Ombwe la Uongozi Tanzania: Siasa zimeshika hatamu, Ubunge ndio kila kitu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
146,399
2,000
Kila jambo huwa na asili... Yaani chanzo.. Hata mtu asili yake ni manii.

Kosa moja kubwa kabisa tulilolifanya hapo nyuma wakati wa Benjamin Mkapa ni kuipa taaluma kisogo na kuipa SIASA thamani kubwa kuliko uhalisia wake

Jambo hilo halikuwahi kurekebishwa na yeyote yule bali ndio kwanza lilizidi kupaliliwa na kuwekewa mbolea.... Matokeo yake ni haya sasa.

Tuko kwenye kilele cha Kuisigina taaluma, kuihujumu na kuifanya si lolote si chochote mbele ya mwanasiasa aliyefeli masomo yote darasani mpaka lile la lugha yake mwenyewe

Minofu na vinono vya SIASA kipandio chake ni cheo cha ubunge. Nafasi ya kuchaguliwa na wananchi yenye uhakika wa kula mema ya nchi kwa kipindi cha miaka mitano bila shida kabisa

Pale unapofanikiwa tu kuipata nafasi hii adhimu ya utumishi uliotukuka basi hapo hapo jina lako linabadilika na kuitwa MHESHIMIWA. Hapa utajihakikishia kibunda cha million kumi tasilimu kila mwezi kwa kazi unayofanya kwa starehe mno. Na baada ya miaka mitano unaondoka na kiinua mgongo cha milioni mia mbili.

Hapo ni ukiwa na kipandio cha ubunge tuu.. Ulibahatika kuukwaa uwaziri ama unaibu wake.. Pepo yako ni hapa hapa duniani

Huko kwenye ubunge kuna fursa na marupurupu ya kila aina tofauti kabisa na kwenye utumishi mwingine wenye suluba na changamoto za kila aina..

Leo hii ubunge sio utumishi wa wananchi tena.. Leo hii ubunge sio kazi ya mkulima na mfanyakazi wa kawaida
Leo hii ubunge ni nafasi ghali, ngumu kupata na ya watu wenye maisha yao... Yaani mambo safi... Kama
Wakurugenzi mbalimbali
Wakuu wa mikoa
Wakuu wa wilaya
Wafanyabiashara wakubwa
Wasanii wakubwa
Watu maarufu nknk
Yaani kupata Ubungo sasa hivi ni lazima uwe fulani kwenye jamii la sivyo utabaki kuwa mpenzi msindikizaji tuu

Wimbi la wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na wakurugenzi kukimbilia ubunge ni kwamba hawana uhakika na kesho yao kwenye nafasi zao.. Lolote muda wowote linaweza kutokea kama aliyekuteua akichafukwa... Ila wanajua kwa hakika kwenye ubunge ni mkataba.. Tena wa miaka mitano

Inashangaza mno kuwa hata wasanii mbalimbali wanaacha kukuza vipaji na vipawa vyao wanakimbilia kuwa wabunge.. Wanashindwa kabisa kujua kuwa ndani ya miaka mitano wakitumikia vema vipaji vyao wanaweza kumake kuliko hata hao wabunge

Nao wamekumbwa na ubinafsi ule wa wengine wasioridhika na walichonacho... Hivi mtu kama Kimei anataka ubunge wa nini? Kwanini asiwaachie damu changa ioneshe uwezo wao? Mzee Wasira bado anataka ubunge... Dah.

Hakika tuna ombwe kubwa la uongozi.. Sasa hivi hata wanataaluma wanaachana na taaluma zao na kukimbilia ubunge
Je tutafika?
 
Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,880
2,000
Dr. Charles Kimei tunamhitaji sana akasaidiane na akina Dk.Philip Mpango kwenye mambo ya fedha na uchumi, sera za sekta binafsi , uwekezaji n.k.

Input yake inaweza kuwa sana kwa taifa letu. NI hasara kuwa na bunge walilojaa akina Kibajaji, ni afadhari tuwe na akina Msukuma watachangia kuhusu kuimarisha sekta binafsi maana angalau anaijua sana biashara kuliko wasomi wa biashara na uchumi ngazi za uzamivu.
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
146,399
2,000
Maslahi ya mbunge Tanzania

1.Mshahara 3.8M kwa mwezi
2.Posho mwezi 8M
3.Posho kikao 240k
4.Kujikimu siku 120k
5.Pensheni 240M baada ya 5yrs
6.Bima ya afya daraja la kwanza wewe&familia.
7.Safari za nje
8.Mshahara bila makato ya Bima ya afya wala mifuko ya hifadhi za jamii.
 
Hahitajiki kuwa mbunge ili afanye hayo.. Yeye ni mtaaluma wanaweza kuunda forums za kitaalam ili kuisaidia serikali na bunge
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
102,123
2,000
Nusu ya mshahara wa Mbunge plus posho ya mwezi ndiyo inastahili kuwa kima cha chini cha mshahara, kwa maoni yangu ili kuwawezesha wafanyakazi kumudu gharama za maisha.

Maslahi ya mbunge Tanzania

1.Mshahara 3.8M kwa mwezi
2.Posho mwezi 8M
3.Posho kikao 240k
4.Kujikimu siku 120k
5.Pensheni 240M baada ya 5yrs
6.Bima ya afya daraja la kwanza wewe&familia.
7.Safari za nje
8.Mshahara bila makato ya Bima ya afya wala mifuko ya hifadhi za jamii.
 
MAGO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,052
2,000
Kuna jamaa wa2 classmates wangu waliupata ubunge 2015 yaani mwaka huu zaidi ya maclassmates 4 wametangaza nia. Kinachonisikitisha jamaa hawakuwa na mbele wala nyuma na pass zao class ilikuwa ni C.
Ila C siyo hoja kibaya ni wazi wanakimbilia kupata security ya biashara zao na kupata pesa zaidi na si kutumikia wananchi, na wanauhakika wa kupita maana pesa tayari zipo...Maamuzi ya wananchi hakuna tena
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
6,459
2,000
Kabisa hata baada ya kuona wenzake wametimuliwa kwenye ukuu wa mkoa jana tu, Ole Sendeka naye aamua kukiuka mwito wa rais, kaamua kwenda kugombea ubunge kwao. Kuna tatiza lisilosemeka kati ya wateule wa rais, inaonekana wamekalia mwiba ndio maana wanaona wakatumikie nafasi za kuchaguliwa na wananchi kuliko nafasi za kuteuliwa.
Kila jambo huwa na asili... Yaani chanzo.. Hata mtu asili yake ni manii...
Kosa moja kubwa kabisa tulilolifanya hapo nyuma wakati wa Benjamin Mkapa ni kuipa taaluma kisogo na kuipa SIASA thamani kubwa kuliko uhalisia wake
Jambo hilo halikuwahi kurekebishwa na yeyote yule bali ndio kwanza lilizidi kupaliliwa na kuwekewa mbolea.... Matokeo yake ni haya sasa...

Tuko kwenye kilele cha Kuisigina taaluma, kuihujumu na kuifanya si lolote si chochote mbele ya mwanasiasa aliyefeli masomo yote darasani mpaka lile la lugha yake mwenyewe
Minofu na vinono vya SIASA kipandio chake ni cheo cha ubunge.. Nafasi ya kuchaguliwa na wananchi yenye uhakika wa kula mema ya nchi kwa kipindi cha miaka mitano bila shida kabisa

Pale unapofanikiwa tu kuipata nafasi hii adhimu ya utumishi uliotukuka basi hapo hapo jina lako linabadilika na kuitwa MHESHIMIWA.... Hapa utajihakikishia kibunda cha million kumi tasilimu kila mwezi kwa kazi unayofanya kwa starehe mno... Na baada ya miaka mitano unaondoka na kiinua mgongo cha milioni mia mbili...
Hapo ni ukiwa na kipandio cha ubunge tuu.. Ulibahatika kuukwaa uwaziri ama unaibu wake.. Pepo yako ni hapa hapa duniani
Huko kwenye ubunge kuna fursa na marupurupu ya kila aina tofauti kabisa na kwenye utumishi mwingine wenye suluba na changamoto za kila aina...

Leo hii ubunge sio utumishi wa wananchi tena.. Leo hii ubunge sio kazi ya mkulima na mfanyakazi wa kawaida
Leo hii ubunge ni nafasi ghali, ngumu kupata na ya watu wenye maisha yao... Yaani mambo safi... Kama
Wakurugenzi mbalimbali
Wakuu wa mikoa
Wakuu wa wilaya
Wafanyabiashara wakubwa
Wasanii wakubwa
Watu maarufu nknk
Yaani kupata Ubungo sasa hivi ni lazima uwe fulani kwenye jamii la sivyo utabaki kuwa mpenzi msindikizaji tuu

Wimbi la wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na wakurugenzi kukimbilia ubunge ni kwamba hawana uhakika na kesho yao kwenye nafasi zao.. Lolote muda wowote linaweza kutokea kama aliyekuteua akichafukwa... Ila wanajua kwa hakika kwenye ubunge ni mkataba.. Tena wa miaka mitano

Inashangaza mno kuwa hata wasanii mbalimbali wanaacha kukuza vipaji na vipawa vyao wanakimbilia kuwa wabunge.. Wanashindwa kabisa kujua kuwa ndani ya miaka mitano wakitumikia vema vipaji vyao wanaweza kumake kuliko hata hao wabunge
Nao wamekumbwa na ubinafsi ule wa wengine wasioridhika na walichonacho... Hivi mtu kama Kimei anataka ubunge wa nini? Kwanini asiwaachie damu changa ioneshe uwezo wao? Mzee Wasira bado anataka ubunge... Dah..
Hakika tuna ombwe kubwa la uongozi.. Sasa hivi hata wanataaluma wanaachana na taaluma zao na kukimbilia ubunge
Je tutafika?
Umenena kweli tupu yani hali hii sijui itatufikisha wapi.
Kuna jamaa wa2 classmates wangu waliupata ubunge 2015 yaani mwaka huu zaidi ya maclassmates 4 wametangaza nia. Kinachonisikitisha jamaa hawakuwa na mbele wala nyuma na pass zao class ilikuwa ni C.
Ila C siyo hoja kibaya ni wazi wanakimbilia kupata security ya biashara zao na kupata pesa zaidi na si kutumikia wananchi, na wanauhakika wa kupita maana pesa tayari zipo...Maamuzi ya wananchi hakuna tena
 
steam of ice

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
208
250
Km wasomi wanatusiwa na wasokuw na hekima nn wasikimbilie kisiman nao wateke madaraka ilhali wanaowanyasinyasi ht kujenga hoja kwao ni lazim wawatumie wanaowatusi
 
Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,880
2,000
Hahitajiki kuwa mbunge ili afanye hayo.. Yeye ni mtaaluma wanaweza kuunda forums za kitaalam ili kuisaidia serikali na bunge
Kuna ushauri mwingine lazima ukatoe kwenye vikao vya siri chini ya viapo ukiwa na wafanya maamuzi au ukiwa mfanya maamuzi.
Huko kwenye ubunge ni moja ya njia ya kufkia huko.

Pia ubunge hukupa fursa ya moja kwa moja kushiriki maamuzi mengi hata ya kutunga sheria au kudai maendeleo flani.
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
146,399
2,000
Kabisa hata baada ya kuona wenzake wametimuliwa kwenye ukuu wa mkoa jana tu, Ole Sendeka naye aamua kukiuka mwito wa rais, kaamua kwenda kugombea ubunge kwao. Kuna tatiza lisilosemeka kati ya wateule wa rais, inaonekana wamekalia mwiba ndio maana wanaona wakatumikie nafasi za kuchaguliwa na wananchi kuliko nafasi za kuteuliwa.
Hao wabunge wamejipangua maslahi manono Sana.

Kwa maslahi hayo ya ubunge hata Mimi ningekuwa na uwezo ningekimbilia huko.
Kwakuwa bungeni ndio chombo pekee cha kuwasemea wananchi kupitia wabunge wao kama wawakilishi kuna haja sasa ya kuwa na mabunge mawili.. Hili lisionekane geni machoni petu.. Nchi nyingi tu zina mfumo wa mabunge mawili uingereza ikiwa mojawapo

1. Tuendelee kuwa na hili bunge la fadhila, kujipendekeza kujikomba nk.. Bunge la wasema chochote ili mradi tu mtu aonekane kaongea
Bunge la wachumia tumbo
Bunge la kulindana na kupeana michongo
Bunge la kulinda maslahi ya kibiashara, uwekezaji na mambo ya siri

2. Tuwe na bunge jipya litakalojumuisha wanataaluma na Wataalam wa fani mbalimbali
Wana uchumi
Wana sheria
Madaktari
Walimu na wakufunzi
Wana usalama
Wana sayansi mbalimbali
Wana historia
Wataalam wa mambo ya giza
Wafugaji
Wakulima
Wanadiplomasia nknk
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
146,399
2,000
Kuna ushauri mwingine lazima ukatoe kwenye vikao vya siri chini ya viapo ukiwa na wafanya maamuzi au ukiwa mfanya maamuzi.
Huko kwenye ubunge ni moja ya njia ya kufkia huko.

Pia ubunge hukupa fursa ya moja kwa moja kushiriki maamuzi mengi hata ya kutunga sheria au kudai maendeleo flani.
Nadhani bungeni kuna seminar za kila mara.. Na Wataalam wabobezi wa fani husika hualikwa bungeni kuwapiga msasa wabunge.. Anyway ni mtazamo pia
 
Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,880
2,000
Nadhani bungeni kuna seminar za kila mara.. Na Wataalam wabobezi wa fani husika hualikwa bungeni kuwapiga msasa wabunge.. Anyway ni mtazamo pia
Ndiyo ni mtazamo tu.
Kuna ukosoaji huwezi ufanya nje ya bunge utaishia jela au utatozwa mamilioni ya fidia.
Kumbuka kauli hii "huko bungeni wewe wafukuze ili wakija kuropoka huku mtaani ...."
 
Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
10,635
2,000
Dr. Charles Kimei tunamhitaji sana akasaidiane na akina Dk.Philip Mpango kwenye mambo ya fedha na uchumi, sera za sekta binafsi , uwekezaji n.k.

Input yake inaweza kuwa sana kwa taifa letu. NI hasara kuwa na bunge walilojaa akina Kibajaji, ni afadhari tuwe na akina Msukuma watachangia kuhusu kuimarisha sekta binafsi maana angalau anaijua sana biashara kuliko wasomi wa biashara na uchumi ngazi za uzamivu.
Mtu akisha fika miaka 60 jua na upeo wake umefika kikomo na uwezo wake kiakiri unapungua siku hadi siku,kama huyo kimei alikuwa bado potential sana basi CRDB walikuwa na uwezo wa kumuongeza hata miaka 20.ukiachana na kibajaji kuna wabunge wengi tu ndani ya CCM ni wazuri sema ndio hivyo kwenye huu utawala hawawezi sema chochote wameacha ulingo kwa akina kibajaji na ndio maana kila siku ww unawasikia.
 
bante22

Member
Jan 29, 2020
69
125
Kila mtu anataka kuwa Bunge shauri ya marupurupu miaka 5 unalipwa milion 220 wakati mnyakazi mwingine msomi miaka 40 analipwa milion 55 mshahara wa mbuge na marupurupu 12 mwezi wakati mwalimu laki 6 kwa mwezi. umesikia mtu alikuwa Ccm ana Master analipwa laki 5 na mbuge wa darasa la saba na form 4 na 6 wanalipwa na posho milion 12 kwa Mwezi hiyo ndio Tanzania mbunge ana mzidi doctor.
 
Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,880
2,000
Mtu akisha fika miaka 60 jua na upeo wake umefika kikomo na uwezo wake kiakiri unapungua siku hadi siku,kama huyo kimei alikuwa bado potential sana basi CRDB walikuwa na uwezo wa kumuongeza hata miaka 20.ukiachana na kibajaji kuna wabunge wengi tu ndani ya CCM ni wazuri sema ndio hivyo kwenye huu utawala hawawezi sema chochote wameacha ulingo kwa akina kibajaji na ndio maana kila siku ww unawasikia.
Unajuaje kama yeye ndiyo hakupenda kuongeza muda sababu alitaka kuja kugombea ubunge? Au hakuongezewa muda sababu kuna mkubwa alimuambia anamuhitaji 2020 agombee aende akatumikie taifa kwenye mambo flani?
 
Agenda1

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
1,420
2,000
Kila jambo huwa na asili... Yaani chanzo.. Hata mtu asili yake ni manii...
Kosa moja kubwa kabisa tulilolifanya hapo nyuma wakati wa Benjamin Mkapa ni kuipa taaluma kisogo na kuipa SIASA thamani kubwa kuliko uhalisia wake
Jambo hilo halikuwahi kurekebishwa na yeyote yule bali ndio kwanza lilizidi kupaliliwa na kuwekewa mbolea.... Matokeo yake ni haya sasa...

Tuko kwenye kilele cha Kuisigina taaluma, kuihujumu na kuifanya si lolote si chochote mbele ya mwanasiasa aliyefeli masomo yote darasani mpaka lile la lugha yake mwenyewe
Minofu na vinono vya SIASA kipandio chake ni cheo cha ubunge.. Nafasi ya kuchaguliwa na wananchi yenye uhakika wa kula mema ya nchi kwa kipindi cha miaka mitano bila shida kabisa

Pale unapofanikiwa tu kuipata nafasi hii adhimu ya utumishi uliotukuka basi hapo hapo jina lako linabadilika na kuitwa MHESHIMIWA.... Hapa utajihakikishia kibunda cha million kumi tasilimu kila mwezi kwa kazi unayofanya kwa starehe mno... Na baada ya miaka mitano unaondoka na kiinua mgongo cha milioni mia mbili...
Hapo ni ukiwa na kipandio cha ubunge tuu.. Ulibahatika kuukwaa uwaziri ama unaibu wake.. Pepo yako ni hapa hapa duniani
Huko kwenye ubunge kuna fursa na marupurupu ya kila aina tofauti kabisa na kwenye utumishi mwingine wenye suluba na changamoto za kila aina...

Leo hii ubunge sio utumishi wa wananchi tena.. Leo hii ubunge sio kazi ya mkulima na mfanyakazi wa kawaida
Leo hii ubunge ni nafasi ghali, ngumu kupata na ya watu wenye maisha yao... Yaani mambo safi... Kama
Wakurugenzi mbalimbali
Wakuu wa mikoa
Wakuu wa wilaya
Wafanyabiashara wakubwa
Wasanii wakubwa
Watu maarufu nknk
Yaani kupata Ubungo sasa hivi ni lazima uwe fulani kwenye jamii la sivyo utabaki kuwa mpenzi msindikizaji tuu

Wimbi la wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na wakurugenzi kukimbilia ubunge ni kwamba hawana uhakika na kesho yao kwenye nafasi zao.. Lolote muda wowote linaweza kutokea kama aliyekuteua akichafukwa... Ila wanajua kwa hakika kwenye ubunge ni mkataba.. Tena wa miaka mitano

Inashangaza mno kuwa hata wasanii mbalimbali wanaacha kukuza vipaji na vipawa vyao wanakimbilia kuwa wabunge.. Wanashindwa kabisa kujua kuwa ndani ya miaka mitano wakitumikia vema vipaji vyao wanaweza kumake kuliko hata hao wabunge
Nao wamekumbwa na ubinafsi ule wa wengine wasioridhika na walichonacho... Hivi mtu kama Kimei anataka ubunge wa nini? Kwanini asiwaachie damu changa ioneshe uwezo wao? Mzee Wasira bado anataka ubunge... Dah..
Hakika tuna ombwe kubwa la uongozi.. Sasa hivi hata wanataaluma wanaachana na taaluma zao na kukimbilia ubunge
Je tutafika?
Mkuu ukishangaa ya kimei utayaona ya mstaafu first lady mama yetu salma. Nae anafuata hayo maslahi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom