OMBI: Serikali iikumbuke mikoa ya pembezoni hasa Kigoma. Hali ya barabara na umeme siyo nzuri

sambulugu

JF-Expert Member
Jun 1, 2021
687
1,000
Nasema hivo kwa sababu barabara ya kuanzia Nyakanzi, Kakonko, Kibondo, Kasulu inajengwa na imeikamilika baadhi ya maeneo ila eneo la Kibondo mpaka Kasulu bado mkandarasi naona uwezo wake mdogo.

Kwa upande wa umeme tunashukuru Makamu wa Rais kumsisitiza sana Waziri Makamba kulivalia njuga suala la mkoa wa Kigoma kuunganishwa kwenye grid ya taifa.

Maombi yangu Wanakigoma na wanasiasa wote wa Kigoma tushirikiane sana na Serikali pamoja na Makamu wetu wa Rais kuihamasisha Serikali kuwekeza haraka na kumaliza miundombinu hiyo.

Serikali pia ijitahidi sana kuongeza usimamizi wa mipaka ili kupunguza usumbufu kwa wananchi kuulizwa uhalali wa uraia wao, Serikali ikiweka wafanyakazi wa uhamiaji wengi na ikishirikiana na wanachi tatizo hilo litapungu.

Mkoa wa Kigoma sasa ni muda wake wa kufunguka kwa kuwa miaka ya nyuma tumekuwa na wanasiasa wazuri lakini hawakuweza kuishawishi Serikali lakini sasa tunaye Makamu wa Rais Dkt. Mpango. Tusaidie sana kwenye hili si kwa upendeleo ila pia kwa kutambua kuwa limekuwa tatizo kwa wenzetu kwa miaka mingi hali iliyopelekea hata uwekezaji kwenye mikoa hii kuwa nyuma.

Asanteh!
 
Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
2,285
2,000
Kwa kuwa kigoma kuna Makamu wa Rais haitakiwo kupewa maendeleo yeyote.Hata magufuri kwa kuwa kwao no choka mbaya..alipojaribu kupeleka maendeleo amabyo tayari yaok mikoa na wilaya zingine,,tulisema amejipendelea..kutokana na hilo licha ya kigoma kuwa nyuma haitakiwi kupewa maendeleo kwa sbb inamakamu wa Rais
 
Mmmmmm lakini mpango upo tokea kwa Jk! Magufuli kaukuta sasa mama Samia amalizie! Kama mateso sasa yatosha!
 
Eng peter pan

JF-Expert Member
Sep 15, 2021
972
1,000
Nasema hivo kwa sababu barabara ya kuanzia Nyakanzi, Kakonko, Kibondo, Kasulu inajengwa na imeikamilika baadhi ya maeneo ila eneo la Kibondo mpaka Kasulu bado mkandarasi naona uwezo wake mdogo...
Dah kila nikisikia barabar naskia saut inasema MTANIKUMBUKA
 
Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
2,285
2,000
Mmmmmm lakini mpango upo tokea kwa Jk! Magufuli kaukuta sasa mama Samia amalizie! Kama mateso sasa yatosha!
Kwa mjibu wa wapinzani na ccm wa kutoka pwani..apanatoko kiongozi hapatakiwi kuendelezwa
 
Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
2,285
2,000
Hao wapumbavu sana wengi wao ni chaggagang! Wanataka maendeleo kwao tu ili wabaki wakicheka wenzao!
Kwa magufuri kupeleka maji kidogo makao makuu ya walaya tunaambiwq ni miradi ya matrillion..swali huko mikoa mingine mbona maji yapo lakini hawakutaka wilayani kwa magufuri pawe na maji..why?

Kwanini hawataki ajenge hospital pale chato ingawa sehemu zingine kunahospital na wataalam wengi..je kule hawastahili kuwq na hospital nzuri?
 
TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
8,684
2,000
Wale wa Mtwara, Mara, Bukoba na nyie mje na mada zenu huku, hiyo mikoa ina matatiza ya barabara za kutoka au kuingia mjini kuliko kawaida.
 
Dec 31, 2017
10
45
P
Nasema hivo kwa sababu barabara ya kuanzia Nyakanzi, Kakonko, Kibondo, Kasulu inajengwa na imeikamilika baadhi ya maeneo ila eneo la Kibondo mpaka Kasulu bado mkandarasi naona uwezo wake mdogo.

Kwa upande wa umeme tunashukuru Makamu wa Rais kumsisitiza sana Waziri Makamba kulivalia njuga suala la mkoa wa Kigoma kuunganishwa kwenye grid ya taifa.

Maombi yangu Wanakigoma na wanasiasa wote wa Kigoma tushirikiane sana na Serikali pamoja na Makamu wetu wa Rais kuihamasisha Serikali kuwekeza haraka na kumaliza miundombinu hiyo.

Serikali pia ijitahidi sana kuongeza usimamizi wa mipaka ili kupunguza usumbufu kwa wananchi kuulizwa uhalali wa uraia wao, Serikali ikiweka wafanyakazi wa uhamiaji wengi na ikishirikiana na wanachi tatizo hilo litapungu.

Mkoa wa Kigoma sasa ni muda wake wa kufunguka kwa kuwa miaka ya nyuma tumekuwa na wanasiasa wazuri lakini hawakuweza kuishawishi Serikali lakini sasa tunaye Makamu wa Rais Dkt. Mpango. Tusaidie sana kwenye hili si kwa upendeleo ila pia kwa kutambua kuwa limekuwa tatizo kwa wenzetu kwa miaka mingi hali iliyopelekea hata uwekezaji kwenye mikoa hii kuwa nyuma.

Asanteh!
Pamoja na miundombinu hiyo ,tunahitajika kujenga nyumban ili kutia chachu ya mabadiliko kuendana na wenzetu wa kili na kagera
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom