Ombi langu Maalum kwa Mhe Rais:Naomba uwaachie Rais wa DARUSO na Katibu wa TGNP | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombi langu Maalum kwa Mhe Rais:Naomba uwaachie Rais wa DARUSO na Katibu wa TGNP

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gembe, Jan 22, 2009.

 1. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mheshimiwa Rais ,

  Naomba nikupe pole na jinsi khali ya uchumi inavyoendelea hapa nchini,Naona jitihada zako mpya za kuweza kufufua uchumi wa nchi hii zikianza kwa nguvu mpya na kasi mpya tena.Mikutano yako na viongozi wa BOT,Wizara ya Fedha itasaidia sana japo kuwapa watanzania maisha bora waliyoyasubiri toka 2005.

  Mhe. Rais,
  Najua tumekuwa tukikushauri kwa muda mrefu sana kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu na tumekusaidia sana katika kuongoza nchini yetu ya Tanzania,tumeweza kuvumbua uozo wa ACTL,Ufisadi katika sehemu mbali mbali,tumekusaidia mambo magumu ambayo kwa khali ya kibinadamu na kirafiki haikuwa rais kufanyika(rejea kashfa ya RDC).

  Mhe Rais najua kuna mambo mengine tumekukera sana kwa kuwa haukutaka tuyazungumze hapa .Yawezekana ulifikia hatua ya kuchukia wachangiaji hapa kama alivyofanya mwandishi aliyemmjibu Mzee Mwanakijiji katika akala ya ndege inayopaa ya mwaka 2007.Rais wetu mpendwa tulifanya hivyo ajili ya maslahi ya nchi yetu na kama kuna sehemu tulikosea tunaomba utusamehe

  Mhe Rais,Leo nina ombi moja tu naombakwako,Ombi lililo maalum.Naomba uagize Jeshi la Polisi liwaachie hawa vijana wawili,Rais wa DARUSO Mhe. MAchibya na steven Owawa ambaye ni katibu wa TGNP,inawezekana wana kosa ila hawana Hatia,Nakuomba sana utoe maelekezo sasa.Nimesoma habari ya kukamtwa kwao kwa masikitiko makubwa sana sababu hii inajenga picha kwamba watanzania walio wadogo hawawezi kuzungumza lile wanaloliamini ni sahihi.

  Mhe Rais,
  umekekuwa ukizungumzia demokrasia kwa muda mrefu sasa,Tena inayotoa uhuru kwa watu kuchagu aviongozi waaadilifu .Hawa vijana ni waadilifu sababu wanatetea jamii nzima ya wanafunzi wa vyuo vikuu.

  Mhe Mwenyekiti wangu,
  Nakuomba sana huku nikikusihi sana uwaachie sababu hawa vijana wanapigania yale yaliyo kweli kwa sasa na wanafanya hivyo kwa ajili ya watanzania masikini(walio wengi).ambao wanategemea msaada wa serikali yao katika maendeleo.

  Kwa wanafunzi wa vyuo,Naomba muwe watulivu wakati serikali ikiangalia njia ya kuweza kutatua jambo hili,na nina uhakika Mhe. Rais ataingilia kati jambo hili kwa kuwa linagusa maisha ya watanzania walio wengi.

  Mhe. Naomba unisaide japoo hili tu.

  Mungu akubariki sana na wasaidie Vijana hawa
   
 2. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kuna wanaharakati LHRC wamajitolea kuwa tetemahakani... haki ya hawa watoto ya kusoma inapotea hivihivi!!!!! linusuru taifa kani hili jambo lina madhara makubwa
  [media]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=3361&stc=1&d=1232611506[/media]
   

  Attached Files:

 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Naamini Mh Rais atasilikiliza sauti hizi za wanafunzi.
   
 4. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mh Mkuu SMU, ATA-sikiliza? Alikuwa wapi siku zote? Yaani wamesota rumande ipindi chote hiki? Pulll-ease!!
  Gembe ndugu yangu, you have done a very noble thing but.... Don't waste your energy pleading with this president! Hana chembe cha huruma! Labda umwambie atauza sura!
  Sorry, but I am tired of people treating him with respect when he disrespects all of us!
   
 5. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,276
  Likes Received: 4,260
  Trophy Points: 280
  Gembe nakupongeza sana kumuomba rais aingilie kati hili suala lakini kila mara naona unamuomba kuhusu mambo mbalimbali hivi kuna jambo hata moja kati ya uliyomuomba amewahi kukusikiliza?
   
 6. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Sahihisho ni kuwa Owawa Stephen sio mwenyekiti wa TGNP bali ni mwenyekiti wa TSNP AMBAYO NI TANZANIA STUDENTS NETWORKING PROGRAMME, Gembe sahihisha mkuu kwani TGNP ni kwa ajili ya wanawake.

  Naunga mkono hoja ya kuwaachia kwani kuandamana na ama kushika mabango yaye ya kusifu ama ya kukosoa ni haki ya kila mmoja wetu, na pindi wanaposifu wapigiwe makofi na wanapokosoa basi wasikilizwe.
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Rais awasaidie hawa vijana kwani 2010 tayari?? Wasomi wa Tz wamejichimbia kaburi lao wenyewe. Si hapo UDSM ambapo 2005 palikuwa kitovu cha kampeni za JK mpaka wengine wakaenda Diamond kuchukua kadi? Si ni hapo UDSM ambapo 2005 kila mtu alipewa mkopo wa 100% na kulipia hata watu wa shahada za uzamili? Sasa kama hela yote ilitumika 2005 walitegemea nyingine itatoka wapi kabla ya 2010?

  Sioni mtu wa kuwaonea huruma labda wazazi wao na watu wenye akili inayofanya kazi kama hao wanasheria wa haki za binadamu. Hata hivyo wasiwe na wasi wasi 2010 watakumbukwa tu!
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Serikali yetu maamuzi yake mengi kuhusu wanafunzi ni ya kuwakomoa ili kuwaharibia future yao. Wanachotaka wao ni kuhakikisha hao vijana hawakanyagi chuo chochote nchini ili kupata elimu ya juu na maisha ya dunia ya leo kama tunavyoyajua bila elimu ya juu basi huwezi kufanya chochote cha kusukuma mbele maendeleo yako na yale ya nchi. Miaka michache ijayo wataanza kulalamika hatuna wataalamu wa fani hii na ile na hivyo kuagiza TXs na kuwalipa mabilioni.

  JK maamuzi kuhusu wanafunzi yanaikomoa nchi maana hawa vijana wengi wataishia kuwa wezi, majambazi, wauza unga na machangudoa na kuzidi kuiweka jamii ya Watanzania katika tishio kubwa siku za usoni.

  Kaeni nao meza moja na msikilize matatizo yao na hatimaye kuwapa mikopo ya 100% ili waweze kumudu gharama zao za kila siku kama wanafunzi wa ulimu
  ya juu.
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  w a a c h i l i w e - bila - m a s h a r t i
   
 10. L

  Labibah Member

  #10
  Jan 22, 2009
  Joined: Jan 20, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanini ufanyike mchezo mchafu mimi naweza kuita hicho kitu aliofanya huyo kikwete kuwa ni mchezo mchafu sana maana kaangalia bila ya kuchukua hatua yoyote.
   
 11. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mh. JK kweli tunaomba uwaachie hawa vijana. Mungu akutie nguvu ya kuamua hilo hata kama hukupenda kufanya hivyo. Nasema hivi kwasababu hakuna sababu ya msingi kuwatia ndani. Magereza yetu yanatakiwa kuingia watu ambao ni genuine. Makosa ya kuokoteza ni aibu kwa taifa.

  Mungu Ibariki Tanzania,
  Mungu Ibariki Afrika.
   
 12. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Gembe hongera kwa kusemea wanafunzi. Wanasema wanachoamini,wanakamatea.Naamini walikamatwa si kwa sababu walikosea,ila kwa sababu wana ushawishi mkubwa kwa wanafunzi hivyo walifanya hivyo ili kupunguza uwezekano wa wanafunzi kugoma.Hata hivyo wanapofikishwa mahakamani ni tatizo na kwa hili serikali imeingia hasara kwa kufungu kesi ambazo hazina ushahidi na hatimae kudaiwa fidia kubwa.Naungana na wewe ,si kumwomba aagize waachiliwe huru tuu bali aangalie matatizo ya elimu hasa ya juu kwa ujumla.
   
 13. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Bubu tuzidishe maombi labda atasikia.Mungu amtie nguvu kweli.
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  L,

  Kwani mchezo mchafu ni mmoja tu ndugu yangu? Mbona ipo nyingi?

  Hukusikia jana kwenye vyombo vya habari kuwa CCM imeuandikia uongozi wa chuo (UDSM) kuwa wanafunzi 40 (ambao wanatuhumiwa kuongoza mgomo) ni wanachama wa CHADEMA kwa hiyo wafukuzwe bila kuonewa huruma?

  Ingawa huu ni wakati wa kuwaonea huruma lakini tuwambie ukweli kuwa makosa ni yao. Wakati sisi tuko chuo miaka 90, tena wakati mfumo wa vyama vingi unakuja tulikataa kata kata kuingizwa kwenye mitego ya vyama. Sasa wanafunzi wanashindana kuvaa jezi za KIJANI Vs Bluu n.k. Nadhani sasa wanafunzi wakome na warudie kwenye mstari kama ambavyo wanategemewa kufanya mambo yao. Waachane na vyama na wafanye kazi ya kujitetea wao wenyewe na kutetea maovu ambayo umma wa Watanzania unatendewa. Vinginevyo yatawapata makubwa zaidi ya haya na hawatapata mtu wa kuwaonea huruma.
   
 15. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #15
  Jan 22, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Wakuu,

  Nimesoma hoja za mkuu Gembe kwa makini sana,amejenga hoja nzuri sana.Lakini naomba kutofautiana nae kidogo.

  Kama tunampa Rais mamlaka ya kuamua au kuingilia masuala ya mahakama basi tutakua tunatoa fursa pana zaidi pasipo kujua kwa mhimili wa utawala na watawala kuingilia mhimili mwingine wa mahakama.Sisi wananchi tutakua tunawazoesha watawala wetu kuingilia uhuru wa mahakama na madhara yake ni makubwa zaidi na sisi wananchi ndio tutakaoathirika.


  Ninatambua uwezo wa Rais kusamehe wafungwa tena ambao wameshahukumiwa,lakini hilo ni tofauti.

  Siungi mkono hawa wanafunzi waliowekwa under detention kuonewa.Kwanini kila kitu tunamuomba Rais kuingilia kati? Tunamtukuza na kumpa uwezo asiokuwa nao na kusalimisha haki zetu zote kwake pamoja na kumpa mamlaka tukufu ya kuingilia mfumo wa kimahakama


  SASA, lifanywe jambo lingine lolote kuishinikiza wizara ya elimu ya juu,wizara ya mambo ya ndani,wizara ya katiba na sheria na au Bunge liingilie kati hilo suala na kufikia azimio la siku moja juu ya mustakabali wa hao wanafunzi.

  Nawasilisha!
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Definitely, but not before 2010.
   
 17. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #17
  Jan 22, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  kama rais haingili masuala ya makama,mbona Obama amezuia Kesi zote za\wafungwa Wa Guantanamo Bay?
   
 18. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Unaweza kutusaidia kifungu cha Katiba (ya Marekani) alichotumia Rais Obama? ... siamini kama alikurupuka tu ... na hiyo Guantanamo Bay iliundwaje na kwa mamlaka ya nani?
   
 19. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #19
  Jan 22, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ben,

  Mtu anaingilia jambo kama linamgusa au anahisi uchungu kwa kile binadamu wenzake wanachotendewa! Ila kwa wanasiasa walio wengi na hasa hawa hapa kwetu wanaoangalia kura tu, wanaingilia endapo hali hiyo inahatarisha ushindi wake au wa chama chake. Sasa Wakulu wanajua kuwa 2010 watashinda tu, kwa nini wahangaike na hawa viongozi wa wanafunzi na wanafunzi kwa ujumla. Ukizingatia kuwa kama wakitumia muda wao vizuri (kukusanya vijisenti), 2010 watatumia ndoana yenye chambo safi (Tshs za kutosha) na kura watapata hadi za kumwaga. Kama lingekuwa suala la Rais kuingilia basi vyuo vinsingefungwa. Hizi dua ambazo baadhi ya watu wanaomba ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa! Please expect nothing and don't be disappointed!
   
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
   
Loading...