Ombi langu kwako Rais na Mwenyekiti CCM Taifa

MwalimuMkuu

Member
Oct 10, 2012
59
12
Mh Rais na Mwenyekiti CCM Taifa.

Awali ya yote nakupa pole na pongezi nyingi kwa kazi unazozifanya katika ujenzi wa Taifa letu. Ni ukweli ulio wazi kuwa jitihada zako zinaonekana ndani na Nje ya nchi. Tunakupenda sana na tunashauku kufika Tanzania uipendayo.

Mh Rais na Mwenyekiti Chama Taifa wiki iliyopita ya tarehe 9/10-15/10 kulikuwepo na masuala makubwa yaliyoibuka ndani ya chama kama ifuatavyo;

ü Kauli ya Ndg Polepole kuwa wagombea Ubunge na Udiwani katika uchaguzi wa 2020 ccm itapitisha wale wanaoishi katika majimbo yao tu.

ü Kauli iliyotolewa na Ndg Mangula kuwa watumishi wa Umma hawatakiwa katika uongozi na ujumbe wa vikao vya chama.


Mh Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa kwanza kuhusu taarifa ya Pole Pole imeshatolewa ufafanuzi na Ndg Pereira Silama hivyo sina haja ya kuendeleza mjadala katika hili.


Kuhusu suala La Mzee wetu Mangula;

Katika hili Mh Mwenyekiti naomba utafkari upya na kuangalia historia ya Chama Tangu enzi za waasisi wa Taifa letu. Hisitoria inaonyesha kwamba CCM ni chama cha wafanyakazi na wakulima na ndiyo msingi wake mkuu.

Mh Rais pamoja na uwepo wa vyama vyingi lakini ccm bado inahitaji kuwa na wafanyakazi wa sekta ya Umma.

Kweli kuwa baada mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi yatapelekea mabadiliko kadhaa katika sekta ya Umma lakini Mh Rais nakuomba sana piga marufuku watumishi wa umma kushika na nafasi za uongozi katika chama kama vile, Mwenyekiti na katibu katika ngazi yeyote ile ya chama.

Lakini nafasi za ujumbe wa vikao mbalimbali iwe mkutano mkuu, Halmashauri kuu, Kamati za siasa ni muhimu kuwaruhusu wale wanaopenda kuonyesha nia na kupendwa na wanachama katika maeneo yao waombe nafasi hizo na wakichaguliwa waruhusu wahudumu sababu vikao zenyewe zinakaa mara chache sana kwa mwaka hivyo hakutakuwa na athari yeyote.

Umuhimu wa kuruhusu watumishi wawe wajumbe wa vikao vya chama

1. Kuenzi Historia ya CCM iliyotambua Tangu awali nafasi ya wafanyakazi

2. Vikao vya CCM kama vile Halmashauri kuu za Mikao na Wilaya zinajadili kwa kiwango kikubwa utekelezaji wa Ilani ya Chama hivyo kwa lugha nyingine inahitaji sehemu ya Utaalam au ushauri wa kitaalam na sababu za kiuhalasia zinazokwamisha utekeezaji wa ilani, na kwa kuwa watumishi wa umma ni wataalam wa kada mbalimbali watakuwa na mchango mkubwa sana katika ukelezaji wa ilani ya CCM na hatimae maendeleo ya Nchi.

3. Kutokuwa ondoa watumishi katika chama. Mh Rais kijana alimaliza shahada ya sheria akajiriwa na katika Sekta binafsi anaweza kuwa na uhuru wa kujiunga na CCM lakini kijana huyo huyo akiajiriwa na Ofisi ya UMMA hatakama ana mapenzi mema kwa ccm na Nchi yake ana zuiliwa kujiunga nacho. Mh Rais hii itakuwa si ile ccm ya Mwalimu iliyoamini katika wafanyakazi na Wakulima. Maana yake sasa ccm itakuwa ya wafanya biashara na wakulima.

4. Mh Rais inawezekana kabisa kuwa watumishi wa umma wamekuwa na mapungufu makubwa sana katika utendaji wao, lakini hoja si kuwatenga wale wachache wenye nia njema na chama ni kuwakaribsiha na kuwaimarisha upya.

5. Haki ya mwanachama wa chama chochote kile ni kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Sasa kama mwalimu ya sekondari Tandahimba anataka kujiunga na CCM kwanini anyimwe haki ya kikatiba ya chama chake.


Mh Rais uyatafakari haya kabla ya vikao vikuu vya chama
 
Sheria inaseamaje? Ni hatari kuchanganya mambo haya, Mimi si lazima niwe mjumbe wa mkutano wa chama ndio nionekane napenda sana chama, mtaani kwangu niweza nikakisaidia chama bila tatizo kama ushauri, ujenzi wa chama etc. Walio nje ya utumishi hawaoni adhari, Rais acha kuwasikiliza hayo!
 
Back
Top Bottom