Ombi langu kwa DStv wekeni na habari za URUSI kupitia TV yao ya kiingereza ya RT yaani Russia Today

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,147
33,302
Kuna tatizo lolote kati ya RT na DSTV?

Kama hakuna tatizo naomba mimi Kama mteja mtuwekee na vipindi kutoka Urusi, sisi wengine ni wapenzi wa habari za kimataifa, pia hupenda kufanya ulinganifu wa taarifa.

Kwa bahati nzuri DStv mnarusha habari za dunia kupitia CNN,BBC,DW,FRANCE, na TV nyingine za MATAIFA mengine na hata nyigi tu za China Kama CGTN,TV za India na nchi nyingine kubwa lakini RT ya URUSI hamrushi.

Kama hamna tatizo Mimi mteja wenu kwa niaba ya wengine naomba mtirushie na taarifa za dunia kupitia RT ya URUSI.

Natumai ombi langu litakubaliwa.
 
Mi nawashangaa sana, sisi Tanzania na Africa mashariki, mnatuletea habari za DW kwa kijerumani na Kifaransa au kiitaliano kwa nini msiwapelekee wanaoongea lugha hizo.

Mimi mkiweka hizo kwa kiingereza mkaongeza na NHK ya kijapan kwenye kifurushi cha bomba, sitawahama na nitalipia kwa wakati. Mnatakiwa mjiongeze msipigwe bao na Azam wamejaza michezo na matamthiliya ya kiswahili kwa ajili ya wanawake.

Dstv mko juu sana, wekeni channel za kiingereza tutawapenda zaidi. Sio mMnatuchanganyia na kijerumani, kifaransa, kiitaliano , kirusi nk. Hizo ziwekeni kwenye vifurushi vinavyofanana huko.

Mfano wa rwanda au burundi na congo wapeni za vifurushi vya lugha zao, kifurushi chenyewe kinaitwa bomba, afu unaniwekea kijerumani au kirusi, weka kwa kiingereza, ongezeni pia na VOA ya america ni nzuri sana.
 
Back
Top Bottom