaweza kufanya ili kulikomboa taifa letu na umbumbumbu wa kuitupa historia yetu?

  • Je wazee wetu mnachukua hatua gani zaidi

  Kwa mtazamo wangu


  • Wizara husika ipitie upya mtaala wa historia na kuhakikisha vijana wanafundishwa historia ya kweli ya nchi yetu kwa mapana yake. Isingoje mpaka watu kuja ku-specialize wakiwa kwenye ngazi ya juu ya elimu lakini msisitizo uwe toka katika ngazi za awali kabisa ili kuondoa pengo la Watanzania/Watanganyika katika kufahamu wapi tumetoka….NI URITHI NA HAZINA MUHIMU KAMA ILIVYO MBUGA ZA WANYAMA

  • Pia wazee wangu mkae chini muizindue serikali usingizini, mtengeneze kitabu kitakachokuwa kimebeba na kuweka wazi historia ya nchi yetu kwa usahihi wake
  Vijana wafundishwe historia kwa usahihi, iwasaidie kujenga NIDHAMU kwa nchi yetu, KUJITUMA katika kuleta maendeleo na zaidi KUWA na mipango inayozingatia historia sahihi za nchi yetu.

  BILA HISTORIA SAHIHI KUPASISHWA KATI YA VIZAZI, TUNAIUA JAMII YETU KIMYAKIMYA
   
 2. n

  nyantella JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  NewDawnTz!
  Ni kweli vijana wengi hawaelewi historia ya nchi yetu na kwa sababu mbali mbali. Ukiangalia kwa makini utagundua kwamba historia ya nchi yetu kama zilivyo nchi nyingi za kiafrica ukiacha vile vipindi mabadiliko toka stone age hadi iron age, inaanzia wakati wa utawala wa machifu mbali mbali na baadae biashara ya utumwa, baadae ukoloni na baade uhuru. kwa bahati mbaya sehemu kubwa haiko katika maandishi ukiachilia mbali kipindi cha wakati wa ukoloni uhuru na baada ya uhuru.
  Mimi si mtaalamu wa historia ila kwa maelezo zaidi tuna jumba la makumbusho pale mtaa wa Shaaban Robert, karibu na IFM. Nafikiri historia, unayotaka kuifahamu ni ile ya kabla na baada ya ya uhuru. kama ni kweli, basi hii ipo kwenye maandishi, na vitabu vipo just read. unajua kuna ile notion kwamba ukitaka kuficha kitu Waafrica wasikione, kiweke katika vitabu, we are not good readers of books. kwa upande wa nci yetu historia ya mapambano ya uhuru inabebwa na vyama vya kupigania uhuru vya wakati huo, TANU bara na ASP visiwani. kwa hiyo ukifahamu historia ya vyama hivyo kwa kiasi fulani utakua umeipata historia ya nchi yetu kuanzia wakati huo hadi sasa. Tatizo litakua kwamba upo chama gani, lakini kama issue ni kujua historia ya nchi yetu ni vyema uka swallow your pride and read anything kinacho husu nchi yako kibaya au kizuri. you may ask why,the reason is that history is history!!, mbaya au nzuri!!! fahamu kwamba mbali na ubaya wa Adolf Hitler, bado NAZI ni part and percel of the current Germany and even watu wanasoma Mein Kamf. so read any think that makes the history of your country, continent and the World history if you can.
  kitu kingine ambacho vijana wa leo wa kitanzania wanakikosa ni JKT, hii ilikua nguzo ya umoja wa taifa hili tulijifunza mengi huko na JKT ilitufanya tukawa real patriotic kwa nchi yetu.
   
 3. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Kaka ni kweli hivi vitu baadhi vipo kwenye maandishi lakini sio vyote ambavyo vipo kwenye maandishi.

  Kwa nchi inayotaka kujijenga katika misingi imara sio suala tu ya kuweka kwenye maanishi ila ni itajenga mfumo ulio wazi na mpana zaidi kuhakikisha vijana wake wengi wanaielewa historia hiyo.

  Kwa mfano ni kweli jumba la makumbusho lina badhi ya kumbukumbu za muhimu lakini jiulize ni wangapi wenye uwezo wa kufika huko
  kwenye jumba la makumbusho? Ndio maana nimesema kwa wanaotaka kujenga watawahamasisha vijana wao kupitia mfumo maalum kama kwa namna ya mitaala ya elimu na baada ya hapo inawajengea ushawishi kutafuta zaidi.

  Maana yangu kubwa ni kutaka jamii yote ya Tanzania kujua umuhimu ulioko katika kupasisha historia ya nchi yetu kuanzia harakati na juhudi za kimaendeleo kabla ya uhuru kwa kuhakikisha kila kijana wa kitanzania anapata fursa hii kwa mahali alipo.

  Mitaala ya elimu na mifumo mingine katika jamii itasaidia lakini ni lazima kwanza wote tukubali kuwa kuna pengo kubwa kati ya historia ya nchi na vizazi hadi vizazi na kisha tuamue sasa wakati ufike historia hiyo iwekwe wazi na ipasishwe kwa vizazi

  Kwenye red ninakubali kabisa...huu nao ni mfumo mwingine wa muhimu wa kusaidia...hapa itasaidia sio tu kujifunza mabadiliko ya kihistoria katika mfumo wa kisiasa tu kwa jumla bali pia katika jamii na uchumi...labda linapaswa kufikiriwa na kupewa uzito zaidi
   
Loading...