Ombi maalum kwa Rais wetu Magufuli, wananchi tunastahili kuheshimiwa

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,492
92,983
With all due respect tena kwa unyenyekevu mkubwa naleta ombi maalum kwa Rais wetu Mzee Magufuli wananchi tunaomba pia atuheshimu.

Mheshimiwa Rais baada ya kuapishwa kuwa Rais katiba ilimpa fursa ya kumteuwa yoyote aliyemtaka na kama mnavyojuwa post za teuzi za rais ziko nyingi mno analo eneo pana la kumteuwa amtakaye na wananchi tunaheshimu maamuzi yake.

Lakini hii tabia mpya aliyoianza kutupangia wananchi tuchaguwe vipi ni kutudharau na kuvunjia heshima na kuona kana kwamba wote hatujakwenda shule.

Nchi hii tangu Uhuru inaongozwa na CCM, na isitoshe uchaguzi wa mwaka 2000 CCM ilizoa viti vyote vya udiwani na ubunge mkoani Dar Es Salaam kasoro jimbo la Kigamboni tu ndio CUF walishinda jimbo lile na mbunge akawa Frank Magoba hatukuwahi kuziona hizi connection tunazoaminishwa leo za mafiga matatu.

Kuna mengi ya kuongea kuhusu tabia hii mbaya ya kutuona kama vile hatujui serikali zinaendeshwaje lakini itoshe tu kusema tunaombatuachie hii ni nafasi yetu ya kutowa ajira kwa tunayemtaka sisi na si anayemtaka yeye.

Kama hajui mfumo wa upigaji kura mtu anaweza akamnyima yeye kura lakini akampigia diwani wa ccm kwa sababu wako wote mtaani na anaujuwa uwezo wake.

Yeye afanye kampeni zake aombe kura swala la maamuzi tutaamuwa sisi hatuwezi kupangiwa, na nchi hii kamwe haiwezi kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom