Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,182
- 883
Kwanza naomba kutamka mapema kuwa haya ni mawazo yangu binafsi. Yanaweza kuwa sio sahihi lakini bado yanabaki kuwa mawazo, na something is better than nothing.Kama ni ya kipuuzi,achana nayo.Kama ni ya muhimu,fanyia kazi tafadhali.
Nimefanya utafiti japo (sio wa kutosha sana) kuhusu nafasi ya raia walio nje ya nchi kuchangia mabadiliko katika nchi yao ya asili. Miongoni mwa tabia zinazoathiri mchango wa raia hao ni ukweli kwamba japo kuwa nje ya nchi, kwa kiasi flani, kunasaidia kuongezeka kwa awareness ya uraia (hasa kutokana na taratibu mbalimbali huko ugenini ambapo from time to time tunajikuta tukijaza forms moja au nyingine zinazotutaka kutaja uraia wetu, hence kutukumbusha tunatoka wapi originally) kikwazo kikubwa ni matarajio ya wale walio karibu nasi (familia, ndugu, jamaa na marafiki) huko nyumbani hasa kwenye suala la misaada. Kwa kifupi, tunajikuta tukikabiliwa na majukumu makubwa (real or imagined) ya kibinafsi (in the sense ya hao walio karibu nasi) kuliko ya umma au jamii nzima.
However,ukaribu huo na walio karibu nasi unaweza pia kuwa manufaa kwa maana ya kwamba msemaji mkuu wa umma ni watawala wetu ambao kama tunavyofahamu wanapenda kutoa takwimu za kupendeza hata pale zinapokinzana na hali halisi.Na hilo ni miongoni mwa matatizo ya jumuiya au umoja: kuzungumzia ujumla badala ya upekee.Wawakilishi au viongozi wa umoja hulazimika kujumuisha yale yanayowahusu wanaounda jumuiya au kundi husika, na hivyo kuficha (kwa kukusudia au kwa ulazima) yanayomgusa mtu moja mmoja au vikundi vidogo vinavyounda umoja huo.
Ukaribu huo unaweza kutusaidia kufahamu yanayofichika kwenye taarifa zinazohusu umoja (kwa maana ya jamii nzima) kwa sababu umoja huo hutokana na wingi au ujumla wa aina hii: mtu mmoja mmoja---kikundi---vikundi---umoja.Kwa lugha nyepesi: mimi/wewe/yeye---familia/marafiki/ndugu/jamaa---ukoo/kijiwe,nk--- kabila,nk---taifa.Ni dhahiri basi ukaribu wetu na hao walio karibu yetu unatuwezesha kabisa kufahamu yanayowasibu kwa ujumla wao.Kinachokosekana,so far, ni networking katika hiyo unit ya kwanza, yaani mimi,wewe,yeye,nk.Laiti ingekuwa hivi: taifa---vikundi---kikundi---mimi,wewe,yeye---SISI (kwa maana ya muungano wa unit ya kwanza) then tunaweza kabisa kupata kitu kama SISI---TAIFA au TAIFA---SISI.
Naamini logic yangu imeeleweka.Hata hivyo, logic hiyo ina-neglect factors flaniflani kwa mfano watu wasio na connection na nyumbani (kwa maamuzi yao binafsi au mazingira waliyomo),wale ambao majukumu au utashi wao hauwaruhusu kuwa na mtazamo tofauti na watawala (yaani wao---taifa,au vice versa),nk.
Sasa tuelekeze macho yetu kwenye unit ya kwanza, yaani mimi, wewe, yeye na hatimaye umoja wetu (sisi, ninyi, wao).Bila kupoteza muda, naomba kuwasilisha ombi kwenu tuanze jitihada za kuleta mabadiliko huko nyumbani.
Natambua vikwazo vilivyo mbele yetu, lakini kila safari ina vikwazo vyake.Kinachohitajika ni determination na resilience.Tukiamini katika mission yetu, then tunaweza kufanikiwa. Safari ya kuelekea kwenye mafanikio inaanza na imani kwamba dhumuni la safari hiyo ni jema, tunajua tunakoelekea na tuna dhamira thabiti ya kufika huko.
Mkakati ninaopendekeza hapa ni huu: anza kuchunguza namna gani unaweza kuwasiliana na mamlaka husika hapo ulipo. Kwa vile mie niko UK, mfano wa mamlaka husika unaweza kuwa Mbunge, vikundi vya kijamii vinavyohusika na masuala ya ustawi wa jamii (hususan kwa nchi za Afrika, au Tanzania in specific) na hata vyombo vya habari. Kwa wenzetu wa Marekani, nadhani kuna watu kama maseneta, members of the house of representantives, advocacy groups, nk.
Baada ya kubaini ni watu au taasisi gani zinazoweza kusikiliza ajenda yako, then anza mawasiliano nao.Waeleze kwamba tunahitaji msaada wao.Kwamba, serikali zao na taasisi zao nyingine ni miongoni mwa wafadhili wetu.Tunawashukuru kwa hilo. Hata hivyo, tunawaomba wafahamu our version of hali halisi ya Tanzania hivi sasa.
Kuongeza uzito (na pengine kuwa-convince kwamba cause yetu inaweza kuwa na manufaa kwao pia) wajulishe kwamba tunafahamu kuwa mingi ya misaada wanayotupatia inatokana na fedha za walipa kodi wao. Kwamba wanajinyima kwa ajili yetu.Kwahiyo basi tunategemea wangependa kuona misaada hiyo ikitumika kulingana na matarajio yao.
Ufumbuzi sio wao kushinikiza kusitishwa kwa misaada. Hilo litawaumiza walalahoi wasio na hati huko nyumbani.Cha kuwaomba ni kuwabana watawala wetu.Na hapa ni muhimu kuwa very specific: kutoa mifano hai ya namna gani misaada ya wafadhili na wahisani imekuwa msingi wa kiburi cha watawala wetu (rejea kauli ya Dkt Makongoro Mahanga kwamba laiti wafadhili wangekuwa hawaridhishwi na performance ya serikali, wasingependelea kutupatia misaada).Naamini pia kuwa kuna mifano hai huko vijijini, wilayani, mikoani na taifani kwa ujumla.
Mifano mingine ni namna ufisadi unavyotafuna fedha za umma (ambazo zingeweza kupunguza kiwango cha misaada tunayohitaji kutoka kwa wafadhili), ukiukwaji wa haki za binadamu sambamba na uminywaji wa uhuru wa kujieleza, nk.
Kwa leo, nadhani haya machache yanatosha.Mwenye kuamini katika ninachoamini, tunaweza kuwasiliana japo ningependelea zaidi iwapo tungepunguza maneno na badala yake tuelekeze nguvu kwenye vitendo.

Last edited: