Ombi la kupunguza sikukuu nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombi la kupunguza sikukuu nchini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Jan 3, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jan 3, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndugu umewahi kukaa na kujiuliza Mtanzania wa kawaida anayefanyakazi Serikalini na baadhi ya sekta binafsi ana pumzika siku ngapi kwa mwaka ? Umewahi kuhesabu kuna sikukuu ngapi zinazotambuliwa na serikali ambazo zinalazimisha mfanyakazi huyu akapumzike nyumbani ?

  Ukiacha sikukuu hizo Mfanyakazi huyu anakuwa na likizo ya karibu mwezi moja kila mwaka kama mkataba wake wa kazi unavyosema hapo jumlisha na siku zake za kuumwa , siku za kwenda Kwenye misiba ya ndugu jamaa na marafiki na siku zingine za sherehe za kiofisi ?

  Ukijumlisha sikukuu zote hizo pamoja na siku zingine za likizo misiba ETC unaweza kupata Mtanzania wa kawaida anakaa karibu mwezi mmoja unusu kwa mwaka bila kufanya kazi , jumlisha na masaa aliyotegea kwa kulala makazini au kuchelewa kufika huko makazini unaweza ukashangaa sana .

  Kwa hali hii naomba kutoa ombi la kupunguzwa sikukuu na siku zingine za mapumziko kwa Nchi yetu pamoja na kurekebisha sheria zingine wa kazi ili kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi
   
 2. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  wenzako tunaomba siku ziongezwe manzeeee....nchi kama india wanasherehe zinazotambuliwa na serikali nyingi naweza kusema hata zaidi ya 20 kwani kila kukicha utasikia leo ni 'holiday'....
   
 3. i

  ishuguy Member

  #3
  Jan 3, 2010
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  tatizo wafanyakazi wetu hawajitumi wakiwa kazini.. wengi hawafanyi kazi kwa kujituma, wanaweka masilahi yao binafsi mbele,shortcuts nyingi.
  bila kubadilika haina maana kupunguza sikukuu. wenzetu wahindi wanasikukuu nyingi lakini hizo siku waliko kazini wanafanya kitu cha kueleweka.
   
 4. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  naomba unithibitishie hiyo katika bold au unazungumzia india ipi?
   
 5. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  shirika la uchimbaji dhahabu la barrick wafanyakazi wanapumzika wiki tatu kila baada ya kazi ya wiki sitamfululizo!

  china sikukuu ya uhuru wanapumzika siku 9, mwaka mpya siku 3, spring festival siku kama 14 hivi! na nyinginezo

  nchi nyingi ulaya nyakati za krismass wanapumzika karibu wiki mbili! hiyo ni bali na pasaka na sikuku nyingine. sisi sikuku zote ni siku mojamoja ukiacha xmass inayojumuisha boxing day, pasaka na idd el fitry.

  sasa nani wana sikukuu nyini? kama ni fanisi duni, mimi siamini kuwa sikukuu zinachangia. mwanadamu si mtumwa. mie ningependa zionezwe ili wafanyakazi wapate muda wa kupumzika na kshuhulikia mambo yao binafsi. uaona kuwa kupumzika ni moja ya vigezo vya kuinua ari kazini. mfanyakazi akipumzika vizuri hupata ari zaidi ya kazi. muhimu muwzeshe kwa vitendea kazi bora na technolojia bora ufanisi utapaa tu mkubwa.

  kabla hujaongea jambo fanya utafiti kwanza.
   
 6. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,720
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  naungana na wachangia hoja wengine...

  muhimu ni ufanisi kazini na si kukaa muda mwingi pasi na ufanisi.kwa hiyo hata kwa sikukuu hizi tulizo nazo bado tunaweza kupiga hatua kimaendeleo kama tutaongeza ufanisi lakini kama kila kitu kitendelea kuwa ni kwa mazoea...hatutofika kokote hata tukiondoa sikukuu zote ikabaki ya uhuru na wafanyakazi.
   
Loading...