Ombi:Riziwani inunue Yanga inakufa hivyo,au ongea na mshua aokoe jahazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombi:Riziwani inunue Yanga inakufa hivyo,au ongea na mshua aokoe jahazi

Discussion in 'Sports' started by Saint Ivuga, Dec 27, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Maji yamfika shingoni Papic.Mbioni kujiuzulu iwapo... [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 26 December 2011 21:12 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Kocha Kostadin Papic

  Vicky Kimaro
  'NDOA' ya Kocha Kostadin Papic na klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, haijasimama kwenye mstari ulionyoka na kwa sababu hiyo, huenda akaachia ngazi kama uongozi hautarekebisha kasoro zilizopo.Jana, Papic aliyerejea kuifundisha Yanga kwa mara ya pili, alikutana na waandishi wa habari na kueleza wazi jinsi mambo yalivyo magumu Jangwani.Katika mengi aliyoeleza mbele ya waandishi, msingi mkuu wa malalamiko yake ni kutengwa kiushirikiano na viongozi wa Yanga.Papic alisema hapati ushirikiano wa kutosha toka kwa viongozi wa klabu hiyo pamoja na jitihada kubwa ya kufanya nao mawasiliano.
  "Ni kama wamenitenga, hatuwasiliani kama inavyopaswa kuwa, napiga simu zao hawapokea na wakati mwingine hazipatikani."Unafanya vipi kazi na watu wasiokuwa ushirikiano hasa katika kipindi hiki timu inakabiliwa na michuano ya kimataifa," alisema.
  "Klabu ina hali mbaya kifedha, mimi na wachezaji hatujalipwa mishahara yetu mpaka leo na uongozi umekaa kimya bila kusema lolote," alilalama Papic.Alisema wachezaji wake wamekaa kimya lakini haina maana kwamba wanafurahishwa na hali ya mambo ndani ya klabu.
  "Wachezaji wangu hawajasema lolote, lakini kwa kuwangalia wanaonekana kuumia na hali hii ya kutolipwa mshahara mpaka sasa. Sura zao matumaini zimepotea kabisa."
  Alisema anashangazwa na ukimya wa uongozi wa Yanga katika kipindi ambacho wanakabiliwa na mtihani mgumu wa mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Zamalek.
  Papic aliyewahi kufundisha soka nchi kadhaa Afrika, alisema katika mazingira magumu kama hiyo si rahisi kuwaandaa wachezaji kupata ushindi."Siyo kwamba najitetea, lakini kama timu itashindwa kufanya vizuri kwenye mechi hiyo, basi asilaumiwe yeye wala wachezaji wake."
  "Hatujafanya mazoezi kwa siku saba ukiacha siku tatu za mvua. Mbali na mazoezi ya uwanjani hata Gym hatujakwenda.
  "Nimechukua jukumu la kuwakumbusha mara kwa mara viongozi kushughulikia suala hili, lakini mpaka leo sijapata jibu la maana.Papic amesema amekata tamaa ya kufanya vizuri kwenye mechi hiyo kwa vile uongozi wake umesema wazi hauna pesa."Hakuna mazoezi, hakuna mechi za kirafiki ukiuliza unaambiwa wiki ijayo, kila siku wiki ijayo, hakuna kinachotekelezwa.
  "Nimeomba mechi sita za kirafiki za kimataifa lakini hakuna kinachotekelezwa mashabiki wasije kuwalaumu wachezaji kwa lolote hali halisi ndio hiyo.Kuhusu mkataba wake na Yanga, Papic alilalamika kutothaminiwa, akitoa mfano wa kuishi kwenye mazingira magumu baada ya nyumba aliyopangishiwa kukatwa maji na umeme.
  "Hali ni ngumu kwangu binafsi na kwa wachezaji wangu, kuamua kwangu kuzungumza ni kwa sababu hali imefika hatua ambayo haipaswi kuvumiliwa."Kujiuzulu ni silaha yangu ya mwisho lakini kwanza napambana, kusaka wadhamini na wadau wa kutusaidia iwapo itashindikana sitakuwa na jinsi," alisisitiza.
  "Yanga ina wanachama na mashabiki wengi, ni vizuri wakasikia kilio hiki na kujitokeza kusaidia ili timu ipate mahitaji na kujiandaa vizuri."

  Kabla ya kutua Yanga pia aliwahi kufundisha timu za Orlando Pirates, Maritzburg United, Kaizer Chiefs na Hearts of Oak.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  tatizo hiyo timu kila kitu inamtegemea manji sasa hapo si ajabu kasafiri nje ya nchi kwa ajili ya mapumziko ya christmas na new year namjua yusuf,mida hii kumpata bongo ni ngumu,hiyo ni mpaka kwenye tarehe january ndio mtamuona hapo bongo...
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  jamaa wanatia huruma..zamaleki atapiga goli mia kwa uzembe wao na kuleta politcs kwenye futboli
   
 4. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,725
  Likes Received: 3,143
  Trophy Points: 280
  Ainunue kwa kutumia pesa ya nani? Hawa mafisadi bado mnawahitaji? Acha ife kwani ikifa itakuwaje? Bora ife kuliko mtu kama huyu anayeitwa nani sijui kwa kutumia pesa yetu walipa kodi aseme ni yake na aendelee kutunyanyasa.
   
 5. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Davis Mosha wa Kiboriloni si huwa anawapa hela mara moja moja? Wamtafute awape hela au naye yupo mapumziko?
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  wewe unafikiri riz hana pesa?
   
 7. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,725
  Likes Received: 3,143
  Trophy Points: 280
  Pesa za dhuluma, pesa za jasho la walipa kodi, pesa za watanzania.Hizi ndizo pesa zake au kuna lingine???? next!
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  hizo hizo pesa za wavuja jasho kuliko azipeleke kwenye mabenki nchi za nje bora zitumika hapa hapa nchini.
   
Loading...