Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,502
- 4,408
Kwako mkuu wa nchi yetu Mhe.Samia Suluhu Hassan kijana wako nina ombi mahususi si kwa ajili yangu ila kwa maslahi mapana ya taifa letu, kwa heshima na taadhima naomba nichukue muda wako kulifikisha mbele yako.
Ombi langu ni moja tu nalo ni kumteua Dkt.Bashiru kuwa waziri wako wa TAMISEMI au Nishati. Kuna mengi tumeyasikia juu ya kiongozi wetu huyo ambayo bado umma haujathibitishiwa lakini bado ni mtu anayekufaa Sana kwenye ujenzi wa Taifa letu.
Sina maslahi yoyote binafsi na uteuzi wake, kwangu ninaangalia ni Nani anayefaa kukusaidia kusogeza gururumu hilo zito mbele. Wahenga wanasema " mzigo mzito mpe mnyamwezi" , kwa uwezo na uzalendo alionao Dkt. Bashiru ndio mnyamwezi anayefaa kufikisha hiyo mizigo( wizara ya TAMISEMI na Nishati)
Pia, nikiri kusema sio kwamba waliopo Sasa ninachuki nao binafsi au hawawezi kufanya kazi hapana wanaweza sana ila kwa kuwa tumetofautiana uwezo wa kutenda, kuamua na kufikiri basi ni ukweli kwamba Dkt.Bashiru kawaacha katika hayo.
Tukiachana na yote , ukali,uwezo na uzalendo wa kweli wa Dkt.Badhiru bado unahitajika na utumie kama silaha ya kukujenga zaidi kisiasa. Ni Imani yangu Dkt.Bashiru atakuwa msaada mkubwa kwa ujenzi wa Tanzania yetu,ni mthubutu, hodari na jasiri na mwenye misimamo ya dhati.
Mwisho, naomba nichukue kukupongeza kuwa juhudi na jitihada mbalimbali unazozitumia kujenga nchi yetu. Kama kijana nazidi kukuombea hekima na busara zaidi ya kuongoza, kutenda na kuamua.
Wako katika ujenzi wa Taifa
Ni Mimi kijana mzalendo.