Ombi:;wabunge wakataeni akina mapuri kuwahutubia kuhusu muungano

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
825
NImekosa usingizi kabisa usiku huu wa manane baada ya kupata sms news alert kuwa eti wale wageni aliowataja Mh.sita leo bungeni kuwa watakuja kuhutubia bunge kuelimisha kuhusu Muungano ni akina Ramadhani Mapuri, mawaziri wa zamani waliotumika hasa kipindi cha Mkapa na Mwiny,i kwa kuwa eti ni watu waliobaki wanaojua muungano kinabaubaga! mheshimiwa sana Sita katamka haya bungeni bila haya kuwa katika watanzania milioni 45 na ushee kuna watu watatu waliobaki wanaoufahamu muungano kilivyo, ndivyo Sita anavyoamini!


Nataka kumweleza wazi Sita na kundi lake la wana nadharia kuwa, wakati wa kutunga nadharia hasi ili kupotosha watu ulishakwisha, na kuwa huu si wakati tena wa bla bla. Hakuna mtanzania aliyesoma hata mpaka darasa la saba asiye jua histotia na asili ya Muungano, sita analifahamu hilo, ukienda leo shule ya msingi lupatingatinga kule chunya, au malinyi kule morogoro au misenyi kule bukoba ukiluza wanafunzi hata darsa la kwanza watakusimulia kuhusu muungano, sembuse ni waheshimiwa sana wabunge??? Muungano unafundishwa shule zote, vyuo vyote, kwenye makambi ya JKT kwenye misikiti na makanisa unatamkwa, Leo tunaambiwa waamebaki watu watatu wanaojua muungano eti Ramadhani Mapuri, naibu katibu mkuu wa zamani wa ccm!

Nia ya sita na wana-nadharia wenzake inajulikana katika hili, ni kutafuta namna ya kupotosha wabunge na kuipotosha rasimu ya katiba ambayo ni dira ya kile wanachokitaka wananchi kuhusu mfumo wa muungano, hili liko wazi, ndiyo maana anataka kuwaleta bungeni wana propaganda waliobobea katika kupotosha, ilikuwatisha wabunge kwa hoja zisizo na mashiko na labda kupigania hoja yao ya serikali mbili inayoelekea kuzama.

kama alivyowahi kueleza mheshimiwa Piusi Msekwa, kinachodumisha muungano si wingi wa serikali bali utashi wa wale walioungana, kamwe machozi ya akina sendeka, propaganda za akina mapuri hazitasaidia katika hili.
lakini pia huyu mapuri alikuwa wapi mwaka 2010, wazanzibar walipoamua kuvunja muungano na kujitangaza kuwa ni taifa huru bila kujali athari zake katika muungano? mbona hakuenda kule baraza la wawakilishi kukemea hili kama kweli anautaka muungano?

tunaambiwa kuwa mwanasheria mkuu wa zamani wa kenya Bwana Amos Wako naye amealikwa dodoma, tunajua ni jinsi gani Wako alivyowayumbisha wakenya na kusababisha kuvugika kwa awamu ya kwanza ya katiba ya kenya, huhitaji digrii ya uzamivu kuwa huyu amealikwa na AKINA CHENGE KWA KUWA ALIFANYA KAZI KATIKA KILE KIPINDI CHA KINA CHENGE ! HUHITAJI PHD KUWA hakuna lolote la maana kutoka kwa mtu aliyechoka kama wako, wakenya watatushangaa sana kama bado tunategemea chochote toka kwa watu aina ya wako.

kuna watu wa kuheshimika hapa Afrika Mashariki akina profesa Ngugi wa Thiongo, profesa Wamba dia Wamba, na maprofesa nguli wataalamu wa katiba, kama yule mfaransa aliyetajwa kama rejea bungeni, lakini eti bado tunakimbilia kwa akina Mapuri!

Tunawaomba wabunge kwa umoja wao, kukataa kupotoshwa na wageni hawa wa ajabu crippled minds walioalikwa kwa busara ya mwenyekiti, wakataeni na kama mlivyofanya leo msiwasikilize kamwe. kama inawezekana tengenezeni orodha ya wageni na mkubaliane siyo kila kitu ni busara za mwenyekiti

 
Kwenye Aya ya kwanza mpaka ya Tano kama unauchungu na nchi hii lazima usingizi utakukosa tu na hata unaweza kwenda mbali kwa wale tulio katikandoa hata hamu ikakosa ukabaki kumwambia Mrs najisikia vibaya kumbe unafikilia haya mambo yanavyotaka kupindishwa aisee Mapuri!!!!Mapauri huyu leo akausemee Muungano!!!!!
 
Mkuu upo sahihi, huyu SS naona ana ajenda ya siri na maccm wenzake, nimemdharau sana jana alivyokuwa ana handle ile issue ya kuvunja kanuni ili Jaji Warioba awasilishe rasimu ya katiba. Nimemuona ni mzee wa ajabu kwelikweli kinyume na matarajio ya wengi.
 
hawawezi kumwalika Aboud Jumbe, au hata Jaji Mark Bomani badala yake wanakimbilia kwa akina Amos Wako kule kenya
 
mapuri huyu au babake....?
2Q==
 
Sidhani kama kuna haja ya kuendelea kupoteza pesa Dodoma ,warudi tu waendelee na shughuli zao.Nuda utakapofika tutapata KATIBA ya watanzania na si KATIBA ya CCM.
 
(Mapuri na)...tunaambiwa kuwa mwanasheria mkuu wa zamani wa kenya Bwana Amos Wako naye amealikwa dodoma, tunajua ni jinsi gani Wako alivyowayumbisha wakenya na kusababisha kuvugika kwa awamu ya kwanza ya katiba ya kenya, huhitaji digrii ya uzamivu kuwa huyu amealikwa na AKINA CHENGE KWA KUWA ALIFANYA KAZI KATIKA KILE KIPINDI CHA KINA CHENGE ! HUHITAJI PHD KUWA hakuna lolote la maana kutoka kwa mtu aliyechoka kama wako, wakenya watatushangaa sana kama bado tunategemea chochote toka kwa watu aina ya wako.

kuna watu wa kuheshimika hapa Afrika Mashariki akina profesa Ngugi wa Thiongo, profesa Wamba dia Wamba, na maprofesa nguli wataalamu wa katiba, kama yule mfaransa aliyetajwa kama rejea bungeni, lakini eti bado tunakimbilia kwa akina Mapuri!

Tunawaomba wabunge kwa umoja wao, kukataa kupotoshwa na wageni hawa wa ajabu crippled minds walioalikwa kwa busara ya mwenyekiti, wakataeni na kama mlivyofanya leo msiwasikilize kamwe. kama inawezekana tengenezeni orodha ya wageni na mkubaliane siyo kila kitu ni busara za mwenyekiti

Uko sahihi kabisa. Prof. WAMBA dia WAMBA ni marehemu, miaka kama kumi imepita tangu atutoke, naona umepitiwa kidogo.

Kama kuna Mkenya wa kutusaidia katika hili suaLA la Katiba, Wako atakua ni mtu wa mwisho kabisa.

Mimi ningefurahi kama angealikwa Prof. PATRICK ODHIAMBO LUMUMBA, wenyewe WAKENYA wanamuita PLO ... Huyu jamaa anatisha katika masuala ya KATIBA... pendekezo lake la KATIBA MPYA ya Kenya ndilo lililotupwa na akina WAKO, nchi ikawaka moto.

PLO aliwahi kuwa mwenyekiti wa tume kama hii ya WARIOBA, na alifanyiwa NA SERIKALI YA KENYA kama CCM inavyomfanyia WARIOBA
 
Sidhani km watakwenda tenda....kwa hotuba hii ya Warioba..wakajipande upya
 
Sita amewekwa pale kwa matakwa ya akina wasira,kinana,mangula,na kikwwte na walimpa mashariti
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom