Ombi la Dharula : CAF ichunguze haraka vyumba vya kubadilishia nguo kwenye uwanja wa Martyrs Kinshasa

Mkuu acha kuweka sababu hapo,kiukweli tumezidiwa kimpira na watu wa nje ya afrika mashariki,bado tuna safari ndefu mpaka kuwafikia,kumbuka hao ni AS Vita tu, huko kuna TP Mazembe kuna Al Ahli na wengine.ukileta imani za kiswahili jua kabisa hufiki mbali.Mpira ni mguuni na kila mmoja anauona unavyochezwa.wacha kuweka visingizio unachotakiwa na ww kujipanga tu.mpira wa cku hizi kila mmoja anajivunia kwao,nawe pigani ua ili mradi kwako hatoki mutu.mcheza kwao hutunzwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka uzi mmoja humu niliwahi kusema Wawa sio beki mzuri akikutana na mshambuliaji wenye kasi. Kuna jamaa alini ignore sana. Sasa jana yametimia hata penati amesababisha yeye.
Usiwe na ushabiki wa kishamba hatuna timu ya ushindani kama unavyodhani.

Ulijua Simba atamfunga AS Vita? Uwe unatumia akili vizuri basi, siyo kisa una mahaba na Simba basi hata akili nazo uwape.

Mimi huwa ni shabiki msema ukweli sina konakona kama nyoka.

SIMBA HATUTAPATA POINT HATA MOJA KWENYE MECHI ZA UGENINI. Ukitaka meza ukiona chungu tema.
 
Hahahaaaaaa! Eti napinga vibaya mno! Hahahaaaa kweli wewe ni mbumbumbu Mkuu! Unadhan Caf hawana chakufanya mpaka waanze kuchunguza hisia zako? Waambie TFF waanze kuchunguza mchezo wenu na Mashujaa kwanza maana pia mlicheza mpira mbovu sana kisha wachunguze Azam maana hata fainali ya mapinduzi mlirukaruka tu uwanjani.

By the way wewe ni mpinzni wa kila kitu hata serikali inayokufanya uandike uozo wako unaipinga kila iitwayo Leo.

Ila unahaki ya kulalamika goli tano zinauma I see asikwambie MTU.

Wewe ni mwanamke najua unajua shughuli ya goli tano ikoje inahusisha mpaka kuchubuliwa ..hahahaaaa
HUYO NI "CHA LAWAMA" SIKU ZOTE KTK UBORA WAKE TENA AMESHAWAZIDI HADI WANA WA ISRAELI WALIPOMLALAMIKIA MUSSA JANGWANI TOKA KULE MISRI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Endapo Simba itawafunga AS Vita taifa naweza nikaamini hoja yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila pia Simba wachunguzwe ile mechi waliyoshinda 3 - 0 kabla ya wao kupigwa 5 - 0, maana huenda hizo ndizo tabia zake hasa kwa timu pinzani zinapokuja pale Uwanja wa Taifa.

Kwanini Simba FC ijishtukie tu bila kukubali matokeo kuwa walikamatika ktk kila idara uwanjani kimchezo jana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba walipaswa kucheza deep kujilinda zaidi na kutengeneza counter attack

Mechi za Africa ukicheza ugenini hupaswi kukabia kwenye highline kama walivyofanya Simba lazima utafungwa nyingi tu
Al Alhy na Esperansa pamoja na ubabe wao wote wakicheza a ugenini wanapaki basi na kupoteza muda wakitafuta sare wale sio wajinga wanajua mechi za Africa zilivyo

Sasa wewe unaenda kwa As Vita unasema tunaenda kushambulia matokeo yake lazima ule nyingi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana Mama kwa kichapo cha jana mpaka ulilala na viatu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wachezaji karibia wote ni 35+ walishatumika kila mahali unafikiri utashindaje.As Vita ni timu kubwa sana.Roul Shungu ni kocha mkubwa sana lakini ni kocha msaidizi pale, Uchebe hata CV take in ya kutafuta kwa tochi lkn ndo kocha mkuu simba unategemea nini? Unajifanya kwenda huku huna breki!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ili uwe shabiki mwenye msaada kwa timu yako lazima uone uovu na uzuri wa timu yako ila ukijidai kuona uzuri tu basi huo siyo ushabiki ni ujinga.

Simba tunatakiwa kuwa na wachezaji wa mpira siyo wachezea mpira.
 
Manara anawaharibu watu wa Simba, mi naungana na negativity attitude ya shafii dauda ikizingatiwa itaivusha simba kuliko positivity ya manara
Yule msemaji ni kilaza sijapata kuona. Anavyoichukulia Simba ni kama anaona ni timu kubwaaa kuliko hata hao washindani wake.

As Vita inajua mikikimikiki ya michuano ya CAF na imefanikiwa kwa kiasi kikubwa na iko mbali sana kuliko timu yetu ila ushabiki wa upofu unatudanganya kuwa tunaweza kwenda Kongo na tuje na matokeo...

Hata tukienda Algeria wale waarabu tuliodhalilisha hapo Taifa watashangaza wengi kule kwao. Hakuna timu pale.
 
Back
Top Bottom