Ombi la Soft Copy ya Katiba ya JMT

Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
682
323
Ndugu wadau,
mimi ni miongoni mwa Wabongo wengi tu ambao hatujawahi kuioma katiba ya JMT. Ingawa naunga mkono hitaji la Katiba mpya na nina sababu za wazi zinazonisukuma kuunga mkono bila kufuata mkumbo wala kushinikizwa
1. Nakerwa na Bunge kuitwa washauri wa serikali na rubber stamp ya matakwa ya wakubwa wa nchi, mfano ni saga la Richmond maamizio ya Bunge hayana nguvu yanatekelezwa au kutotekelezwa kulingana na Serikali inavyojisikia (Hii inanikera maana naona hao wabunge wanakula mlungula wetu bure hawana meno)
2. Nguvu ya Mamlaka ya rais - Haihitaji kusoma katiba ili kujua rais ana nguvu kubwa kiasi gani Bongo ya kimadaraka - Anateua wakuu wa wilaya, mikoa, mabalozi, mawaziri, anapanga ukubwa wa baraza ajisikiavyo humpiga amtakaye na kumuinua amutakaye katika nchi ya demokrasia kama hii, ateue mabalozi na msururu mrefu mno na wote hao hawana njia isipokuwa kufanya ayatakayo vinginevyo watamwaga unga.
3. Suala la Muungano wa so called Tanganyika na Zanzibar - hapa kuna mengi mno yaliyojificha yanayotukera angalia leo Zanzibar wakiullizwa ni nchi wanakana lakini ina kila kitu kinachostahili nchi kuitwa nchi huku Tanganyika ikiwa stooni bila kujua itatoka lini na mengine mengi yaliyojificha huhko.
I name many of them but anyway kama kuna anayeweza kutuwekea katiba hapa nitamshukuru
 
Back
Top Bottom