Ombwe la Uongozi Tanzania: Nchi Imeyumba na iko Hatarini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombwe la Uongozi Tanzania: Nchi Imeyumba na iko Hatarini!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyami2010, Dec 13, 2011.

 1. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wapendwa wanajamii

  1. Hivi, ni kitu gani kinamsibu Rais wetu J.K, kiasi kwamba haoni haya yanayoendelea nchini kwetu?

  Mifano dhahili ni mingi sana, naomba nitaje michache:

  a) Swala la posho za wabunge: Hivi kulikuwa na haja gani Dr. Kashilila kukanusha nyongeza ya posho hizo wakati akijua ukweli wake? Kana kwamba Dr. Kashilila hawasiliani na Mhe. Spika, siku mbili baadaye Mhe. Spika Anna Makinda, akaja na ya kwake..:lol:

  Ndg. Nape naye jana, kana kwamba hawasiliani na M/Kiti wake na Mhe. Spika, naye amekuja na ya kwake.....:lol:

  b) Swala la Jairo: Hivi kulikuwa na uharaka gani Ndg Luhajo kumsafisha Ndg Jairo huku vikao vya Bunge vikiendelea, wakati Bunge hilo lilikuwa limebakiza siku mbili kumaliza vikao vyake? Kana kwamba, Mhe. Rais hawasiliani na Katibu Mkuu wake, siku moja baadae, Mhe. Rais akaja na ya kwake.......:lol:

  c) Kwa muundo wa Serikali tulioizoea tokea Uhuru, ilikuwa na dhahiri Rais kuteua wakuu wa Wilaya na Mikoa mara tu baada ya Uchaguzi Mkuu. Hatuwezi kusema wakuu hawana kazi yoyote, la hasha.....Mpaka sasa ni zaidi ya mwaka, Mhe. Rais hajateua wakuu wa Wilaya na baadhi ya Mikoa. Ebu chukulia mfano wa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa (kama sikosei), Ndg Halima Dendegu anaekaimu Wilaya nne. Hivi Mkuu huyu wa Wilaya anafanyaje kazi? Ni wilaya ngapi nchini ziko na Matatizo kama haya?

  d) Ziko nafasi nyingi hususani kwenye Halmashauri na baadhi ya Taasisi ambazo hazina watendaji wakuu. Waliopo wanakaimu tu, na hivyo kushindwa kutoa baadhi ya maamuzi mazito ya kimaendeleo. Hivi, Rais halijui hilo? Hivi, Mhe. Rais hana washauri?

  e) Wafanyakazi wa Umma, hususani kwenye Halmashauri zetu wamepokea pungufu kwenye mishahara yao ya mwezi Novemba...kulikoni? Jamani, hivi Mhe. Rais hayajui haya?

  e) Mbona haya tunayoyaona na kuyasikia huko Serikalini, hayakutokea vipindi vya Mhe. Mkapa, Mwinyi na Baba wa Taifa? Kuna kitu gani kinamsibu Mhe. Kikwete?

  Hivi, madhara ya haya yote pamoja na Ombwe hili la Uongozi katika Taifa letu, anaeumia ni nani?

  Hakika, 2015 Watanzania tuamke tufanye maamuzi mazito kwa mustakabali wa Taifa letu!
   
 2. d

  dada jane JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umeongea mambo mazito sana. Mwenye macho na masikio na aone hayo.
   
 3. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  napita ntarejea baadae
   
 4. sam2000

  sam2000 JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Tuliyataka sisi wenyewe wazee walitwambia jamaa hafai tukajifanya tunajua, ndio matunda yake hayo na bado four more years!
   
 5. P

  Paul J Senior Member

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamii legelege huongozwa na uongozi legelege. Nani aliwaweka madarakani? Kura mlipiga wenyewe, na uwezo wa kuwatoa mnao nyinyi! Tusilalamike it is a byproduct of our decision making through the box of vote!
   
 6. Yakuza

  Yakuza Senior Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Nyami

  Unayoyasema ni kweli. Akina Salva Rweyemamu na Mhe. Rais wanapitia hapa JF, nina uhakika ujumbe utafika!
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  suala posho hupaswi KUMLAUM kikwete.bado liko liko kwa wate
  ndaj ndo mana makinda ametofauttiana.haya uloyasema hayamhusu jk peke ake but jamii kwa ujumla.acha uchochezi.jk yuko smart na wakuu wilaya tamisemi imeachiwa kuratibu mchakato wa kiutawala ikiwemo mipaka na uongozi wa ngaz za chini hususan kata,vijiji na vitongoj.acha uchochez
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  jairo amesimamishwa na rais unataka nn tena
   
 9. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #9
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  unajua enzi za kina nyerere, mwinyi na mkapa maisha ni kweli yalikuwa magumu kidogo lakini kulikiwa na unafuu sana kwa wafanyakazi wa serikalini maana walau walikuwa wanaheshimiwa katika mambo haya ya malipo yao.. cheki saiz sasa...duh...noma hata kusema..!!:tape:
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  acha uongo wkt wa mwinyi hali ilikuwa mbaya sana labda ulikuwa hujazaliwa.
   
 11. Yakuza

  Yakuza Senior Member

  #11
  Dec 13, 2011
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Katikati

  Hivi kweli, Nyami kasema uongo katika lipi? Pengine wenzetu mnaishi Tanzania nyingine!
   
 12. Shagiguku

  Shagiguku JF-Expert Member

  #12
  Dec 13, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 400
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  unajua rais anaona na kusikia mambo mengi sana tofauti na unavyofikiria, sasa kuanza kuyatolea maamuzi kila jambo analolisikia na kuliona atajikuta hafanyi kazi tulizomtuma kuzifanya pale magogoni, hivo ni bora anyamaze na zingine wazifanye wasaidizi wake,

  kwa mfano: hapo ulipotuma hii tread tayari mheshimiwa rais amekwisha isoma na amekwishajua mawazo yako pamoja na shutuma zako kwake, sasa akisema achukue hatua kwa hii thread yako uliyotuma unadhani utabaki wewe...?? si bora akunyamazie na wewe...!!!
   
 13. CHIETH

  CHIETH Senior Member

  #13
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  A person who cannot genuinely empathize with others can never excel as a leader. So much of what ails society today is the result of too many people in leadership positions who do not or cannot identify with the plight of their fellow men and women. Jk cannot empathize with his fellow Tanzanians who are suffering following inflation in the country and as such his leadership is a burden to his own people from which he swear he will defend.
   
 14. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #14
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa Dr Dr Dr Dr Dr Kikwete ni kama sikio la kufa vile. Hata utoe ushauri mara elfu kumi au ulete mawazo toka mbinguni kamwe hatakusikiliza na hatafuata ushauri wako. Heri kuuchuna tu
   
 15. HT

  HT JF-Expert Member

  #15
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  akianza kufukuza washauri wabovu wanaomzunguka, nitajua sasa ameanza kutumia cheo chake!
   
 16. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutegemea 2015 kufanya mabadiliko!! mimi bado sina imani na 2015 kwa sababu ni wapiga kura wachache sana wanaona haya matatizo. Na kama wakipiga kura zao sina imani na tume ya uchaguzi.
   
 17. rifwima

  rifwima JF-Expert Member

  #17
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Huyo ndo Dr JK KIWETE
   
 18. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #18
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Maamuzi yepi mazito embu kuwa wazi, ili watu waelewe la kufanya pindi ifikapo hiyo mida 2015!!!!!

   
 19. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #19
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Wenyewe wamefika majibu hayo, ukweli kwao ni uchochezi si umeona???????

   
 20. U

  UNIQUE Senior Member

  #20
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tz ipo kwenye experiment. Kusanyeni data/takwimu. Hiki nikichwa cha mwenda wazimu kila mtu anaweza kujifunza kunyoa. Hata kama kuna ombwe utafanya nini? Ni zamu yake kutupiga bei. Watz ni waoga sana kwa hiyo acha atupe kitu mpka machozi ya damu
   
Loading...