Ombi la Bashe Kwa Wabunge Wa CCM Kuhusu Posho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombi la Bashe Kwa Wabunge Wa CCM Kuhusu Posho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Jun 24, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Ombi Langu kwa wabunge wa chama changu, si kila jambo kulipinga swala la Posho (sitting allowance) hakuna sababu ya kulivalia njuga na kulazimisha kulipata,wabunge wanapata Mshahara,posho ya kuwa nje ya kituo ,posho ya ubunge FEDHA HIZI zinawatosha ukiangalia hotuba ya zito tunasema pato la mtanzania ni 770,000 lakini kuna asilimia 20% ambao wanashikilia 42% ya pato la taifa (32trillion) kati ya hizo wakati 20% ya masikini wa chini kabisa wanashikilia only 7% ya pato la Taifa.

  Kwa mtazamo wangu ikiwa sitting allowance ambayo kwa ujumla wake ikipunguzwa tuta save 900bn fedha hizi zikiamuliwa kupelekwa katika sekta ya ELIMU kuondoa kero ya waalimu kuishi madarasani kwa kuwajengea nyumba, kwa majirani,ama kuondoa kero ya Mabweni ktk shule za kata,ama kuondoa kero ya MAABARA katika shule za kata,ama kupelekwa katika sekta ya Afya , tutakuwa kama Taifa tutamaliza tatizo kubwa sana tutaipunguzia serekali na walipa kodi mzigo wa fedha ambazo haziendi katika shughuli za maendeleo,Niwaombe wasiitazame hoja imetoka kwa nani wa chama gani waipokee na kuiunga mkono Mtakuwa mmeitendea HAKI nchi yetu,na watanzania ambao mustakabali wa maisha yao katika miaka mitano ijayo upo mikononi mwa serekali ya CCM (cham chetu) hata kama kama mnaipata kwa mujibu wa sheria na kanuni fanyeni cost benefit analysis kwa kuliangalia taifa na si nyinyi peke yenu.kama taifa tutfaidika zaidi fedh hizi msipopokea na kuamua kama bunge zipelekwe katika shughuli za maendeleo.

  Wapo wabunge ambao wana jenga Hoja ya kwamba Posho hizo zinawasaidia ktk shughuli za Majimbo, inawezekana inaukweli,lakini kama MFUKO WA MAENDELEO WA JIMBO ,POSHO YA UBUNGE 5M,ALLOWANCE YA KUKAA NJE YA JIMBO 80,000,MSHAHARA 2M vyote hivi vimeshindwa kukusaidia kuhudumia Jimbo basi hata hiyo Posho haita weza,naamini mnatuongoza tutawaona si wabinafsi mkiunga mkono hili kwani mnachpata kwa maisha yenu kinawatosha.

  Itendeeni haki Nchii hii katika kipindi hiki ambachi ambacho maisha yanazidi kuwa magumu shilingi inashuka, kuna vijana wenzetu million 11 wanahitaji msaada waliopo mashuleni na vyuoni wanahitaji msaada wenu mtakuwa mmetenda haki sana kwa kusamehe hicho kidogo,nimuombe Mbunge wangu aunge Mkono kusamehe hiyo Posho 70,000 ni Tofali 350 za kuchoma kwa bei ya kule kwetu ,mara siku za vikao ,ni fedha nyingi tutapata mabweni, maabara,ama fedha hiyo utakuwa umesaidia vijana wengi kulipiwa ada ktk shule za Kata. Kwahiyo ni vizuri likaungwa mkono jambo hili ili kuisaida Nchi.

  H@ki Ngowi
   
 2. K

  Kikambala Senior Member

  #2
  Jun 24, 2011
  Joined: Jun 28, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Muda mwingi mawazo yako huwa mazuri sana,ila ninachokiona ni kuwa hawa wa mawazo mgando aka magamba hawataki ukweli,watakuona kama mpinzani wao japo kuwa ni mmoja wao.ukizingatia ya kuwa ni mwajiriwa wa ra basi taaabu tupu.ila upo juuuuuu
   
 3. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bro u a an exellent player but being in a wrong team! jivue gamba nawe achana na utumwa fight in your own clean way, kama nyota yako ipo itang'ara tu,manake kwa sasa usemayo mazuri yanachafuliwa na hapo ulipo because hata hizo bilion 900 tunazoweza kusev jamaako RA anaweza kuzikwapua kwa kuleta hata kampuni feki ya kuuza vitabu vya shule.ushauri wangu fikiria future yako ya kisiasa then chukua maamuzi magumu ya kuachana na wrong team,najua una ka hofu ka kuvuliwa uraia,hii isikupe taabu,hata Jen Ulimwengu alipigwa the same mkwara na Ben lakini baadae kukatulia,ufanyalo sasa ni sawa na kumvisha nguruwe suti huku ukijua atarudi kwenye matope yaleyale. Usiharibu kipaji chako cha kisiasa find a right team,huko pamekwisha bro.
   
 4. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Bashe anaakili sana kulio yule kasuku msema chochote...
   
 5. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Mimi hupenda kuangalia mantiki ya hoja na sio mlete hoja. Kusema kweli Bashe amekuwa akileta hoja nyingi zenye mshiko. Walau Chama cha Magamba wageweza kuzifanyia kazi basi huko ndiyo kungekuwa kujivua gamba kwa ukweli na siyo usaniii wa akina RACHEL. ambao Leo tu Nape ametwambia lazima wavuliwe gamba lakini jioni hii tumeshudia tena unafiki mkubwa wa Magamba pale EL aliposhangiliwa bungeni zaidi ya JK. Nafikiri hata Nape mwenyewe ameogopa maana Chiligati naye ameonekana akipiga meza kwa nguvu.

  Bashe kama kweli unasimamia hicho unachokiamini nenda CDM, 2015 uchukue jimbo la Nzega kutoka kwa msanii Dr. Said Nassoro Bagaile alias Dr. Hamis Andrea Kingwangala. I know utakutana na mikwara mingi ya kuvuliwa uraia but believe me fainally you will prevail. GO BASHE
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hongera sana H. Bashe............ninafurahia sana kuona ulivyo bold kusema kile unachoamini ni sahihi..........wenzako wengi wameshindwa walau kuonyesha (si kutenda) this honesty...........
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,423
  Trophy Points: 280
  [h=2]Bashe ni nani? huyu mwarabu namuona ona tu ....naonaga thread zake[/h]
   
 8. L

  Logician Senior Member

  #8
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  It sounds good and logical. May any one tell me if MPs' salaries and allowances are taxable or not? if not, why they are not taxable?
   
 9. O

  Ogah JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Pia tusisahau kuuliza swali ..............nini msingi wa hizi posho zilizokuwepo muda wote huo?
   
 10. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wewe wacha kuwa kasuku! sitting allowance na waondoshewe wabunge kwa vile wao wana maposho mengine ya ktuosha kuendesha maisha. Sasa mie mtumishi wa umma nilie na mshahara wangu tu hiyo sababu ya wabunge kuachwa kulipwa posho inapply pia kwangu mimi?
   
 11. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kudos!
   
 12. K

  Karata JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Una hoja za msingi kabisa Bwana Bashe, lakini ww ni mwanachama hai wa CCM unatakiwa uwasilishe hizi hoja (maombi) katika vikao vya ndani vya chama chako ili wachukue maamuzi magumu otherwise, utakuwa kama kasuku tu.<br><br>Chukua hatua!&nbsp;
   
 13. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ingawa sijui kama ana dhamira ya dhati ya kuwasemea watanzania maskini, given his unwavering support kwa mafisadi ambao nao, kama walivyo wang'angania posho wanawamaliza watanzania, tena mafisadi kwa kasi kubwa, nakubaliana naye kwamba sasa ufike wakati wabunge wetu waangalie na kule wanakovuna kura. Waangalie hali za hayo mashamba yao ya kura na waelewe kwamba hali kule inazidi kuwa mbaya na tusipowaangalia hawa, ambao hata kusomesha watoto kwenye shule za kata hawawezi, nchi hii itakuja kufutika kwenye ramani huko mbele. Ubinafsi huu, unaofanana na wabunge wa nchi jirani ya Kenya utakuja kutuletea machafuko huko mbele maana akitokea mtu mmoja aka-take advantage ya shida za wananchi, akawahamasisha kuingia mtaani, nchi aliyotuachia Mwalimu haitakuwa moja tena. Chonde wabunge wetu, fungueni macho!
   
 14. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Natabiri huyu Bashe hatodumu CCM.
  Atatafutia shutuma nzito mpaka atasahaulika kabisa kwenye ulimwengu wa siasa.
   
 15. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Pamoja na undumila kuwili wako na mapungufu uliyonalo kwa hilo nakuunga mkono kwa mara ya kwanza toka nikusikie katika harakati zako za kisiasa,ni kama vile Paulo wa kwenye biblia
   
 16. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na yeye kapatia hili tu na dhamira yake haijawa wazi sana! Jamaa ni katika wale foot soldiers wa mafisadi.
   
Loading...