Ombi: Mkapa, it's now high time to shun away active politics

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Jana baadhi ya vyombo vya habari viliripoti Vincent Nyerere akimshukia Rais Mst Mkapa akijibu hoja kuwa yeye; Vincent si wa familia ya Mwl Nyerere. Hapa JF, topic hiyo ilichangiwa sana na leo MtanzaniA wameripoti Mkapa akiomba suluhu na Familia Mwl Nyerere kuhusu suala hilo.

Nimetafakari na kuona kuwa Mkapa alijiingiza kwenye mtego huo akiwa amechanganywa na harakati za CDM na kujisahau kuwa ushawishi wake umepungua sana.

MY TAKE
Ajitenge na siasa za ki CCM ili atumike mshauri na msuluhishi kitaifa.
 
Tatizo la huyu mkimbizi toka Msumbiji ni ubishi na kiburi, hawezi kupokea ushauri, sasa shauri yake, ameukalia msumari ngoja umchome.
 
Jana baadhi ya vyombo vya habari viliripoti Vincent Nyerere akimshukia Rais Mst Mkapa akijibu hoja kuwa yeye; Vincent si wa familia ya Mwl Nyerere. Hapa JF, topic hiyo ilichangiwa sana na leo MtanzaniA wameripoti Mkapa akiomba suluhu na Familia Mwl Nyerere kuhusu suala hilo.
Nimetafakari na kuona kuwa Mkapa alijiingiza kwenye mtego huo akiwa amechanganywa na harakati za CDM na kujisahau kuwa ushawishi wake umepungua sana.
MY TAKE
Ajitenge na siasa za ki CCM ili atumike mshauri na msuluhishi kitaifa.

Ila ukweli utabaki pale pale kuwa Vicent si mmoja wa wanafamilia ya MWALIMU bali ni mwanafamilia ya NYERERE.
 
Ila ukweli utabaki pale pale kuwa Vicent si mmoja wa wanafamilia ya MWALIMU bali ni mwanafamilia ya NYERERE.

Ndivyo Mkapa alivyosema au unamlisha maneno?
Vyovyote iwavyo, Mkapa atambue kuwa alikuwa Rais wa Watanzania wote, ni vema akae pembeni ili kulinda hadhi yake, yeye hana ubavu wa kupambana ktk siasa za maji taka anazoziasisi.
 
Napata tabu sana kuamini kuwa huyu mzee anaweza kuwa mshauri mzuri kwa ccm naona amepoteza dira kwanini asipumzike nilimkubali sana pale ambapo alikaa kimya sana kipindi cha kwanza cha utawala wa JK.
 
Kwa kweli sitarajii kumsikia tena Mkapa kwenye jukwaa la siasa ajifunze kwa mzee Rukhsa, Mwinyi mbona yuko kimya?
 
Raisi mstaafu Benjamin Mkapa itakuwa vizuri kwake kuachana na siasa za majukwaani kwa kuwa badala ya kumjenga kisiasa zinaelekea kumdhalilisha. Chama cha Mapinduzi nacho kimeona baada ya kushiriki kampeni za Igunga na kushinda ndo wamemuona yeye kuwa muarobaini wa chaguzi ndogo ili wagombea wao washinde. Igunga ufisadi alioufanya akiwa ikulu ulianikwa na sasa Arumeru ni yale yale. Kwa nini ccm inatumia watu wakubwa kama wale kwa chaguzi ndogo!? Wamuache mzee wa Lushoto apumzike la sivyo watamuua kwa pressure. Najua ccm ina makada wengi vijana, nadhani ni vema ikawatumia hao. Amuige mzee Mwinyi kajipumzikia kivyake yeye na dini na mikutano ya ndani na vikao yatosha. HUO NI USHAURI WANGU
 
Huyu mzee alisema hatajihusisha na siasa za ndani alipostaafu. Ni nini kilichomwamsha. Nakubali ya wahenga waliposema "ALIYELALA USIMWAMSHE". Hujui akikurupuka atafanya nini. CCM pamoja na mapenzi yenu kwa wastaafu waacheni wapumzike.
 
Back
Top Bottom