Ombi: Serikali iwalipe mshahara watumishi waliotia nia Ubunge

7 ELEVEN

Member
May 29, 2017
74
138
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) na M/KITI wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli;

Kwa heshima kabisa, ninakuomba uwakumbuke kuwalipa mishahara watumishi wa Umma ambao walijitoa kwa moyo mmoja kukipigania Chama Chetu – CCM huko majimboni kwa kujitokeza kuwania nafasi ya kugombea Ubunge au Udiwani kupitia chama chetu - CCM.

Wapo watumishi wa Umma – MAKADA WA CCM - takribani elfu saba (7,000) ambao walijitokeza kutia nia katika majimbo mbalimbali hapa nchini. Ni dhahiri hawa ni wenzetu, na walikuwa wanakipigania chama chetu na bado watakipigania chama chetu CCM kuhakikisha tunapata ushindi mnono. Hivyo basi ukiwa kama M/KITI WA CCM TAIFA na Rais wa JMT, naomba ulithamini hili jeshi (hawa makada). Hii ndio hazina ya Chama katika taasisi mbali mbali za Umma kama vile – Vyuo Vikuu, taasisi za utafiti, vyuo vya kati na halmashauri mbali mbali nchini ambao ndio watakuwa msaada mkubwa huko waliko kuhakikisha chama chetu kinashinda kwa kishindo.

Walio wengi ni wasomi kuanzia ngazi ya bachelor degree hadi PhD (Muulize Dr. Ndumbaro – Katibu Mkuu Utumishi) atakuambia kwa sababu taarifa zao tayari anazo. Kwetu sisi kama Chama ni jambo la kujivunia kuona kuwa tuna mtaji mkubwa sana wa makada wa chama chetu katika taasisi mbali mbali hapa nchini na wapo tayari kukipigania Chama.

Pia kumbuka hawa Makada huko majimboni wameombwa kuunganisha nguvu kwa umoja na kuhakikisha anayepitishwa na Chama chetu – CCM kinaibuka mshindi, sasa huyu kada ambaye hajapata mshahara wa mwezi wa saba, na huu mwezi wa nane hapati tena; je atakuwa na nguvu gani ya kukipigania chama? Je, atakuwa na mapenzi na chama chake? Huko aliko kwa jinsi familia yake inavyoishi kwa shida, je atakuwa na upendo tena na chama? Mheshimiwa M/KITI funika kombe mwanaharamu apite, maana tusije tukampa adui faida muda huu.

Mheshimiwa M/KITI – CCM TAIFA nakuomba utambue kuwa hili jeshi ni la leo na kesho. Watumishi wa Umma zaidi ya elfu 7 kujitokeza hadharani nchi nzima kukipigania chama sio kitu kidogo ujue! Wape moyo kwa kuwalipa mshahara wao wa mwezi wa nane ili wawe na nguvu kuzunguka majimboni kukipigania chama na wenzao ambao wameteuliwa leo na Chama chetu kupeperusha bendera ya CCM.

Kwa namna moja au nyingine ni kweli wamekiuka taratibu za kiutumishi, lakini tambua kuwa watumishi wengi hawakupata nafasi ya kuuona huo Waraka. Pia wapo wengine wengi tu waliouona huo Waraka lakini kwa mapenzi ya dhati na chama Chetu- CCM waliamua kwenda kufia chama huko majimboni kupitia chama chetu CCM, hivyo ni heri ikatumika busara na hekima ili hili jeshi letu liweze kuwa na nguvu ya kukipambania chama chetu – CCM leo na kesho pia.

Mheshimiwa M/KITI wangu wa Chama – CCM na Rais wa JMT, nimeamua kukuandikia ujumbe huu kwa sababu ya upendo nilio nao kwenye chama changu CCM, na pia mapenzi mazito ambayo watumishi wa UMMA (MAKADA WA CCM) kutoka taasisi mbalimbali za Umma, Idara za Serikali na Watumishi toka Halmashauri mbali mbali nchini walivyoonyesha moyo kwa kukipenda na kukipigania chama toka mchakato ulipoanza tarehe 14/07/2020 hadi leo hii ulivyohitimishwa kwa kutaja majina tarehe 20/08/2020.

Makada hawa (watumishi walio tia nia) wamevumilia mengi na bado wanakipenda chama Chao – CCM, nakuomba fumba macho Mheshimiwa Mwenyekiti ili mwezi huu walipwe mshahara wao ili waweze kuwa na nguvu ya kuendelea kukipigania chama hadi hapo October, 28 mwaka huu na kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa Chama chetu – CCM.

NB: Kwa walio karibu na Mheshimiwa M/KITI WA CCM – TAIFA na ambaye pia ndio Rais wa JMT, naomba mumfikishie ujumbe huu pasipo kupunguza maneno ili aweze kutumia hekima na busara zake kwa hawa Makada walio jitoa majimboni kukipigania chama chetu – CCM.

Nakala kwa :


  • Katibu Mkuu wa CCM – TAIFA, Dkt. Bashiru Ally (Aione kwenye Jalada)
  • Katibu Mkuu – UTUMISHI – Dkt. L. Ndumbaro
  • Makamu Mwenyekiti wa CCM – TAIFA, Mzee Mangula
  • Katibu wa NEC – Itikadi na Uenezi, Ndugu H. PolePole
Mheshimiwa M/KITI WA CCM TAIFA nakutakia Afya Njema, Mungu azidi kukubariki na upate Ushindi Mnono hapo Octoba 28, mwaka huu.
 
7 ELEVEN,

Kiukweli mimi siipendi CCM, ila hao wafanyakazi walipwe, ni stahili yao na ni haki yao. Kila mtanzania ana haki kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa katika uongozi. Kwanini viongozi wa umma wawe punished kwa kutamani kuwa viongozi? Hii si sawa. Huyo mwenyekiti wao wa chama mwenyewe asingekua hapo alipo bila tamaa. Alikua mwalimu wa kemia, akautamani ubunge, akaupata, akateuliwa kuwa naibu waziri, akaja kuwa waziri kamili, na mbali zaidi akautamani uRais na akaupata.

This is how we get leaders. Huwezi kumnyima mtu mshahara wake kisa kaomba nafasi ya uongozi. Tena kibaya zaidi unaweza kuta fomu aliiomba siku isiyo ya kazi. This is NONSENSE!!
 
Tatizo mna tamaa na muheshimiwa alishalisemea hili! Hapa umekuja kwa gia ya kupigania chama..hebh subirini uchaguzi upite kisha muandike tena barua tuangalie kama kuna nafasi!
 
Tatizo mna tamaa na muheshimiwa alishalisemea hili! Hapa umekuja kwa gia ya kupigania chama..hebh subirini uchaguzi upite kisha muandike tena barua tuangalie kama kuna nafasi!
Una maana kuwa kiongozi au kugombea nafasi fulani ya uongozi ni tamaaa? Huenda labda mimi sijakuelewa.

Una maana waliokuwa ma Rais mfano Nyerere, Mkapa, Mwinyi, Kikwete na hata Rais wa sasa waligombea hizo nafasi mbali mbali kwa sababu ya tamaa zao ? Nifafanulie hilo mkuu.
 
Una maana kuwa kiongozi au kugombea nafasi fulani ya uongozi ni tamaaa? Huenda labda mimi sijakuelewa.

Una maana waliokuwa ma Rais mfano Nyerere, mkapa, mwinyi, kikwete na hata Rais wa sasa waligombea hizo nafasi mbali mbali kwa sababu ya tamaa zao ? Nifafanulie hilo mkuu .
Nimemnukuu mkuu wa kaya..!
 
Kwa kweli hiki chama kitabaki na ukiwa sana. Mikwara ya polepole ni fake tupu. Watoa rushwa wengi wamepenya. Imani na upendo wa hao makada 7000 kwa ccm yanaelekea zerooo
Absolutely ! Unalolisema ni sahihi na ndio tumeshauri busara itumike ili kuondoa hili sononeko la hawa watumishi wa Umma ambao ni makada waliojitoa kukipigania chama chao majimboni.

Kinyume na hapo nafikiri majibu yatapatikana na viongozi wa Chama watakuwa tayari wameshachelewa kuziba huo ufa ndani ya chama .
 
nadhan utawala huu haupo upande wa watumishi hata kidogo kuanzia ulipo chaguliwa mpaka Leo tulipo ona watumishi kibao wamejitokeza kugombea kupitia ccm tukajua mambo yatabadilika labda utawala utarujirud kwa watumish kwa kuona wanaungwa mkono bwana weeee kumbe ndo wamelizua kabisaa na usishangae kesho unatoka waraka mwingine kusema wasirudi kazin kabisaaaaa mpaka wafe na wakome

watumishi, watumishi, watumishi Ccm sio chama cha wakulima na wafanyakazi tena badilikeni angalie jaribuni kwingine mmesha ona kupitia wenzenu walio nyolewa, asanten rais hawa watu wasirudi kabisaaaaa kazini akili iwakae sawa mana kila ukiifundisha jinsi ya kuikataa Ccm yenyewe haielew
 
nadhan utawala huu haupo upande wa watumishi hata kidogo kuanzia ulipo chaguliwa mpaka Leo tulipo ona watumishi kibao wamejitokeza kugombea kupitia ccm tukajua mambo yatabadilika labda utawala utarujirud kwa watumish kwa kuona wanaungwa mkono bwana weeee kumbe ndo wamelizua kabisaa na usishangae kesho unatoka waraka mwingine kusema wasirudi kazin kabisaaaaa mpaka wafe na wakome

watumishi, watumishi, watumishi Ccm sio chama cha wakulima na wafanyakazi tena badilikeni angalie jaribuni kwingine mmesha ona kupitia wenzenu walio nyolewa, asanten rais hawa watu wasirudi kabisaaaaa kazini akili iwakae sawa mana kila ukiifundisha jinsi ya kuikataa Ccm yenyewe haielew
Una hasira nao sana mkuu enhee?
 
Back
Top Bottom