Ombi: Serikali iangalie vizuri bei za mbolea zilizoongezeka hivi karibuni

ndenjii handsome

JF-Expert Member
Apr 27, 2021
579
1,000
Husika na kichwa cha mada hapo juu

Serikali yangu pendwa ya Tanzania na wahusika wa hili mimi kama mwananchi na mkulima wa nchi hii

Tunaomba muangalie vizuri kwenye suala hili la mbolea kiukweli mbolea ipo juu sana na sio rafiki kwa mkulima huyu wa chini

Na ukizingatia mazao yenyewe soko lake ni dogo na sehemu nyingine hakuna ksbisa soko mfano Ruvuma
Kilo ya maind ni kg1=240

Na wanunuzi wenyewe wakusopoka sasa kwa hali hiyi sizani kama kuna mkulima atarudi shamban msimu unaokuja

Hebu tuweke siasa kwanza pemben mtusaidie kwanza wananchi kwa hili maana tusipoingia tena shamba kwa kukosa hizo mbolea madhara yake.

Taifa litaingia kwenye upungufu wa chakula na hamtoweza kulisha taifa lote hili kwa hizo akiba mlizojiwekea

Waziri husika angalia hili siasa weka pemben tupambambanie wananchi wako ili tuendelee kulipa tozo yetu pendwa ya kizalendo
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,441
2,000
Kilichopandisha bei ya mbolea ni kupanda bei katika soko la dunia au kodi za serikali? Kama ni kodi, serikali ijitafakari; kama kuna vitu sio vya kuchezea basi ni pembejeo kwa wakulima.
 
ndenjii handsome

JF-Expert Member
Apr 27, 2021
579
1,000
Kilichopandisha bei ya mbolea ni kupanda bei katika soko la dunia au kodi za serikali? Kama ni kodi, serikali ijitafakari; kama kuna vitu sio vya kuchezea basi ni pembejeo kwa wakulima.
Wanadai kupanda huku kumesababishwa na india na china kuitaj kwa wingi mbolea sasa sijajua kivipi? Haya alisema waziri husika.
 
Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
9,962
2,000
Mabeberu wemeshachukua nchi mkuu, tulie tu.Ila tulishaonya,hasa ukizingatia background ya huyu mama na mume wake. Hawa wote wamefanya kazi muda wao wote kwenye NGOs za mabeberu, na NGOs zipo kwa ajili ya kuendeleza agenda za mabeberu!Sasa unategemea nini. It's like expecting to get ice from fire.
 
Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
1,375
2,000
Halipo kwenye ilani alafu CDM mnalalamika Sana mbona sisi kijani maisha ni mepesi UVCCM tunapata teuzi kila uchwao " alisikika mlevi mmoja akisema
 
Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,529
2,000
Taarifa isiyo rasmi toka kwa mfanyakazi wa muuzaji/muingizaji mkubwa wa mbolea kwa nchi za Afrika Mashariki anasema kulikuwa na mgomo kwa watengenezaji/waagizaji wa mbolea nchi nzima dhidi ya utaratibu flani uliowekwa na serikali.

Akasema mgomo umeisha kwa muda kwa hivyo mbolea nyingi sana zimeagizwa toka nje. Tutazipata madukani kuanzia tarehe 20 na kitu August 2021.

Hali ni mbaya sana, mazao yanadumaa hakuna mbolea madukani na chache inayopatikana inauzwa bei kubwa sana mkulima analima kwa hasara.
 
ivunya

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
2,005
2,000
Serikali yangu pendwa ya Tanzania na wahusika wa hili mimi kama mwananchi na mkulima wa nchi hii
Serikali hii ni Serikali ya wafanya Biashara siyo wakulima.
Sina kumbukumbuka kama Rais amekutana na wakulima.
Bei za vitu kila kukicha zinapanda juu ,Serikali ipo kwenye hatua za kukuza Uchumi
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
55,166
2,000
Serikali ya CCM haina huruma na yoyote kwa raiya kwadababu wanajua hamna cha kuwafanya kwenye sanduku la kura simply kwasababu hata wakiiba kura wananchi wanasema hewalaaa!
 
ze-dudu

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
14,967
2,000
Mabeberu wemeshachukua nchi mkuu, tulie tu.Ila tulishaonya,hasa ukizingatia background ya huyu mama na mume wake. Hawa wote wamefanya kazi muda wao wote kwenye NGOs za mabeberu, na NGOs zipo kwa ajili ya kuendeleza agenda za mabeberu!Sasa unategemea nini. It's like expecting to get ice from fire.
Aibu naona mimi

Au ni njaa ndio inakusumbua
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,095
2,000
Mabeberu wemeshachukua nchi mkuu, tulie tu.Ila tulishaonya,hasa ukizingatia background ya huyu mama na mume wake. Hawa wote wamefanya kazi muda wao wote kwenye NGOs za mabeberu, na NGOs zipo kwa ajili ya kuendeleza agenda za mabeberu!Sasa unategemea nini. It's like expecting to get ice from fire.
Yaani MWENDAZAKE MASALIA , mna shida kweli, toka october mwaka jana mafuta ya kula yalipopanda sana bei, ambayo hadi leo yako juu, alikuwa nani rais?, saruji mwaka jana ilipopanda bei nani alikuwa rais?mwendazake alikuta bei ya sukari 1800, leo hii ni bei gani?tatizo la nchi hii wala sio kiongozi kama kiongozi bali ni chama kinachotoa hao viongozi, hawana huruma na mwananchi, na ni kutokana na upimbi wa mwananchi, kila yamekuwa ni majitu ya kudanganywa tu na kukubali, tena hao wakulima ndio sio wa kuonea huruma kabisa, kwani ndio marafiki zao wakubwa wakati wa chaguzi., naomba tu hata mfuko wa UREA uuzwe 200, 000/ kabisa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom