Ombi la nafasi ya kujitolea kufundisha shuleni

nyamalagala

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
744
673
Habari zenu enyi wana wa Mola,

Mimi ni kijana wa kitanzania ninayetarajia kuhitimu shahada yangu ya kwanza ya elimu hasa katika masomo ya historia na Kiswahili kutoka chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA-Kigamboni).

Kama kuna yeyote anamiliki shule, ni mwalimu ama anajua wapi naweza kupata nafasi ya kazi kufundisha (bila malipo) masomo tajwa hapo juu kuanzia mwezi Julai.

Naomba aniunganishe ili nikalijenge taifa. Popote pale nitapiga kazi kwa moyo wote.

Kwa ufupi mimi ni:-

Kijana wa kiume.
Miaka 25+
Mkristo.
Mwenye kuishi kulingana na hali iliyopo.
Kwa sasa niko Kigamboni katika harakati za kuhitimisha masomo yangu.
Kubwa zaidi mimi ni mtunzi na mwandishi wa kazi za kifasihi ya kiswahili ambapo licha ya kuwa na miswada mingi nimefanikiwa kuchapisha kitabu ( Riwaya) yangu ambayo sasa iko sokoni.
Kwa mwenye kuguswa na uzi huu namkaribisha. Kwa mawasiliano zaidi.

Karibu PM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom