Korea Kusini yaikopesha Tanzania Sh. bilioni 103!
13th October 2011
B-pepe
Chapa
Maoni
Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo
Korea Kusini imeipatia Tanzania mkopo wa Sh. bilioni 103.6 kusaidia upanuzi wa vituo vinne vya umeme na vifaa tiba.
Mkopo huo umetolewa na Benki ya Exim Korea, kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Uchumi (EDCF).
Hafla ya kutia saini ilihudhuriwa na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, wambaye aliishukuru serikali ya Korea kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali.
Waziri Mkulo alisema sehemu ya fedha hizo itatumika kupanua mradi wa umeme katika mikoa ya Iringa, Shinyanga, Dodoma na Singida na uwekaji wa vifaa tiba utafanyika katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili (MUHAS) kampasi mpya ya Mlonganzila, Kwembe.
Alieleza kuwa Sh.bilioni 59.9 zitatumika kwa ajili ya kupanua mradi wa umeme Iringa-Shinyanga na kwa ajili ya mkondo wa kusafirisha umeme wa KV 400. Mradi huo utasaidia maeneo ya wa kusini na mashariki ya Tanzania.
Aidha, alisema mkopo wa pili ni wa Sh. bilioni 44.1 utatumika katika maendeleo ya MUHAS ambao utahusisha usambazaji wa vifaa vya tiba na uwekaji wa vifaa hivyo.
CHANZO: NIPASHE
OMBI: Kwa kasi hii ya ukopaji wa serikali kuna umuhimu wa kuanzisha thread ya kuodhoresha madeni ya nchi ya kujiuliza kama kweli yanaweza kuja kulipika miaka ijayo? Leo nimesikia mikopo mitatu mikubwa imenistua na kujiuliza je mikopo hiyo italipika kweli. Hebu nianze kuodhoresha Kwanza huu wa shilingi Billioni 103 kutoka Korea Kusini (Nipashe leo asubuhi). Pili mkopo wa $1 billioni ambao ni sawa na Trillioni 1.73 umetajwa na rais leo kupanua gas pipeline kule Mtwara na Lindi. Pia kuna mkopo wa milioni 407 (Mwananchi la leo mkopo wa World Bank). Zote ni jumla ya Trilioni 1.84. Tuwe waangalifu kinachotokea Greece sio ajabu kitakumba na sie kama hatujakua waangalifu na kasi hii ya kukopa.