Ombi maalumu kwa Dk Wilbrod Slaa: Anzisha chama cha siasa ili kiwe chama cha Upinzani

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
4,643
2,000
Hakika mkuu.nakumbuka ile siku mzee slaa anang’atuka alisema “sijawahi kutofautiana na mwenyekiti wangu lakini kwa hili la lowasa tumevutana sana.”””mzee ana msimamo sana yule
Dr. was the best of the best! Ile combination yake na Mbowe iliwaumiza sana CCM
 
Dp800

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,370

Yawezekana asiwe candidate mzuri wa urais lakini mchango wake ni muhimu sana kwenye muelekeo wa kuindoa ccm 2025, kwa Sasa ccm pamoja na Hangaya hawana chochote cha kufanya kuinusuru nchi wameamua kwa makusudi kuyazika mema yote ya JPM ni wakati muafaka wa kuvuna pando lao
 
Drifter

JF-Expert Member
Jan 4, 2010
3,407
2,000
Ni ukweli kabisa na falsafa za Dr. Slaa ndio falsafa za Magufuli nadhani hata ndio sababu za yeye kuumunga mkono

Kiukweli walio karibu wamuombee mzee afanye hilo jambo mapema mafisadi yamekuja na speed kali sana tusipojidhatiti mapema tutapoteza pambano.

Magufuli na Slaa wote mrengo wao ni mmoja uongozi kwa manufaa ya uma, usimamizi wa rasilimali tulizojaliwa pamoja na udhibiti wa rushwa na matumizi mabaya ya rasilimali.

Kikubwa nakiona kwa Dr. Slaa ni kuiamini vijana katika kupiga hatua ndio maana hata alipokuwa chadema kwa wakati wake aliweza kuwainuia vijana wengi sana zito,mnyika, mdee ni mifano hai

Wafuasi wa Magufuli msiokubaliana na CCM kubalini kuwa nje ya CCM hamna chenu. Ndivyo Tanzania ilivyo. Hata Magufuli ile jeuri na kibri alikuwa navyo kwa kushika rungu la CCM. Nje ya CCM hakuwa na tofauti na Cheyo.

Slaa ndio kabisaa. Hana chake. CHADEMA ndiyo ilikuwa nguvu yake hapo awali.
 
Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
4,643
2,000
Yawezekana asiwe candidate mzuri wa urais lakini mchango wake ni muhimu sana kwenye muelekeo wa kuindoa ccm 2025, kwa Sasa ccm pamoja na Hangaya hawana chochote cha kufanya kuinusuru nchi wameamua kwa makusudi kuyazika mema yote ya JPM ni wakati muafaka wa kuvuna pando lao
Mema yepi ya JPM waliyoyazika Chief?
 
Dp800

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,370
2,000
Mema yepi ya JPM waliyoyazika Chief?
Kama ulikuwepo Tanzania na hujayaona hata nitumie siku nzima kukushawishi sitafanikiwa hilo. Nadhani itoshe kusema maombi ya mtoa mada kwa Dr. Slaa yapokelewe kwa faida ya Tanzania ya sasa na baadae
 
Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
4,643
2,000
Kama ulikuwepo Tanzania na hujayaona hata nitumie siku nzima kukushawishi sitafanikiwa hilo. Nadhani itoshe kusema maombi ya mtoa mada kwa Dr. Slaa yapokelewe kwa faida ya Tanzania ya sasa na baadae
Chief orodhesha hata mema 3 tu ya JPM ambayo hayaendelezwi awamu hii, kushindwa kufanya hivyo ina maana wewe ni muongo na una chuki zako binafsi tu
 
Kanyawela

Member
Aug 22, 2015
98
125
Hapa utaibana Ccm kama enzi zile unaibana juu ya mafisadi papa na list of shame ukiwa Chadema.

Wewe unavyanzo kibao vya kupata data za wezi wa mali za umma. Ukiwa na chama chako utakuwa na nafasi kubwa kuibana Ccm.

Watanzania wanaimani kubwa na wewe, maana hauna historia ya upigaji madili. Hivyo utaungwa mkono na watanzania wengi.

Anzisha chama kiwe mbadala wa Chadema ambayo imelala chari kifo cha mende.
Ni ideology ya chama wala siyo sura ya mtu itakayoleta wafuasi
 
Dp800

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,370
2,000
Wafuasi wa Magufuli msiokubaliana na CCM kubalini kuwa nje ya CCM hamna chenu. Ndivyo Tanzania ilivyo. Hata Magufuli ile jeuri na kibri alikuwa navyo kwa kushika rungu la CCM. Nje ya CCM hakuwa na tofauti na Cheyo.

Slaa ndio kabisaa. Hana chake. CHADEMA ndiyo ilikuwa nguvu yake hapo awali.
Maoni yako sio msaafu hivyo sitapinga unachoamini
Ila yeyote mwenye nia ya dhati ya kuikwamua Tanzania kutoka kwenye hali duni na usimamizi mbovu wa Tanzania yetu huyo ni rafiki yetu na ninaimini hiyo ndio sala ya watanzania wengi
 
Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
7,707
2,000
Hakika mkuu.nakumbuka ile siku mzee slaa anang’atuka alisema “sijawahi kutofautiana na mwenyekiti wangu lakini kwa hili la lowasa tumevutana sana.”””mzee ana msimamo sana yule
Halafu baada ya kuvutana na Mbowe, Dr. Slaa akarudi CCM na akawa mpiga debe wa CCM dhidi ya upinzani.
Huyo mtu atakuwa ana akili timamu kweli?

Yaani mtu aliyekuwa kwenye upinzani kwa miaka 20, akizunguka nchi nzima kuhakikisha CCM inaondolewa madarakani, ghafla anatofautiana na Mbowe kwa suala la Lowassa kuhamia CHADEMA na hapo hapo anahamia CCM kinyemela na kuhakikisha inapata ushindi.

Bora Yuda aliyemsaliti Yesu (maana usaliti wake ulizaa wokovu kwa wakristo) kuliko Slaa, mtu mpuuzi aliyehakikisha watanzania wanabakia kwenye utumwa wa CCM huku yeye akitafuna vitu vinono kwenye hoteli ya kifahari na kutunzwa Canada kwa pesa za wavuja jasho la watanzania.

Kuna uwezekano mkubwa sana kile kilichomkuta Yuda ipo siku kitamkuta Dr. Slaa, otherwise Dr. Slaa azunguke nchi nzima kuwaomba radhi watanzania kwa uovu wa kisaliti aliowafanyia watanzania kuanzia 2015.
 
Dp800

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,370
2,000
Ni ideology ya chama wala siyo sura ya mtu itakayoleta wafuasi
Ideology ya chama bila watu wenye dhamiri ya dhati kutekeleza hayo yanabaki kuwa maandiko tu.
Ndio maana hata CCM kwenye makaratasi wana hoja nzuri lakini watu walioshika hatumu ni mafisi na mafisadi. Kwa upande wa Dr. Kila mtu anafahamu integrity yake na muelekeo wake juu ya Tanzania ndio maana haikua shaka kwake kushirikiana na Magufuli sababu wana shabihiana mitazamo ingali hawakua chama kimoja
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,451
2,000
Hapa utaibana Ccm kama enzi zile unaibana juu ya mafisadi papa na list of shame ukiwa Chadema.

Wewe unavyanzo kibao vya kupata data za wezi wa mali za umma. Ukiwa na chama chako utakuwa na nafasi kubwa kuibana Ccm.

Watanzania wanaimani kubwa na wewe, maana hauna historia ya upigaji madili. Hivyo utaungwa mkono na watanzania wengi.

Anzisha chama kiwe mbadala wa Chadema ambayo imelala chari kifo cha mende.

Anzisheni chama - hata CCM yasemekana wamewachoka:

IMG_20211028_091647_207.jpg

IMG_20211028_091624_829.jpg

CCM jitengeni na kundi la Wasiojulikana
 
Dp800

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,370
2,000
Halafu baada ya kuvutana na Mbowe, Dr. Slaa akarudi CCM na akawa mpiga debe wa CCM dhidi ya upinzani.
Huyo mtu atakuwa ana akili timamu kweli?

Yaani mtu aliyekuwa kwenye upinzani kwa miaka 20, akizunguka nchi nzima kuhakikisha CCM inaondolewa madarakani, ghafla anatofautiana na Mbowe kwa suala la Lowassa kuhamia CHADEMA na hapo hapo anahamia CCM kinyemela na kuhakikisha inapata ushindi.

Bora Yuda aliyemsaliti Yesu (maana usaliti wake ulizaa wokovu kwa wakristo) kuliko Slaa, mtu mpuuzi aliyehakikisha watanzania wanabakia kwenye utumwa wa CCM huku yeye akitafuna vitu vinono kwenye hoteli ya kifahari na kutunzwa Canada kwa pesa za wavuja jasho la watanzania.

Kuna uwezekano mkubwa sana kile kilichomkuta Yuda ipo siku kitamkuta Dr. Slaa, otherwise Dr. Slaa azunguke nchi nzima kuwaomba radhi watanzania kwa uovu wa kisaliti aliowafanyia watanzania kuanzia 2015.
Mkuu lile genge lillohamia chadema ambalo lilimfanya Slaa akaicha kazi alioisimamia zaidi ya miaka 20 nitajie ni nani bado yupo chadema. Dr aliliona hilo na hakutaka kuwa sehemu ya upuuzi ule ndio maana aligoma kata kata kuinajisi dhamira yake.
Itoshe kusema alikuja lengo la wale waliokuja sio kujenga bali maslahi binafsi ambayo yanakinzana na yake aliyo huburi siku zote.
 
Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
5,117
2,000
Hapa utaibana Ccm kama enzi zile unaibana juu ya mafisadi papa na list of shame ukiwa Chadema.

Wewe unavyanzo kibao vya kupata data za wezi wa mali za umma. Ukiwa na chama chako utakuwa na nafasi kubwa kuibana Ccm.

Watanzania wanaimani kubwa na wewe, maana hauna historia ya upigaji madili. Hivyo utaungwa mkono na watanzania wengi.

Anzisha chama kiwe mbadala wa Chadema ambayo imelala chari kifo cha mende.
Utitiri wa vyama utaleta unafuu zaidi kwa ccm.
Ifike mahali tukubaliane kuwa tunahitaji vyama viwili tu vya siasa!
Ikiwa hivyo tutafika mbali sana!
 
ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
11,771
2,000
Hapa utaibana Ccm kama enzi zile unaibana juu ya mafisadi papa na list of shame ukiwa Chadema.

Wewe unavyanzo kibao vya kupata data za wezi wa mali za umma. Ukiwa na chama chako utakuwa na nafasi kubwa kuibana Ccm.

Watanzania wanaimani kubwa na wewe, maana hauna historia ya upigaji madili. Hivyo utaungwa mkono na watanzania wengi.

Anzisha chama kiwe mbadala wa Chadema ambayo imelala chari kifo cha mende.
Hamna haja ya kuhangaika, si mpeni chama kimojawapo kati ya vile vyenu ambavyo wenyeviti wao weshajichokea; TLP au UDP
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom