Ombi: Usambazaji wa Picha za Rais Samia Mitandaoni akiwa Marekani ziendane na 'Direct Economic Impact' Mifukoni mwa Watanzania

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Naanza kuona taratibu Nguvu Kubwa inatumika kumuonyesha Mheshimiwa Rais Samia akikubalika zaidi na Wazungu (hasa hasa hawa Wamarekani) na kwamba aliyekuwa Boss wake hakuliweza au hakulifanikisha hilo ila kwa bahati mbaya mno Nguvu hiyo hiyo haitumiki Kuwafafanulia Watanzania ni jinsi gani Ziara hiyo itapunguza Maisha magumu ya Watanzania na je, zile Ziara zingine za 'Kujikomba' kwa Wazungu mpaka wakatupa Fedha hizo Fedha zimebadili hata kidogo Maisha ya Mtanzania anayetaabika sasa na Ugumu wa Maisha ambapo anajibiwa kirahisi na kipuuzi tu kuwa sababu ni Vita vya Urusi na Ukraine?

Nawasubiri kwa hamu Team Kusifia, Kujipendekeza na Mazuzu waje kwa Wingi katika Kutusaidia kutupa Mawazo yao ili tuwaamini kuwa kweli Vichwani mwao kumejaa Madini tupu kuliko wengine ambao Siku zote tuko 'Neutral' katika Mitazamo ya Kimasuala na tunaona mbali kama Ndege Tai ( An Eagle )
 
Hili swali liulizwe baada ya mwaka mmoja ndio itakua na mantiki? Waulizwe wadau wa utalii na serikali Je? Baada ya Royal Tour namba ya bookings ziliongezeka au kama taifa tulipigwa?
 
Naanza kuona taratibu Nguvu Kubwa inatumika kumuonyesha Mheshimiwa Rais Samia akikubalika zaidi na Wazungu ( hasa hasa hawa Wamarekani ) na kwamba aliyekuwa Boss wake hakuliweza au hakulifanikisha hilo ila kwa bahati mbaya mno Nguvu hiyo hiyo haitumiki Kuwafafanulia Watanzania ni jinsi gani Ziara hiyo itapunguza Maisha magumu ya Watanzania na je, zile Ziara zingine za 'Kujikomba' kwa Wazungu mpaka wakatupa Fedha hizo Fedha zimebadili hata kidogo Maisha ya Mtanzania anayetaabika sasa na Ugumu wa Maisha ambapo anajibiwa kirahisi na kipuuzi tu kuwa sababu ni Vita vya Urusi na Ukraine?

Nawasubiri kwa hamu Team Kusifia, Kujipendekeza na Mazuzu waje kwa Wingi katika Kutusaidia kutupa Mawazo yao ili tuwaamini kuwa kweli Vichwani mwao kumejaa Madini tupu kuliko wengine ambao Siku zote tuko 'Neutral' katika Mitazamo ya Kimasuala na tunaona mbali kama Ndege Tai ( An Eagle )
Ni mkulima gani awezae kulima and at the same time anavuna?, Njia hutengenezwa and then matarajio mema hufuata (the same kama unavyo tayarisha shamba kupanda mbegu kusubiri and them kuvuna.
 
Back
Top Bottom