Ombi: Namna ya kuhamia Dodoma na CDA kukopesha viwanja

Eneo linauzwa dodoma ekari 40 lina hati miliki iliyokamilika...lipo karibu na ikulu ya chamwino
 
Dodoma kwa sasa ni better ukanunua viwanja vilivyopimwa from CDA. Kiwanja kinaanzia Sh. 2 m. ndio kizuri. Jipangeni kununua vikubwa au vilivyoungana ili familia ijimwage.
Hili eneo limepimwa na cda na ni la ukubwa huo ...na kila kitu kipo tayar
 
Mji wa Dodoma umupagwa vizuri, lami sehemu kubwa na kuna mitimiti. Chakula sio ghali kama Mwanza.
 
Ndio maana nimependekeza TBA, kwa sababu si siri tena Tanzania tulikuwa tukipigwa na construction company
Pia serikari inaweza kuja na bei elekezi ya nyumba
Hata viwanja vyenyewe bado Watanzania wanaibiwa, una kuta mita moja ya mraba ya 5000 inauzwa 8000, na ya kuuzwa 8000 inauzwa 10000
Ndugu Finite Automata, sisi kinachotuponza ni utamaduni. Tuna utamaduni wa kupenda kujenga hata kama ni kihenge. Kuna nchi (India) familia hadi wajukuu wanaishi nyumba ya kupanga kwa miaka hadi 50! Huko sio kila mtu anajenga, kwahiyo mipango unayosema inawezekana. Ni rahisi kwa serikali kujenga majengo yenyewe, badala ya wananchi.

Wananchi wataendelea kupigwa tu maana ndiyo sheria yetu ya manunuzi ya umma inayofanya hayo yatokee. Kitendo cha kuipa TBA kazi bila kutangaza tenda ni ukiukwaji wa sheria ya manunuzi ya umma.
 
Kwani watumishi wanaohamia Dom kutokea Dar wana umaalum gani mpaka wakopeshwe viwanja na mbwembwe kibao? Ni kusema wote wana nyumba Dar? Hamjawahi kupanga nyumbani huko?

Ikiwa watumishi walioko Dom hawajawahi kukopeshwa viwanja na CDA sasa wataanzaje kwa hao wanaotoka Dar? Let us be realistic, watu wa dar wasitake kujiona wao ni maalumu kuliko watumishi wengine.

Kwa kupunguza gharama, ni vema watumishi wanaohamia Dodoma toka Dar na mikoa mingine waje kwa kutumia usafiri wa treni na magari ya mashirika ya umma, hii ni pamoja na yale ya Jeshi la Wananchi, Magereza na kadhalika. Hii itasaidia kubeba mizigo.

Tusichukulie kuwa kuhamia Dodoma ndio watu wengi watatoka Dar na kuja Dom. Dodoma pia kuna watendaji wa Serikali, hivyo nadhani watakao kuja ni wale watendaji wakuu kitaifa na sio ki mikoa mfano toka Kinondoni,Temeke ....???.

Ingependeza kama Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), kupima na kutoa mikopo ya viwanja kwa watumishi wa Serikali wanaohamia Dodoma. Hii itawahamasisha kuhamia, pia itawatoa katika midomo ya madalali na gharama ya ununuzi toka mikononi mwa watu.

Pendelezo kwa malipo yafanywe kwa muda ya miaka miwili, ili kuwapa fursa ya kujenga na kuhamia kwa muda mfupi.

Tujikumbushe kuwa kuhamia Dodoma, kunatupa fursa ya kujenga Taifa kiurahisi, yaani hadi vijijini kutafikika kuhurahisi. Dodoma ni katikati na kuna nafasi nzuri tu. Hali ya hewa ni nzuri sana, hakuna vumbi sana kama mnavyofikiria.

Twendeni Dodoma.
 
Back
Top Bottom