Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,179
- 7,330
Barabara na mitaa iwekwe vibao kuonyesha majina. Miji yote mikubwa hili suala hupewa kipaumbele sana.
Kwa bahati mbaya Dar jambo hili ni kama limepuuzwa. Barabara na mitaa mingi haina vibao vya kuonyesha majina yake na pale vilipo, vimechakaa au kipo kimoja au vichache sana
Kwa jiji kubwa na linalokua kwa kasi kama Dar, addressing na movement vinakuwa tatizo sana pala barabara zinapokosa majina, sio kwa wageni tu, bali hata kwa wenyeji.
Tatizo linakuwa kubwa zaidi pale kunapokuwa na tatizo la dharura na kukaitwa msaada mfano wa uokoaji nk, inakuwa ngumu sana eneo fulani kufikiwa kwa muda kwani wanaoenda mara nyingi hupotea na kulazimika kuzungukazunguka
Kwa miaka ya karibuni movement kwenye miji inasaidiwa sana na Google map directions. Sasa huwa kwa Dar application ya hii kitu inakuwa ngumu sana kutokana na barabara kutotambulishwa
Niliwahi kumtumia meya wa Kinondoni hili jambo, sina uhakika amefikia wapi...