Ombi: Trafiki wa kwenye mataa ya Benki ya Stanbic (salender bridge) tendeni haki

SWEET GIRL

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
520
377
Habari za majukumu wadau!

Nimekuja hapa kutoa ombi kwa Trafick wanaoongoza magari hapa kwenye njia panda na mataa ya bank ya stanbic karibu na daraja la salender tafadhali tunaomba mtende haki.

Tunajua kazi yenu ni ngumu sana lakini tunaomba mtende haki.sisi abiria tunaotoka kinondoni road yaan wakazi tunaotoka mwanyamala,leaders,Kinondoni makaburini n.k na tunatumia hii barabara ya Kinondoni road tunateseka sana na hili ni kwa muda mrefu sasa.

Tunawekwa kwenye foleni kwa muda mrefu huku magari yanayotokea oysterbay na wale wanaotoka Ali Hassan Mwinyi road wakiruhusiwa kupita mpaka sometimes magari yanakwisha kabisa kwenye hizo barabara.

Mfano leo tarehe 10.10.2018 tumewekwa kwenye foleni kwa saa nzima bila kupita ambapo kwenye mida ya saa tatu kasoro ndo tumeanza kuruhusiwa kupita.

Tunaomba sana mtutendee haki kwani na sisi tunawahi makazini kama hao wanaotokea masaki na ally hassan mwinyi.ninaomba maombi haya pia yamfikie kamanda wa kikosi cha barabarani wa wilaya ya kinondoni.asante sana.
 
Poleni mkuu! Najua adha za barabarani kwakweli, wala siwezi kukutania hapa.
 
Pole mkuu. Uwe unapita kilimani road unatokea ubalozi wa ufaransa.

Au unapita hyo Tunisia road unatokea leaders kisha unatembea mbele.

Mwisho kabisa acha usumbufu kwa watu wengine kutumia herufi kubwa, kwa mwendo huu trafiki watakuweka sana hapo ubalozi wa India.
 
Vumulia, linakuja daraja la kupita baharini kwa hisani ya Wakorea
 
sasa nyie samaki si zinakuwa kwenye friji haziharibiki muda wowote mnazikuta, ungekuta kipindi cha afande samweli si ungelia
 
Back
Top Bottom