Ombi la punguzo la tozo za umiliki wa vitalu vya uchimbaji madini ni la nani?

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,450
487
Watanzania tunakoelekea yawezekana hatupajui au tumekuwa kama watu tuliofungwa kitambaa cheusi usoni. Nasema hivyo kutokana na tabia yetu ya kulialia ambayo kamwe imekuwa haiwasilishi uhalisia wa yale tunayoyataka! Kwa nini nasema hivyo?. Kupitia vyombo vya habari nimeona baadhi ya watu wanaojiita wamiliki wa vitalu vya uchimbaji wa dhahabu huko Geita wakilalamikia Selikari kuwapandishia kodi ya Leseni za umiliki wa vitalu hivyo kutoka shilingi 150,000 hadi kufikia shilingi 800,000.

watu hao ambao hata kwa muonekano wa macho ya kawaida hawaoneshi uhalisia wa kumiliki vitalu hivyo ndiyo wamekuwa wakijiweka mbele ya hadhira kuonesha kuwa wao ni walengwa kabisa ambao wanstahili kuonewa huruma na selikari kwa mgongo wa kuinua wajasiliamali.
Leo hii kuna watu wanamiliki zaidi ya Leseni tano za uchimbaji dhahabu, iweje kama unaweza kumiliki Leseni tano na wafanyakazi zaidi ya miatano ushindwe kulipa kodi ya shilingi laki nane kwa mwaka?

Kwa hili naomba nisimame kati kuwa Selikari inatakiwa kuwa macho na ulaghai huu.
Ikumbukwe kuwa wakati wa harakati za bunge letu kutaka kupitia upya mchakato wa umiliki na marekebisho ya vitalu vya uwindaji, walijitokeza watu wengi wakilalamika kuwa viwango vinavyopendekezwa na selikari ni vikubwa mno ambavyo hawataweza kuvilipa wakati huo huo wao wakiwa wamevikodisha kwa wageni kwa gharama kubwa tena wakilipwa kwa pesa za kigeni.

Vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa hawa ndugu zangu wa migodini, wanatumiwa na wana siasa ambao ndio wamiliki wa Leseni hizo kwa maslahi yao. Selikari iliangalie hili kwa macho ya ziada kwani mafisadi wanajaribu kuvumbua mbinu mpya kila uchao kwa lengo la kuendelea kulinda maslahi yao tu.
Kaa chonjo, watch out!!
 
Hapo ni kuwanyang'anya vitalu hivyo kiintelligensia. Wanavihitaji na kuwatoa kavu kavu wameona lazima ilete tafrani!
 
Ni la wakubwa maana hakuna mdogo hata mmoja mwenye kitalu cha uwindaji, wadogo wote wanapozungumza vitalu wanamaanisha vya kuoteshea mbegu za bustanini
 
Watanzania tunakoelekea yawezekana hatupajui au tumekuwa kama watu tuliofungwa kitambaa cheusi usoni. Nasema hivyo kutokana na tabia yetu ya kulialia ambayo kamwe imekuwa haiwasilishi uhalisia wa yale tunayoyataka! Kwa nini nasema hivyo?. Kupitia vyombo vya habari nimeona baadhi ya watu wanaojiita wamiliki wa vitalu vya uchimbaji wa dhahabu huko Geita wakilalamikia Selikari kuwapandishia kodi ya Leseni za umiliki wa vitalu hivyo kutoka shilingi 150,000 hadi kufikia shilingi 800,000. watu hao ambao hata kwa muonekano wa macho ya kawaida hawaoneshi uhalisia wa kumiliki vitalu hivyo ndiyo wamekuwa wakijiweka mbele ya hadhira kuonesha kuwa wao ni walengwa kabisa ambao wanstahili kuonewa huruma na selikari kwa mgongo wa kuinua wajasiliamali. Leo hii kuna watu wanamiliki zaidi ya Leseni tano za uchimbaji dhahabu, iweje kama unaweza kumiliki Leseni tano na wafanyakazi zaidi ya miatano ushindwe kulipa kodi ya shilingi laki nane kwa mwaka? Kwa hili naomba nisimame kati kuwa Selikari inatakiwa kuwa macho na ulaghai huu. Ikumbukwe kuwa wakati wa harakati za bunge letu kutaka kupitia upya mchakato wa umiliki na marekebisho ya vitalu vya uwindaji, walijitokeza watu wengi wakilalamika kuwa viwango vinavyopendekezwa na selikari ni vikubwa mno ambavyo hawataweza kuvilipa wakati huo huo wao wakiwa wamevikodisha kwa wageni kwa gharama kubwa tena wakilipwa kwa pesa za kigeni. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa hawa ndugu zangu wa migodini, wanatumiwa na wana siasa ambao ndio wamiliki wa Leseni hizo kwa maslahi yao. Selikari iliangalie hili kwa macho ya ziada kwani mafisadi wanajaribu kuvumbua mbinu mpya kila uchao kwa lengo la kuendelea kulinda maslahi yao tu.Kaa chonjo, watch out!!

Tanzania msomi hathaminiki tunafanya mambo ilimradi tu
 
Tanzania msomi hathaminiki tunafanya mambo ilimradi tu

Autorun; Nimekupata mwanangu, ila siku ya msomi kuonekana kama yeye badala ya jina la baba au mama yake kutangulia haliko mbali. Tusubili siku ya mageuzi haipo mbali.
 
Back
Top Bottom