Ombi, ushauri au ufafanuzi ofisi za NACTE ofisi za Dar es Salaam

CTP

Member
May 6, 2024
6
3
Habari zenu ndg zangu,

Ndugu zangu naomba ufafanuzi au ufahamu na ufafanuzi juu ya hali anayopitia mdogo wangu, mdogo wangu kafuata TRANSCRIPT yake ofisi za NACTE DAR tarehe 29/05/2024 akajibiwa arudi baada ya may-mosi yaani tarehe 02/05/2024 na akarudi tarehe hzo lakini alijibiwa MTANDAO UPO CHINI RUDI KESHO, sasa kila siku anaenda ofisini kwao na majivu yamekuwa ni MTANDAO UPO CHINI hadi leo hii.

Dhumuni la uzi huu ni kutaka kujua kama ni kweli siku 7, week nzima mtandao upo chini au kuna mazingira mengine na si mtandao.

Zaidi mdogo wangu huyu masafiri kutoka mkoani na kafikia LODGE sasa ni week mbili yupo Dar hadi amefikia hali ya kukata tamaa.

Mdogo wangu huyu kapata sehem kama ajira baada ya kufaulu INTERVIEW yake lakini kikwazo kinataka kuwa ni hii TRANSCRIPT kumbuka kajiajiri mala baada ya chuo miaka toka miaka 4 nyuma. Katumia hadi mtaji wake wote kwa matumizi ya LODGE na chakula hadi kufikia hatua naanza kumtumia vipesa kughalamia japo hakuna matumaini maana kila akienda jibu ni MTANDAO UPO CHINI.

Swali najalibu kuwaza hivi kweli ofisi ya NACTE DAR week nzima hakuna mtandao au ni mazingira fulani yanaandaliwa hapa yasiyo rafiki na si mtandao.

Naomba wadau, kiongozi au vyombo vinavyoweza kutatua hali hii kumsaidia huyu mdogo wangu na wenzie waliopo ofisi hizo kipindi hiki juu ya jibu hili la MTANDAO UPO CHINI na kuzingatia upatikanaji wa hitaji lao.

Vijana tunapambana sana hivyo ifikiapo kijana kahitajika mahala kwa taaluma yake tusaidiane kuwakamilishia mahitaji yao maana itakatisha tamaa vijana na kujikuta wanaangukia njia zisizofaa kwa uzembe wa wachache.

MUNGU IBARIKI JF NA WATU WAKE.
 
Dogo kasota mtaani miaka kadhaa,leo mtu kafungua ofisi kawafanyia INTERVIEW dogo kapita na kinachohitajika ni TRANSCRIPT naóna anarudi mtaani kiutani utani na mtaji kaishiwa na hali yenyewe hii sijui maisha yake yatakuwaje tu.
Kuna muda huwa naona vile WAZIRI D. GWAJIMA anashughulikia mambo hapa JF nadhani hili lingekuwa upande wake angeshalitatua.

Sijui hata dogo akimbilie wapi apate msaada, sijui ni waziri gani anahusika hapa dah!Waziri D.Gwajima MUNGU akulinde zaidi kazi yako inagusa na kuwapa matumaini na mwanga wengi wakiao pale wanapohitaji msaada uhusuo idara yako.
Inasikitisha sana
 
Ofisi za serikali nyingi zina shida sana.. ukiwa na tatizo la haraka kusaidika n mpaka uwe na mazingira fulani.

Watakuja weny uelewa zaid utasaidika ndugu
 
za serikali nyingi zina shida sana.. ukiwa na tatizo la haraka kusaidika
Hatari sana dogo anapitia wakati mgumu sana hadi nawaza jumamosi siku aliyosema anarudi hata asipopata kama akifika atakuwa sawa, ukizingatia alivyopata mtaji kwa shida na mtaji katumia wote na alichokifuata asipate.
 
Dogo kasota mtaani miaka kadhaa,leo mtu kafungua ofisi kawafanyia INTERVIEW dogo kapita na kinachohitajika ni TRANSCRIPT naóna anarudi mtaani kiutani utani na mtaji kaishiwa na hali yenyewe hii sijui maisha yake yatakuwaje tu.
Kuna muda huwa naona vile WAZIRI D. GWAJIMA anashughulikia mambo hapa JF nadhani hili lingekuwa upande wake angeshalitatua.

Sijui hata dogo akimbilie wapi apate msaada, sijui ni waziri gani anahusika hapa dah!Waziri D.Gwajima MUNGU akulinde zaidi kazi yako inagusa na kuwapa matumaini na mwanga wengi wakiao pale wanapohitaji msaada uhusuo idara yako.
Mungu amtetee tu mdogo wako. Nchi hii wazembe wengi wamejaaa kwenye ofisi za umma. Aibu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu ndg zangu,

Ndugu zangu naomba ufafanuzi au ufahamu na ufafanuzi juu ya hali anayopitia mdogo wangu, mdogo wangu kafuata TRANSCRIPT yake ofisi za NACTE DAR tarehe 29/05/2024 akajibiwa arudi baada ya may-mosi yaani tarehe 02/05/2024 na akarudi tarehe hzo lakini alijibiwa MTANDAO UPO CHINI RUDI KESHO, sasa kila siku anaenda ofisini kwao na majivu yamekuwa ni MTANDAO UPO CHINI hadi leo hii.

Dhumuni la uzi huu ni kutaka kujua kama ni kweli siku 7, week nzima mtandao upo chini au kuna mazingira mengine na si mtandao.

Zaidi mdogo wangu huyu masafiri kutoka mkoani na kafikia LODGE sasa ni week mbili yupo Dar hadi amefikia hali ya kukata tamaa.

Mdogo wangu huyu kapata sehem kama ajira baada ya kufaulu INTERVIEW yake lakini kikwazo kinataka kuwa ni hii TRANSCRIPT kumbuka kajiajiri mala baada ya chuo miaka toka miaka 4 nyuma. Katumia hadi mtaji wake wote kwa matumizi ya LODGE na chakula hadi kufikia hatua naanza kumtumia vipesa kughalamia japo hakuna matumaini maana kila akienda jibu ni MTANDAO UPO CHINI.

Swali najalibu kuwaza hivi kweli ofisi ya NACTE DAR week nzima hakuna mtandao au ni mazingira fulani yanaandaliwa hapa yasiyo rafiki na si mtandao.

Naomba wadau, kiongozi au vyombo vinavyoweza kutatua hali hii kumsaidia huyu mdogo wangu na wenzie waliopo ofisi hizo kipindi hiki juu ya jibu hili la MTANDAO UPO CHINI na kuzingatia upatikanaji wa hitaji lao.

Vijana tunapambana sana hivyo ifikiapo kijana kahitajika mahala kwa taaluma yake tusaidiane kuwakamilishia mahitaji yao maana itakatisha tamaa vijana na kujikuta wanaangukia njia zisizofaa kwa uzembe wa wachache.

MUNGU IBARIKI JF NA WATU WAKE.
Ye hapo ameshindwa Kuelewa Nini??
Mtandao Ukiwa chini Unapandishwa kwa namna yake..
Yaani Ile namna kama unavuta Uradi kwa Tasbhi..
Aache mkono mfupi alitakiwa Ajue kuwa Tangu tarehe 29 ile alipaswa Kujiongeza atakaa miezi mitatu hapo ohooo 😅😅😅
 
RUSHWA hawezi toa, na huwa ikifikiaga hapa huwa nawaza sana familia zetu hizi mtoto afikie jaribu hili, yaani ni yeye na MACHOZI YAKE na kukufuru tu juu ya hali anapitia
Kama hawezi toa Asubiri Mwezi wa Sita atapewa..
Siku hizi wTu wanakula kwa urefu wa kamba mkuu
 
Back
Top Bottom