Ombi: Mh. RAIS kuhutubia Siku ya Mwisho wa Mwaka

Kitikiti

JF-Expert Member
Nov 4, 2015
353
250
Ni ombi kwa Mh. RAIS kulihutubia Taifa siku ya mwisho wa mwaka huu ya tarehe 31 December, 2016 kabla ya kuingia tarehe 01 January, 2017. Bado siku chache kufikia siku hiyo.

Ni utaratibu ambao Nchi nyingi ikiwemo Tanzania hulifanya. Kuna miaka mingine Viongozi hawaonekani na Wananchi tuna hamu ya kuwasikia na kupata busara zao. Nyakati hizo wengi huwa tuko macho na familia zetu.

Hotuba zao ujenga au kuendeleza upendo, haki, amani na furaha. Ni hotuba sio ya kisiasa sana, bali itawaliwe na upendo au uzalendo. Sio ya kidini, bali ya ki MUNGU.

Tunakuombea Afya njema.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRICA NA DUNIA KWA UJUMLA!. Amen
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,977
2,000
Nyie watu vipi? Mumeanza kukataa sauti yake hata ikiigizwa na comedians kwenye maharusi sasa mkimsikia redioni hamtazima redio zenu kweli? Hebu anzeni kwanza kupenda kusikia akiigizwa kwenye masherehe yenu na tunataka kusikia mkipiga kelele " Once moreeee!" Ndio tutapata kumshawishi ahutubie sio mwisho wa mwaka tuu, hata robo, nusu na thelusi ya mwaka.
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,958
2,000
Wewe ni nani hadi umshauri Mtukufu?

Kwani wewe hujui kuwa huyo jamaa hashauriki wala kuambilika?

Zaidi sana kwa ushauri huo usije ukajikuta unageuziwa kibao na kuitwa Mchochezi kwa kutaka kumjaribu Bwana yule!

Kwa kuwa Bwana yule kama angekuwa mpenda kushauriwa angelipenda jukwaa la JF kuliko jukwaa lolote hapa nchini kwa kuwa ndilo limekuwa chombo cha habari namba 1 ya ufichuaji wa maovu yote nchini, lakini badala ya kulienzi jukwaa hili badala yake anaombea 'Malaika' washuke toka mbinguni waje waizime JF!!
 
Kitikiti

JF-Expert Member
Nov 4, 2015
353
250
Nyie watu vipi? Mumeanza kukataa sauti yake hata ikiigizwa na comedians kwenye maharusi sasa mkimsikia redioni hamtazima redio zenu kweli? Hebu anzeni kwanza kupenda kusikia akiigizwa kwenye masherehe yenu na tunataka kusikia mkipiga kelele " Once moreeee!" Ndio tutapata kumshawishi ahutubie sio mwisho wa mwaka tuu, hata robo, nusu na thelusi ya mwaka.
Muhimu ni neno na sio sauti.
 
takangumu

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
245
500
Unataka na utu uzima huu turudie kwenda kupokea mwaka night club sbb hata kanisani atakuepo mwenye kukujuza
 
Nyamtalakyono

JF-Expert Member
Dec 17, 2015
793
500
Ni ombi kwa Mh. RAIS kulihutubia Taifa siku ya mwisho wa mwaka huu ya tarehe 31 December, 2016 kabla ya kuingia tarehe 01 January, 2017. Bado siku chache kufikia siku hiyo.

Ni utaratibu ambao Nchi nyingi ikiwemo Tanzania hulifanya. Kuna miaka mingine Viongozi hawaonekani na Wananchi tuna hamu ya kuwasikia na kupata busara zao. Nyakati hizo wengi huwa tuko macho na familia zetu.

Hotuba zao ujenga au kuendeleza upendo, haki, amani na furaha. Ni hotuba sio ya kisiasa sana, bali itawaliwe na upendo au uzalendo. Sio ya kidini, bali ya ki MUNGU.

Tunakuombea Afya njema.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRICA NA DUNIA KWA UJUMLA!. Amen
Amen
 
Nyamtalakyono

JF-Expert Member
Dec 17, 2015
793
500
Wewe ni nani hadi umshauri Mtukufu?

Kwani wewe hujui kuwa huyo jamaa hashauriki wala kuambilika?

Zaidi sana kwa ushauri huo usije ukajikuta unageuziwa kibao na kuitwa Mchochezi kwa kutaka kumjaribu Bwana yule!
Nani kakwambia rais Magufuli hashauriki? Halafu nahisi uwezo wako wa kufikiri ni mdogo. Kwa taarifa yako Rais Magufuli ni Rais wa watanzania wote na yuko tayari kushauriwa na kila mtanzania.
 
Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,550
2,000
Unataka kututia gundu na mwaka mpya, unadhani nani anahamu na hotuba zake kwa sasa? Labda mleta uzi
 
Kisu Cha Ngariba

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
22,170
2,000
Nani kakwambia rais Magufuli hashauriki? Halafu nahisi uwezo wako wa kufikiri ni mdogo. Kwa taarifa yako Rais Magufuli ni Rais wa watanzania wote na yuko tayari kushauriwa na kila mtanzania.
Leo uko zamu? Wenzako kina Lizaboni wamekimbia. Nchi haina matumaini.
 
Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,550
2,000
Nani kakwambia rais Magufuli hashauriki? Halafu nahisi uwezo wako wa kufikiri ni mdogo. Kwa taarifa yako Rais Magufuli ni Rais wa watanzania wote na yuko tayari kushauriwa na kila mtanzania.
Watanzania wa rangi ya kijani labda, kama wa wote mwambie apeleke rambirambi za Bukoba Kwanza,
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom