Ombi maalum kwa Ndugu Masako wa ITV

kamikaze

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
422
610
Kutokana na matatizo ya umeme yanayoikumba nchi yetu, jana sikuweza kuangalia kipindi chako cha kipima joto ambacho nimesikia mlikuwa mkizungumzia kuhusu Tanesco na tatizo la umeme na Mmoja wa wachangiaji wa mada hiyo alikuwa ndugu Mkinga, Huyu ndugu huwa napenda sana hoja zake anapochangia katika mada mbalimbali, kwa hiyo kwa kuwa ITV haina utaratibu wa kurudia vipindi vya kipima joto nakuomba ukiupload/kiweke kipindi cha jana 3/6/2011 kwenye Youtube ili nasi ambao hatukukiona tuweze kudownload na kukiangalia.
Aksante.
 
Ni likiangalia!
Nilipenda sana hoja za mzee uliemsifia ....japo mzee masako alikua anambania mara kwa mara.
Haya subiri akuwekee kwenye utube!.
 
Ni likiangalia!
Nilipenda sana hoja za mzee uliemsifia ....japo mzee masako alikua anambania mara kwa mara.
Haya subiri akuwekee kwenye utube!.

yule mzee alikua anaongea ukweli sana,, masako lazima angembana, lasi hivyo angeweza hata kufukuzwa kazi,,,,,
kwakweli mzee anatisha yule,, hakuna mfano
 
hata akiongea ukweli, inchi yetu twaijua wenyewe. Hizo hoja zinaishia pale pale kwenye tv. Mana kama kweli zingekua zinafanyiwa kazi nadhani tungekua mbali kimaendeleo coz mengi yamezungumzwa. Anyway, endeleeni kufuatilia maana hakuna mnachopoteza.
 
Back
Top Bottom