Ombwe la Uongozi Tanzania: Siasa zimeshika hatamu, Ubunge ndio kila kitu

IMG-20200717-WA0069.jpg
 
Kila jambo huwa na asili... Yaani chanzo.. Hata mtu asili yake ni manii.

Kosa moja kubwa kabisa tulilolifanya hapo nyuma wakati wa Benjamin Mkapa ni kuipa taaluma kisogo na kuipa SIASA thamani kubwa kuliko uhalisia wake

Jambo hilo halikuwahi kurekebishwa na yeyote yule bali ndio kwanza lilizidi kupaliliwa na kuwekewa mbolea.... Matokeo yake ni haya sasa.

Tuko kwenye kilele cha Kuisigina taaluma, kuihujumu na kuifanya si lolote si chochote mbele ya mwanasiasa aliyefeli masomo yote darasani mpaka lile la lugha yake mwenyewe

Minofu na vinono vya SIASA kipandio chake ni cheo cha ubunge. Nafasi ya kuchaguliwa na wananchi yenye uhakika wa kula mema ya nchi kwa kipindi cha miaka mitano bila shida kabisa

Pale unapofanikiwa tu kuipata nafasi hii adhimu ya utumishi uliotukuka basi hapo hapo jina lako linabadilika na kuitwa MHESHIMIWA. Hapa utajihakikishia kibunda cha million kumi tasilimu kila mwezi kwa kazi unayofanya kwa starehe mno. Na baada ya miaka mitano unaondoka na kiinua mgongo cha milioni mia mbili.

Hapo ni ukiwa na kipandio cha ubunge tuu.. Ulibahatika kuukwaa uwaziri ama unaibu wake.. Pepo yako ni hapa hapa duniani

Huko kwenye ubunge kuna fursa na marupurupu ya kila aina tofauti kabisa na kwenye utumishi mwingine wenye suluba na changamoto za kila aina..

Leo hii ubunge sio utumishi wa wananchi tena.. Leo hii ubunge sio kazi ya mkulima na mfanyakazi wa kawaida
Leo hii ubunge ni nafasi ghali, ngumu kupata na ya watu wenye maisha yao... Yaani mambo safi... Kama
Wakurugenzi mbalimbali
Wakuu wa mikoa
Wakuu wa wilaya
Wafanyabiashara wakubwa
Wasanii wakubwa
Watu maarufu nknk
Yaani kupata Ubungo sasa hivi ni lazima uwe fulani kwenye jamii la sivyo utabaki kuwa mpenzi msindikizaji tuu

Wimbi la wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na wakurugenzi kukimbilia ubunge ni kwamba hawana uhakika na kesho yao kwenye nafasi zao.. Lolote muda wowote linaweza kutokea kama aliyekuteua akichafukwa... Ila wanajua kwa hakika kwenye ubunge ni mkataba.. Tena wa miaka mitano

Inashangaza mno kuwa hata wasanii mbalimbali wanaacha kukuza vipaji na vipawa vyao wanakimbilia kuwa wabunge.. Wanashindwa kabisa kujua kuwa ndani ya miaka mitano wakitumikia vema vipaji vyao wanaweza kumake kuliko hata hao wabunge

Nao wamekumbwa na ubinafsi ule wa wengine wasioridhika na walichonacho... Hivi mtu kama Kimei anataka ubunge wa nini? Kwanini asiwaachie damu changa ioneshe uwezo wao? Mzee Wasira bado anataka ubunge... Dah.

Hakika tuna ombwe kubwa la uongozi.. Sasa hivi hata wanataaluma wanaachana na taaluma zao na kukimbilia ubunge
Je tutafika?
Hata mgombea urais wa Act wazalendo anatamani kugombea ubunge wa Magogoni
 
... Hivi mtu kama Kimei anataka ubunge wa nini? Kwanini asiwaachie damu changa ioneshe uwezo wao? Mzee Wasira bado anataka ubunge... Dah.
Wassira alianza kula bata la uwaziri tangu enzi za Julius Nyerere. Hili ni funzo kwa vijana kujifunza kuinvest mapema. Nadhani pia iwepo sheria inayomzuia mtu kuwa mbunge kwa vipindi vinne mfululizo. Pia kuna haja ya kuyaangalia upya maslahi ya wafanyakazi wengine (RAS, DAS, RC, DC, DED etc) pamoja na assurance ya ajira zao ili kuepuka hii dhahama ya teuzi kila kukicha
 
Dr. Charles Kimei tunamhitaji sana akasaidiane na akina Dk.Philip Mpango kwenye mambo ya fedha na uchumi, sera za sekta binafsi , uwekezaji n.k.

Input yake inaweza kuwa sana kwa taifa letu. NI hasara kuwa na bunge walilojaa akina Kibajaji, ni afadhari tuwe na akina Msukuma watachangia kuhusu kuimarisha sekta binafsi maana angalau anaijua sana biashara kuliko wasomi wa biashara na uchumi ngazi za uzamivu.
Politicians” who don’t read:
-can parrot, but can’t produce (ideas)
-can mimick, but can’t mentor
-can imitate, but can’t innovate
-can chant, but can’t sing
-can rant, but can’t rhyme
SO:in this day&age of global neo-fascism if you want to be a succesful politician, DON’T read.
 
Maslahi ya mbunge Tanzania

1.Mshahara 3.8M kwa mwezi
2.Posho mwezi 8M
3.Posho kikao 240k
4.Kujikimu siku 120k
5.Pensheni 240M baada ya 5yrs
6.Bima ya afya daraja la kwanza wewe&familia.
7.Safari za nje
8.Mshahara bila makato ya Bima ya afya wala mifuko ya hifadhi za jamii.
Kwa malipo haya kwann wasomi wasikimbilie SIASA
 
Kwakuwa bungeni ndio chombo pekee cha kuwasemea wananchi kupitia wabunge wao kama wawakilishi kuna haja sasa ya kuwa na mabunge mawili.. Hili lisionekane geni machoni petu.. Nchi nyingi tu zina mfumo wa mabunge mawili uingereza ikiwa mojawapo

1. Tuendelee kuwa na hili bunge la fadhila, kujipendekeza kujikomba nk.. Bunge la wasema chochote ili mradi tu mtu aonekane kaongea
Bunge la wachumia tumbo
Bunge la kulindana na kupeana michongo
Bunge la kulinda maslahi ya kibiashara, uwekezaji na mambo ya siri

2. Tuwe na bunge jipya litakalojumuisha wanataaluma na Wataalam wa fani mbalimbali
Wana uchumi
Wana sheria
Madaktari
Walimu na wakufunzi
Wana usalama
Wana sayansi mbalimbali
Wana historia
Wataalam wa mambo ya giza
Wafugaji
Wakulima
Wanadiplomasia nknk

👍

HOUSE OF LORDS - Nyumba ya Mabwana ni Bunge la pili la Uingereza. lina jukumu muhimu katika kutengeneza na kupanga sheria
Hawa wote kwanza ni matajiri wakubwa, wanaitwa Aristocracy ambao ni daraja la ju la kijamii (mabwanyenye) ambalo jamii fulani inazingatia agizo lake la juu zaidi. Katika majimbo mengi, aristocracy ilijumuisha jamii ya juu ya watu na kiwango cha kurithi na majina na kulambana ili kupata ulaji.

HOUSE OF COMMONS - Nyumba ya Wazawa ni Bunge lililochaguliwa kidemokrasia ya Bunge la Uingereza, inayohusika na kutunga sheria na kuangalia kazi ya Serikali, Nyumba ya Wazawa, ambayo kawaida hujulikana kama Commons, ndio nyumba ya chini ikihusisha kila mwananchi mwenye sifa za kugombea na kukubalika na wananchi.
 
Maslahi ya mbunge Tanzania

1.Mshahara 3.8M kwa mwezi
2.Posho mwezi 8M
3.Posho kikao 240k
4.Kujikimu siku 120k
5.Pensheni 240M baada ya 5yrs
6.Bima ya afya daraja la kwanza wewe&familia.
7.Safari za nje
8.Mshahara bila makato ya Bima ya afya wala mifuko ya hifadhi za jamii.
Aiseeee !!
 
Kila jambo huwa na asili... Yaani chanzo.. Hata mtu asili yake ni manii.

Kosa moja kubwa kabisa tulilolifanya hapo nyuma wakati wa Benjamin Mkapa ni kuipa taaluma kisogo na kuipa SIASA thamani kubwa kuliko uhalisia wake

Jambo hilo halikuwahi kurekebishwa na yeyote yule bali ndio kwanza lilizidi kupaliliwa na kuwekewa mbolea.... Matokeo yake ni haya sasa.

Tuko kwenye kilele cha Kuisigina taaluma, kuihujumu na kuifanya si lolote si chochote mbele ya mwanasiasa aliyefeli masomo yote darasani mpaka lile la lugha yake mwenyewe

Minofu na vinono vya SIASA kipandio chake ni cheo cha ubunge. Nafasi ya kuchaguliwa na wananchi yenye uhakika wa kula mema ya nchi kwa kipindi cha miaka mitano bila shida kabisa

Pale unapofanikiwa tu kuipata nafasi hii adhimu ya utumishi uliotukuka basi hapo hapo jina lako linabadilika na kuitwa MHESHIMIWA. Hapa utajihakikishia kibunda cha million kumi tasilimu kila mwezi kwa kazi unayofanya kwa starehe mno. Na baada ya miaka mitano unaondoka na kiinua mgongo cha milioni mia mbili.

Hapo ni ukiwa na kipandio cha ubunge tuu.. Ulibahatika kuukwaa uwaziri ama unaibu wake.. Pepo yako ni hapa hapa duniani

Huko kwenye ubunge kuna fursa na marupurupu ya kila aina tofauti kabisa na kwenye utumishi mwingine wenye suluba na changamoto za kila aina..

Leo hii ubunge sio utumishi wa wananchi tena.. Leo hii ubunge sio kazi ya mkulima na mfanyakazi wa kawaida
Leo hii ubunge ni nafasi ghali, ngumu kupata na ya watu wenye maisha yao... Yaani mambo safi... Kama
Wakurugenzi mbalimbali
Wakuu wa mikoa
Wakuu wa wilaya
Wafanyabiashara wakubwa
Wasanii wakubwa
Watu maarufu nknk
Yaani kupata Ubungo sasa hivi ni lazima uwe fulani kwenye jamii la sivyo utabaki kuwa mpenzi msindikizaji tuu

Wimbi la wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na wakurugenzi kukimbilia ubunge ni kwamba hawana uhakika na kesho yao kwenye nafasi zao.. Lolote muda wowote linaweza kutokea kama aliyekuteua akichafukwa... Ila wanajua kwa hakika kwenye ubunge ni mkataba.. Tena wa miaka mitano

Inashangaza mno kuwa hata wasanii mbalimbali wanaacha kukuza vipaji na vipawa vyao wanakimbilia kuwa wabunge.. Wanashindwa kabisa kujua kuwa ndani ya miaka mitano wakitumikia vema vipaji vyao wanaweza kumake kuliko hata hao wabunge

Nao wamekumbwa na ubinafsi ule wa wengine wasioridhika na walichonacho... Hivi mtu kama Kimei anataka ubunge wa nini? Kwanini asiwaachie damu changa ioneshe uwezo wao? Mzee Wasira bado anataka ubunge... Dah.

Hakika tuna ombwe kubwa la uongozi.. Sasa hivi hata wanataaluma wanaachana na taaluma zao na kukimbilia ubunge
Je tutafika?
Olesendeka!?? Mwanri?!!! Too much!
Hakika nimechoka!
Km Mungu aishivyo hakuna kupita wawaachie vijana!

JESUS IS LORD
 
*Sasa hivi !!!!!!!!!!!mgombea unaweza kwenda kwa mganga ukakuta mganga nae kachukua form, kwa ajili ya kugombea jimbo hilohilo unalotaka kugombea... *
 
Kinachowapeleka huko sio kingine, maslahi. Posho na mishahara Yao ni mikubwa mno, pensheni zao ni kubwa kuliko. Ndio maana mtu yupo tayari kuacha kazi ya kufundisha chuo kikuu pale mlimani na kwenda kutukana majukwaani.

Ningekuwa na nafasi hakika pensheni ya miaka mitano (240mil) ingeshuka hadi 50mil, mishahara ingekuwa 2mil with little add-ons. Watu sasa ni ubunge tu hakuna kufikiria kingine.
 
Dr. Charles Kimei tunamhitaji sana akasaidiane na akina Dk.Philip Mpango kwenye mambo ya fedha na uchumi, sera za sekta binafsi , uwekezaji n.k.

Input yake inaweza kuwa sana kwa taifa letu. NI hasara kuwa na bunge walilojaa akina Kibajaji, ni afadhari tuwe na akina Msukuma watachangia kuhusu kuimarisha sekta binafsi maana angalau anaijua sana biashara kuliko wasomi wa biashara na uchumi ngazi za uzamivu.
Sio lazima awe mbunge ili asaidie wizara ya fedha. Serikali inaweza mwajiri kama mtaalam mshauri wa maeneo ambayo jamaa ni mtaalam. By the way waziri sio mtendaji, mtendaji ni katibu mkuu wa wizara and for that case kimei angeleta matunda zaidi kuwa katibu mkuu au mtaalam mshauri. Alifaa kuwa hata Mtendaji Mkuu wa BOT maana alionesha uthubutu mkubwa sana wakati akiwa CRDB, aliichukua ikiwa hohehahe lkn ameacha ikiwa miongoni mwa benki bora kabisa nchini
 
Kuna ushauri mwingine lazima ukatoe kwenye vikao vya siri chini ya viapo ukiwa na wafanya maamuzi au ukiwa mfanya maamuzi.
Huko kwenye ubunge ni moja ya njia ya kufkia huko.

Pia ubunge hukupa fursa ya moja kwa moja kushiriki maamuzi mengi hata ya kutunga sheria au kudai maendeleo flani.
Sio lazima kuwa mbunge ili kufanya hayo na kama kweli anahitajika serikali itamchukua tu.Tena huyu mzee Magu aliisha mhakikishia kabisa....hivyo sioni haja ya yeye kugombea ubunge...Ni tamaa tu na kuwazibia vijana kupata experience ya uongozi...hamna jipya...
 
IMG-20200717-WA0048.jpg
 
Mtu kama Kimei ni asset kwenye hii nchi jmn
Binafsi i wish apate afanye mambo zaidi..nani asiejua uwezo wake?.

Kemeeni watu ambao hatujaona impact yao yoyote kabla ya kutia nia
Hao ndo wanakuja na njaa zao kwanza hadi washibe ndo watende mema

KIMEI anaweza kuaminika atleast kuwa na nia ya utumishi mwema wa umma mana pesa na madaraka anayo long kipindi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom