Ombi la Dharula : CAF ichunguze haraka vyumba vya kubadilishia nguo kwenye uwanja wa Martyrs Kinshasa

Hizi za chakubanga
 

Attachments

  • IMG-20190120-WA0020.jpg
    IMG-20190120-WA0020.jpg
    62.3 KB · Views: 16
Upo uwezekano mkubwa sana kwa chumba ambacho timu yetu ya simba ilipewa kuwekewa kitu kibaya , haiwezekani Simba kucheza vile , ni lazima kutakuwa na kitu kimefanyika , hii si ile simba tunayoifahamu , napinga vibaya sana .

Na kwa hili ni lazima timu ya AS VITA ifungiwe maisha , hii michezo ya kupuliza dawa za usingizi kwenye vyumba vya timu pinzani imepitwa na wakati

Nakala - Ismail Aden Rage
Bangi mbaya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fikra hasi na dalili za kuchanganyikiwa. TZ bado hatuna wachezaji na timu bora. Siku zote mpira wetu unachezwa na waandishi wa Habari magaazetini, kwenye maredio na TV. Ni aibu. Hatuna wachezaji walio consistency leo anabahatisha kucheza vizuri kwa nguvu za mungu na inapotokea hivyo anasifiwa sana lakini mechi ya kesho anaharibu huwezi amini. Na masifa yamewajaa. Jana ndiyo mwisho wa Simba tunawasubiri kwenye ligi jitahidini mje haraka au sivyo aibu ni yenu.
 
Facts
Usiwe na ushabiki wa kishamba hatuna timu ya ushindani kama unavyodhani.

Ulijua Simba atamfunga AS Vita? Uwe unatumia akili vizuri basi, siyo kisa una mahaba na Simba basi hata akili nazo uwape.

Mimi huwa ni shabiki msema ukweli sina konakona kama nyoka.

SIMBA HATUTAPATA POINT HATA MOJA KWENYE MECHI ZA UGENINI. Ukitaka meza ukiona chungu tema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule msemaji ni kilaza sijapata kuona. Anavyoichukulia Simba ni kama anaona ni timu kubwaaa kuliko hata hao washindani wake.

As Vita inajua mikikimikiki ya michuano ya CAF na imefanikiwa kwa kiasi kikubwa na iko mbali sana kuliko timu yetu ila ushabiki wa upofu unatudanganya kuwa tunaweza kwenda Kongo na tuje na matokeo...

Hata tukienda Algeria wale waarabu tuliodhalilisha hapo Taifa watashangaza wengi kule kwao. Hakuna timu pale.
Kila mwenye ufahamu aelewe kwamba hawa vita ni finalists wa mwaka Jana. Sasa manara duuuu na waswahili wenzako wanashindwa kutumia akili kidogo ili nyingine wafanyie mambo mengine....duuu
 
Simba walihama hotel kwa kuhofia fitna wakasahau hawawezi kuhama uwanja!! Pale DRC ni machinjio ya timu ngeni kwa nafasi walizokosa wale Vita ni jambo la kumshukuru Mungu, fedhea ingeweza kuwa kubwa zaidi.
2nd half kocha alijitahidi kuwaambia wachezaji wetu kucheza pressing football kwa kuanzia na strikers lakini tatizo likabaki kwa beki za kati kupitika kirahisi kabisa.
Tumefundishwa kutumia vizuri mipira iliyokufa wale Vita mipira ya kona na faulo unaanza kuhesabu goli.
Muhimu tujipange kwa game za nyumbani ambapo wapinzani wengi wanakuja kutafuta sare
 
Back
Top Bottom