OMBI: Tubadilishe Mwelekeo wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

OMBI: Tubadilishe Mwelekeo wa Tanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kichuguu, Jul 6, 2010.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Jul 6, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  CCM ni chama kilichoiongoza Tanzania virtually miaka yote tangu tumepata Uhuru, ama kwa joho la TANU/ASP au kama CCM. Kwa bahati mbaya, nchi hii imekuwa inarudi nyuma miaka yote amabyo tumekuwa tukiongozwa na CCM hiyo.

  Kuna haja ya kubadilisha mwelekeo wa Tanzania ili kuwanusuru watanzania wasje jikuta wakawa ni watumwa pekee wa dunia ijayo.

  Njia mojawapo nyepesi sana ya kuinusuru nchi hii ni kwa sisi kuwahamasisha ndugu zetu wa vijijini kuendelea kupokea zawadi zote zitakazotolewa na wagombea wa CCM lakini wasimpigie mgombea yeyote wa CCM. Wamchague mtu yeyote anayepingana na CCM, na katika uchagzui huu wasipoteze muda kujiuliza kuwa mtu huyo ataleta nini jimboni kwani tunajua kuwa hata wale wa CCM hawataleta kitu. Jambo la muhimu liwe ni kuipumzisha CCM kutoka madarakani tu. Kwa vile upinzani hauna organaizesheni kubwa sana kama ilivyo CCM, ujambazi watakaoufnya kwa nchi hii hautakuwa organized kama ule uliofanywa na CCM katika mika ayote waliyokaa madarakani na hivyo madhara yake yatakuwa ni mdogo au hayatakuwepo kabisa. Tutakuwa na viongozi wa CUF, CHADEMA, TLP, UDP na utitili mwingine ambao kila mmoja atapenda afanye vizuri ili uchaguzi ujao apate kura nyingi, na hapo ndipo tutakapoanza kuona maendeleo halisi. Vinginevyo tutandelea kuota.
   
 2. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hili suala la kukimbilia kuitoa CCM madarakani na kuwapa wapinzani nchi bado siamini kama ni suluhisho la matatizo yetu.

  Tumetawaliwa na emotions/hate/visasi kiasi kwamba uwezo wa wetu wa kufikiri na kuchanganua mambo unakuwa questioned/jeopordized. Ukitazama kwa jicho la tatu na kutafakuri inavyotatikana utaona kwamba upinzani bado haujakomaa kiasi cha kuweza kuongoza serikali!
  I'm certainly sure, kama tukiwapa wapinzani nchi kwasasa ili waunde serikali yao. Basi taifa litatawaliwa na viongozi vihiyo kuliko wakati mwingine wowote!

  Hebu changanua nafasi zote za kisiasa ambazo zipo halafu upime kuona kama tunaweza kuwapa nchi wapinzani, anza na Urais na Umakamu(and his/her team), Mawaziri na Manaibu wao, Washauri wa Rais(It's a big team), PM and his/her team, wakuu wa mikoa na wilaya, watendaji wa post za kuteuliwa na Rais(Jeshi, polisi, etc) na nafasi nyingine nyingi. Kiukweli utaona kuwa CCM bado inastahili kuendelea kuongoza nchi.

  Nashauri tusikimbilie kusema hatuitaki CCM bila ya kuwa na "succession plan" baada ya CCM kuondoka.

  Let's always think critically, and do the cost benefit analysis before we decide.
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Jul 6, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hofundiyo hufanya future yetu iwe gleam; hakuna sheria inayosema kuwa viongozi wa CCM ndio wanaofaa kuongza nchi hii tu ukiacha propaganda. Kuna watu waliokuwa upinzani, lakini walipohamia CCM wakawa na madaraka makubwa sana (Nsanzugwako, Tambwe, Kaborou, Makanga na kadhalika) vile vile kuna watu waliokuwa CCM wakiwa na madaraka makubwa lakini leo wako upinzani ( Sherif Hamad, Mrema, Mpendazoe n.k); hyapo ukaicha wale waliokuwa CCM wakaingia upinzani na baadaye wakachukuliwa na CCM tena kama vile Wassira. Kwa hiyo uongozi siyo chama bali ni mtu mwenyewe; tatizo la Tanzania tume-instutionalize uongozi wa nchi kuwa ni mradi wa CCM tu, hata wapumbavu wanataka waingie CCM ili baadaye wawe viongozi wetu. Tukishaachana na hiyo dhana ya kuinstitutionalize dhamana ya uongozi kuwa mali ya CCM tutaweza kuona upande wa pili wa giza lililotandzabele yetu kwa jina la CCM. Ni Makosa sana kudai kuwa wabunge wote wa upinzani (kwa mfano) hawafai kuingoza nchi hii kwa vile tu hawako CCM.

  Tujifunze machache haya kuhusu hofu za namna kama unayoonyesha:

  "People are afraid of the future, of the unknown. If a man faces up to it and takes the dare of the future he can have some control over his destiny."
  -- John Glenn


  "The fishermen know that the sea is dangerous and the storm terrible, but they have never found these dangers sufficient reason for remaining ashore."
  -- Vincent Van Gogh

  “Sometimes when people are under stress, they hate to think, and it's the time when they most need to think.”
  -- Bill Clinton


  “Pessimism is an excuse for not trying and a guarantee to a personal failure.”

  -- Bill Clinton


  "Trying does not guarantee success, but it is a hell of a lot better than not trying."
  -- Unknown author


  "Trying does not guarantee success, but failure to try is guarantee that you will never succeed"
  -- Bill Clinton????

  "I have often been afraid, but I would not give in to it. I made myself act as though I was not afraid and gradually my fear disappeared."
  -- Theodore Roosevelt

  "Of all the liars in the world, sometimes the worst are your fears."
  -- Rudyard Kipling
   
 4. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kabengwe

  Kimfumo wa utawala tulionao na tuliouzoea unaweza kufikiri kila kitu lazima kiendeshwa kisiasa, ndiyo maana unakuta wengi wetu tuko very skeptical kusikia wapinzani wanaachiwa nchi. Kuna institutions zingine hazihusiani moja kwa moja na siasa, umetaja jeshi, polisi vitu hivi vinatakiwa vijitegemee hata endapo chama tawala kinaondoka madarakani vibaki bila kutikisika.

  Labda tuseme mawaziri wanaweza kuwa influenced moja kwa moja na siasa kwa vile ndio watekelezaji wakuu wa sera za chama, lakini Mahakama, wakuu wa wilaya hata wakuu mikoa,majeshi, walimu, banking system, wakurugenzi, etc wanatakiwa wasijihusishe na vyama moja kwa moja endapo kama kutahitajika changes zinatakiwa kuwa very minimal.

  Nchi zingine haya mambo yanafanyika kuna post za kisiasa na post za kitaaluma, mara nyingi government organs(institutions) hubaki kama zilivyo. Hata hapa kwetu inatakiwa watu waelewe hivyo lakini ukizingatia vyeo hugawiwa kwa kujuana inakuwa vigumu.

  Lakini all in all usifikiri viongozi wote wa CCM hawana mioyo ya uzalendo, wengine wana mioyo ya upinzani lakini kimwili wako CCM kwa maslahi yao, nafikiri watakuwa tayari kushirikiana na kusaidia chama chochote kitakachokuwepo kwa wakati huo, ndiyo maana wakati mwingine tunasikia wapinzani wamepata nyaraka za siri na taarifa muhimu za serikali.
   
 5. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160

  Kibwengwe,

  Mimi sikushangai, kwani wewe ni mmoja wa watu ambao wameshindwa kuelewa kuwa katika kuendesha serikali zipo political figures na watendaji serikalini. Kwa mfano katika kila wizara kuna makatibu wakuu na mawaziri; hawa ndiyo viongozi katika kila wizara. Political figure hapa ni waziri na mtendaji ni katibu mkuu. Maana yake nini!! Leo CCM ikiondoka madarakani waziri atabadilika lakini katibu mkuu anaweza asibadilike; kwani kikatiba hatambuliwi na chama, ni muajiriwa wa serikali. Huu ni mfano wa kutofautisha hawa watendaji. CCM toka wakati ule wa chama kimoja walitufanya tuone hakuna tofauti ya chama cha siasa na serikali.

  KWa hiyo, leo CCM wakiondoka waajiriwa wa serikalini watabaki kama walivyo; na ni discretion ya mkuu atakaye kuwepo kubadili watendaji ikiwa itamlazimu. Serikali ni tofauti kabisa na siasa. Ndo maana hata juzi wengi tulishangaa inakuwaje CJ na jopo lake walipiga siasa kwenye suala la mgombea binafsi ilihali wanajua kabisa kikatiba wanatakiwa kutoa tafsiri kisheria ili kufanya mambo yaende!!

  Acha hofu mkuu, naturally human being needs changes!! This goes up to personal levels, every one needs changes almost everyday. Ingelikuwa inawezekana watu kuoa na kuonja mpya kihalali wengi tungenenepa tu!!! (just kidding!!:loco:)
  We have to try the other side of the coin!!!
   
 6. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimewaelewa!
  But I'm not conviced kama wapinzani wanaweza kuongoza nchi kwa sasa. Nakubali kwamba kunatakiwa kuwe na political figures na watendaji, lakini hiyo bado ni politics. Hamna Rais atakemuweka katibu mkuu asiemuamini, au mkuu wa jeshi/polisi/usalama wa taifa. Hilo haliwezi tokea.

  Kwa sasa wapinzani hawawezi kuongoza nchi. Bado wanahitaji kuimarika kwenye ubunge na udiwani kwanza. Huko ndo watapata viongozi wa kupewa nafasi za uongozi. Hatuwezi kuwapa nchi halafu more than 2/3 ya viongozi wawe kwenye majaribio ya uongozi. Hatuwezi kuwa na nchi ya aina hiyo.
  Kwa hesabu za haraka haraka, ni wapinzani wangapi ambao utendaji wao unaonesha wanaweza kuwa mawaziri wazuri?! Sidhani kama namba itazidi 5. Which means wengine wote tutawaweka kwa kuwajaribu!
  Nchi haiwezi kuendeshwa kwa dizaini hiyo
   
 7. B

  Bilimbi Member

  #7
  Sep 4, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ignorant and coward
   
Loading...