OMBI: Watanzania Tuwachague wasomi watuongoze na kutuwakilisha

Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
3,281
2,423
Wanajamvi, kilio changu kwa muda mrefu ni kuona nchi ikiongozwa na watu ambao wamepata weledi na taaluma mbali mbali.

Kwangu naona kuwa ni jambo la aibu sana na fedheha tena kwenye karne hii nchi yetu kuongozwa na watu ambao aslimia kubwa hawana taaluma au weledi.

Wapo wanaodhani na kuamini kua kuongoza na kutenda ni vitu tofauti mpaka kufikia kusema kuongoza hakuitaji elimu au taaluma.

Tuzingatie ila kwamba wana siasa ndio viongozi wetu kwa kiasi kikubwa lakini hao hao taaluma zao zipo chini na wengine wanakua kusoma na kuandika tu.

Katika karne hii jamii yoyote aiwezi kupiga hatua kwakua viongozi na wawakilishi wenye kujua kusoma na kuandika tu.

Mfano kwa wabunge, madiwani,wenyeviti wa vijiji,vitongoji na mitaa. Watu awa ndiyo viongozi wa Taifa ila lakini sasa wengi wao hawana taaluma yoyote.

Ni muda muafaka Taifa ili tuwe na viongozi wenye taaluma na utaalamu wote kuanzia ngazi ya Rais,Mbunge, Diwani,Mwenyekiti wa Kijiji,Mtaa na kitongoji.

Falsafa ya kusema kua moja ya maadui wetu ni Ujinga basi iendane na kua na viongozi wenye taaluma.
 
Hususani kwenye bunge, tuache kuchagua mbumbumbu, CCM inapenda sana kuwasimamisha kwakua ni rahisi kuwadhibiti.
 
Bishweko, Mimi ni msomi napenda msomi ajitosheleze katika,elimu upeo,ujuzi na
Competency ndio jambo la msingi.vinginevyo hatufai.
 
Hata uwe msomi lakini ukiitumia taaluma yako kama siitaki hata unieleweshe vipi sikubali sawa
Ukitaka wasomi nenda kwa mabeberu


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Wasomi hawahawa wanaoongoza kwa kufanya maamuzi ya kitoto nchi hii au? Mi ningependa waje wagombee wasomi ambao ni Diasporas labda watakuja na mapya.
 
Bishweko,

Tatizo wananchi hawajawahi kuona faida ya taaluma kwenye siasa. Hivyo wanachagua watu wanaowajua na kuwasikiliza. Kuna professors kibao ambao hawafanyi kazi ya maana kwenye siasa na hawahitjiki. Kuna tofauti ya uongozi na usomi mfano PHD ya Magu ambayo ni ya majani ya korosho imesaidia nini? Hata biashara ya korosho yenyewe alishidwa tukapata hasara sasa watu wakiona hivyo wanajua hapa ni bure tu. Kuna idara chache tu zinahitaji wasomi lakini nyingi zinahitaji zaidi uzoefu hasa wa kibiashara
 
Back
Top Bottom