Elections 2010 Ombi maalum kwa Jaji Lewis Makame - tunataka amani Tanzania.

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Bado nakumbuka yaliyotokea kwa jirani zetu Kenya ambako tamko la aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Bwana Samuel Kiviutu, lilivyoweza kuigeuza nchi jirani, Kenya, kuwa uwanja wa mapambano na vita. Matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2008 yaliyotangazwa na kumpa ushindi incumbent, Raisi Mwai Kibaki, yalisababisha umwagaji mkubwa wa damu ambao karibu usambaratishe nchi hiyo. Ni juhudi tu za ziada za mataifa na wadau mbali mbali zilizowezesha hali angalau ya amani kurejeshwa tena na kuzuia mauaji zaidi.

Hali kama hii pia tuliishuhudia Tanzania Visiwani ambapo kwa mara ya kwanza kabisa Watanzania walijikuta wakiwa wakimbizi nchi za jirani kama Kenya na kwingineko. Kama ilivyotokea huko Kenya, ni matokeo ya Uchaguzi Mkuu Visiwani yaliyotangazwa na kumpa ushindi incumbent, Salmin Amour, huku ushindi wake ukiwa umegubikwa na mashaka kibao. Tulishuhudia wananchi kadhaa wakiuawa na wana usalama ambao kimsingi walitakiwa kuwalinda lakini Raisi Benjamin Mkapa akaamua vinginevyo.

Mheshimiwa Jaji Lewis Makame, kosa si kosa ila kurudia kosa na ninakuomba usije ukawa Sameli Kiviutu wetu wa Tanzania. Dalili zote zaonyesha kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa tofauti kidogo na wananchi wameamua kuwa hawako tayari kuendelea kuwabeba viongozi wasio na uwezo. Nakuomba uweke historia kwa mara ya kwanza kuendesha uchaguzi wa haki kuanzia matayarisho ya awali hadi siku matokeo yanatangazwa. Kama ni kujifunza naamini umejifunza na, for heavens sake, Kofi Anan hatakiwi hapa - tafadhali usiliangushe taifa, ni ombi tu.
 
Hakuna mtu yeyote anayeweza kuzuia nguvu za asili. Yes, ni vema kuweka tahadhari mapema lakini kumbuka binadamu sio kondoo.
 
Mkuu ni wazo zuri sana, lakini nachelea kukuambia kwa stori kama hizi badala ya kufanyiwa kazi kulinda umoja wetu basi watakimbilia kusema ni uchochezi na itapelekea uvunjifu wa amani.

Ukweli ni kwamba kila mtu anaomba nchi yetu isifike huko ila wasiwasi wangu ni kuwa ndiko tunakopelekwa. Ukiisha ona wananchi wanakata tamaa basi ujue ni dalili mbaya sana kwa nchi. Baba wa Taifa alisema katika sherehe za CCM 5/2/1988 pale uwanja wa CCM Ali Hassan Mwinyi Tabora, nakumbuka nilikuwa Tabora kikazi kipindi hicho; kuwa hakuna kitu kibaya kama wananchi wakikata tamaa, maana wao hawataona tofauti kati ya kuishi na kutoishi na hapo ndipo penye hatari yenyewe. Ila wametia pamba wanasubiri litokee ndiyo waunde tume ya kuangalia chanzo.
 
Bandika namba ya Jaji Lewis hapa, tuanze kumpa petition ya Uchaguzi Huru na wa Haki
 
Mwenye email au No za simu yake. Mag3 huewezi kuorodhesha halafu tukifika namba fulani tuangalie namna ya kuwalikisha au tuombe gazeti mojawapo lirushe?
 
Wazo zuri mi nafkiri tumuandikie barua kabisa...! Jaji Lewis Makame

Mawazomatatu, on the contrary, naona aandikiwe barua kujiuzulu. Nikiangalia umri wake niaona kiakili amechoka. Nikaangalia sheria inayounda tume ya uchaguzi, kifungu cha nne kinatamka bayana:

" (1) The Commission shall, subject to the Constitution and to this Act, consist of the following members–
(a) a Chairman who shall be a Judge of the High Court or of the Court of Appeal of Tanzania;

Mwenyekiti ya tume ya uchaguzi sio Jaji wa mahakama kuu wala wa mahakama ya rufaa, ila aliwahi kuwa Jaji wa mahakama ya Rufaa na akastaafu hivyo hana sifa za kukalia kiti hicho, Kama bunge lingetaka wastaafu wawe kwenye nafasi hiyo lingetafuta maneno ya kucover hiyo situation, kwa busara yake bunge liliona kuwa mwenyekiti lazima awe jaji na sio jaji mstaafu.

Hivyo basi kama anaandikiwa barua ni kumueleza kuwa ajiuzulu kwa sababu hana sifa.

We always take things for granted, watu wa ajabu sana sisi.
 
Bado nakumbuka yaliyotokea kwa jirani zetu Kenya ambako tamko la aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Bwana Samuel Kiviutu, lilivyoweza kuigeuza nchi jirani, Kenya, kuwa uwanja wa mapambano na vita. Matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2008 yaliyotangazwa na kumpa ushindi incumbent, Raisi Mwai Kibaki, yalisababisha umwagaji mkubwa wa damu ambao karibu usambaratishe nchi hiyo. Ni juhudi tu za ziada za mataifa na wadau mbali mbali zilizowezesha hali angalau ya amani kurejeshwa tena na kuzuia mauaji zaidi.

Hali kama hii pia tuliishuhudia Tanzania Visiwani ambapo kwa mara ya kwanza kabisa Watanzania walijikuta wakiwa wakimbizi nchi za jirani kama Kenya na kwingineko. Kama ilivyotokea huko Kenya, ni matokeo ya Uchaguzi Mkuu Visiwani yaliyotangazwa na kumpa ushindi incumbent, Salmin Amour, huku ushindi wake ukiwa umegubikwa na mashaka kibao. Tulishuhudia wananchi kadhaa wakiuawa na wana usalama ambao kimsingi walitakiwa kuwalinda lakini Raisi Benjamin Mkapa akaamua vinginevyo.

Mheshimiwa Jaji Lewis Makame, kosa si kosa ila kurudia kosa na ninakuomba usije ukawa Sameli Kiviutu wetu wa Tanzania. Dalili zote zaonyesha kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa tofauti kidogo na wananchi wameamua kuwa hawako tayari kuendelea kuwabeba viongozi wasio na uwezo. Nakuomba uweke historia kwa mara ya kwanza kuendesha uchaguzi wa haki kuanzia matayarisho ya awali hadi siku matokeo yanatangazwa. Kama ni kujifunza naamini umejifunza na, for heavens sake, Kofi Anan hatakiwi hapa - tafadhali usiliangushe taifa, ni ombi tu.
Mkuu kumbe ulianza kumkomalia kitambo cheki HAPA
 
Back
Top Bottom