OMBI: Rais amteue Kafulila kuwa mbunge ili kunogesha mapambano ya ufisadi

Nicholaus Kilunga

JF-Expert Member
Feb 15, 2014
1,173
1,250
OMBI

Ili kunogesha na kutia nguvu zaidi katika mapambano na vita dhidi ya rushwa kubwa na ndogo,ufisadi na uhujumu uchumi,vita ambayo ameonekana mh rais Magufuli anaipigana na ili aweze kuishinda inabidi mh rais awe na maaskari hodari na wenye weredi wa kupambana katika vita hii ngumu na ya muda mrefu,namshauri mambo makubwa yafuatayo

1:Mosi aache kuwaona wapinzani kama maadui zake na maadui wa nchi,ama kuwaona si wazalendo kwa kuamini kila anaemkosoa ni sehemu ya wezi.
2:Asione aibu kuwaita na kukaa nao meza moja na kupokea hoja zao za msingi,kwa maana meza humaliza jambo gumu,kama ameweza kukubali kukaa meza moja na watu tunaowatuhumu kutuibia madini miaka dahali nafikiri hili halitamshinda kama anadhamira ya kweli.

3:Akubali na kuruhusu mijadala ya kumkosoa yeye kama rais,akubali serikali yake ikosolewe na chama chake pia,kuanzia ndani ya bunge,nje ya bunge na kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,ili mradi ukosoaji uwe wa staha,lugha isiyouzi na ukweli na heshima.

4:Kuanzia sasa awe anatoa hotuba za kuliunganisha taifa zaidi,na aepuke kuongea ama kusema jambo lolote litakalotafsiriwa kama kutugawa watanzania,mfano kusema kushirikiana na wapinzani nk,aunganishe taifa zaidi ili aweze kuungwa mkono na watu wote wenye itikadi na mitazamo tofauti ili kuijenga nchi kizalendo.

5:Mwisho ila sio kwa umuhimu,nimwombe sasa mh rais amteue David Kafulila kuwa mbunge katika bunge la jamhuri TZ,kama hilo linawezekana,kwani nafahamu bado anazo nafasi 2,huyu ni kiungo muhimu sana katika vita hii,kama ingekuwa jeshini mstari wa mbele kule vitani tungemwita runer(wale askari maalumu wanaotumwaga kusafisha eneo na kumchokoza adui ili ajulikane yupo wapi na jeshi zima baadae limshambulie)kwa kauli ya David Kafulila mwenyewe rais Magufuli wakati huo alikuwa ni miongoni mwa mawaziri 5 waliomtia moyo Kafulila ili aendelee kupambana kwa kumwambia escrow ni dili na akomae mpaka mwisho,

mh rais uwezo wa Kafulila katika kujenga hoja unaufahamu,uzalendo wake sio wa kutilia shaka,maana asingekuwa mzalendo haswaa sakata la escrow lisingemwacha salama,maana walijaribu mara kazaa kumuhonga na waliposhindwa walimtishia maisha,hivyo mh watanzania tunamuhitaji zaidi mh Kafulila bungeni ili aende kuliamsha dude,na unafahamu ni kwa namna gani Kafulila alifanyiwa figisu ili asirudi bungeni,na hata alipojaribu kwenda mahakamani,wote tunajua yaliyotokea,na watuhumiwa wa escrow walikuwa nyuma kuhakikisha harudi bungeni kama kumkomoa kwa lugha yao wao walisema walipokea maagizo ya "kumfix"
 

ngosha wa mwanza

JF-Expert Member
Feb 23, 2015
880
1,000
Na kweli mkuu maana km atajaribu kuwasikiliza wapinzani na kumchukua kafulila nchi hii itakua na mijadala mipana na c hao wanasema ndiooo tu
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
10,687
2,000
Rahisi bado ana nafasi 1......imebakia....huwa hawezi kuitoa labda kama bado miezi 6 tu!! Nakumbuka JK alimpa dada mmoja kama bado miezi 6 hivi.....!!!!
 

Nicholaus Kilunga

JF-Expert Member
Feb 15, 2014
1,173
1,250
wala mh asione aibu kwenda kinyume na kauli yake aliyoitoa kule Zenji kwamba hatateua wapinzani katika serikali yake,utaifa unahtajika zaidi
 

data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
22,411
2,000
Mbatia alimgeuka Kikwete...labda hicho ndo anahofia...
 

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,097
2,000
Si ametoka kusisitiza juzi tu wakati anamwapisha mama Anna mghwira kama nafasi ya ubunge imebaki moja tu na hiyo hatampa MTU wa upinzani!
Au Mara hii watu mmeshasahau.......
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,092
2,000
Si ametoka kusisitiza juzi tu wakati anamwapisha mama Anna mghwira kama nafasi ya ubunge imebaki moja tu na hiyo hatampa MTU wa upinzani!
Au Mara hii watu mmeshasahau.......
Usimwamini mwanasiasa, au umeshasahau?
 

othiambo

JF-Expert Member
Nov 15, 2014
1,588
2,000
Wallah,Mungu analipa hapahapa,nakumbuka sana hudhuni ya kafulila akiojiwa na EATV akidai hakubaliani nna matokeo na atakat rufaa,huku ikionesha wazi zengwe aliloundiwa haliwezi.
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,092
2,000
KAFULILA:LEO NI SIKU MUHIMU KWANGU NA VITA DHIDI YA UFISADI!

Hatimaye imekuwa! Vinara katika ufisadi wa IPTL/ESCROW Singasinga Sethi na Rugemalila watiwa nguvuni. Huu ni uamuzi mkubwa uliosubiriwa sana. Na siku zote sikujua kwanini Mhe Rais alikuwa anahofu kuagiza hatua hii.

Sikujua kwanini kwasababu wakati wa mnyukano wa hoja hii, Mhe Rais alikuwa bungeni na alikuwa sehemu ya maazimio ya Bunge kutaka mitambo ya IPTL itaifishwe na wahusika watiwe nguvuni..

Nakumbuka nikiwa kwenye kipindi kigumu hata kutishwa kuondolewa kichwa na kuitwa majina ya wanyama, yeye alikuwa miongoni mwa mawaziri 5, walionidokeza kwamba ESCROW ni dili.nikomae tu mpaka kieleweke!

Nampongeza Mhe Rais kwa uamuzi huu muhimu uliosubiriwa siku nyingi kuamua hatma ya ufisadi huu uliomshinda vibaya mtangulizi wake.

Singasinga huyu alinifungulia kesi kunidai Sh300bn Mahakama Kuu ya Tanzania mwaka 2014, Agust2015 nikamshinda lakini akamua kunifungulia upya Mahakama ya Kisutu akidai Sh100m, zote akidai nimsafishe kuwa yeye na wenzake hawakuchota zaidi ya 300bn kifisadi.

Kifupi naomba PCCB na DPP wasituangushe watanzania. Nilipata kuwaza kumwomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali anipe kibali niendeshe kesi na hawa majabali wa escrow kwani nina ushahidi wakutosha,Sasa nina furaha kwamba PCCB wameamua kuwaburuza.

Nashauri mambo machache;

1.Mall zote za wahusika hawa ziwekwe chini ya ulinzi kabla hawajahamisha umiliki kwani nimuhimu zikakamatwa kusubiri hukumu ya kesi hii ya Tanzania lakini pia kesi iliyopo Mahakama ya kimataifa ya International Centre For Settlement of Investment Disputes (ICSID).Ambako Sept2016, iliamuliwa tulipe Bank ya SCB-HK kiasi zaidi ya 400bn kwakua ndio wamiliki halali wa IPTL na wenye share certificate za IPTL..

Mwaka huu TANESCO imekata rufaa.Najua TANESCO hawajakata rufaa kushinda kesi bali kuomba wapunguziwe hukumu ifanane na uamuzi wa ICSID wa Feb2014.

Lakini kwakuwa Singasinga Sethi alisaini hati na Bank Kuu ya Tanzania, kwamba deni lolote lotakalotokana na migogoro ya IPTL atawajibika yeye na wenzake wanaomiliki kampuni PAP, ndio maana nasisitiza Mali za watu hawa zishikiliwe.

2.Mtambo wa IPTL uwekwe chini ya TANESCO kama ilivoazimiwa na Bunge Nov2014, tuachane kabisa na kulipa matapeli 7bn kila mwezi ambazo ni malipo ya capacity charges walizokuwa wanalipwa na serikali hii bila kujali IPTL imezalisha au haijazalisha umeme.

3.Mwisho watanzania watambue kwamba huyu Singasinga anaetambulishwa kama mmiliki wa PAP iliyopora 300bn za escrow kama mmiliki mpya wa IPTL,mpaka pesa hizo zinaporwa alikuwa anamiliki asilimia50% tu yakampuni.lakini asilimia 50% zilikuwa zikimilikiwa na kampuni ijulikanayo kama SIMBA TRUST, inayomilikiwa na watu wasiojulikana. Hawajawahi kutajwa popote kwenye report zote.

Nilijaribu kutaka majina yao kwenye Kamati ya Viwanda wakati tukiwahoji BRELA na hata baadae bungeni Serikali iliendelea kusisitiza kuwa majina hayo ni SIRI.Hawa ni wahusika muhimu sana wajulikane kwani inawezekana ndio msingi wa serikali ya awamu ya nne kuibeba IPTL kama mtoto!

Naam, Hongera Mhe Rais kwa hatua hii, nazidi kuomba Mungu kesi hizi zifike mwisho kwani kwangu leo ni siku muhimu katika kumbukumbu zangu kuliko Aprili28,2015, siku niliyopewa tuzo kwa mapambano dhidi ya Ufisadi kwa rejea ya sakata la ESCROW. Kwani tuzo haina maana kama vita haifiki mwisho!

Mwisho nishauli asiwepo yeyote wakulindwa kwa Kinga yoyote kwani Katiba na Sheria vipo kwajili ya watanzania na sio watanzania kwajili ya Katiba na Sheria. Tusipofika huko vita ya UFISADI mkubwa itakuwa ngumu sana kufika mwisho!
David KAFULILA
JUNE19,2017
 

Nicholaus Kilunga

JF-Expert Member
Feb 15, 2014
1,173
1,250
Hakuna mpinga ufisadi angekubali kunadiwa na gwiji la rushwa mamvi, kafulila njaa kali hakuna mpingajiwa ufisadi hapo

umerukia hoja hii tena?ile ya awali ya kuwasifia CCM umeikimbia?itafika mahali tulazimike kuwapima wafuasi wa CCM huenda mnamwili wa binadamu akili ya ngiri mnyama maarufu kwa kusahau haraka,
ila kwa kukusaidia kama unaona aliemnadi Kafulila ni gwiji wa rushwa mshauri mwenyekiti wako ampeleke mahakamani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom