Ombi kwa Waziri wa elimu prof. Ndalichako kuhusu ufadhili wa masomo ya ualimu kwa kozi za sayansi

mzee wa giningi

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
519
336
Nichukue fursa hii kukupongeza Mhe.Waziri wa elimu sayansi na teknolojia kwa jitihada zako za kuboresha elimu yetu nchi pia nichukue fursa hii kukuomba kuwa mwaka huu mmeleta stashahada za ualimu kwa upande wa sekondari lakini zaidi mmetoa vipaumbele kwa masomo ya sayansi ili kuziba pengo la uhaba wa walimu wa sayansi ni jambo zuri sana hilo lakini ninachoiomba wizara ya elimu itoe ufadhili wa masomo ya ualimu kwa diploma kwa upande wa sekondari kwa vyuo vya serikali ambavyo vipo chini ya wizara ili kuwawezesha hawa wanafunzi wasome ukizingatia gharama kubwa za masomo kwa vyuo vya serikali wanafunzi wengi wanaochanguliwa kusomea ualimu masomo ya sayansi wanashindwa kupata karo na kushindwa kuripoti vyuoni serikali ichukue jukumu hili kuwafadhili hawa wanafunzi kwenye vyuo vya serikali kama wanavyofanya wizara ya Afya naiomba serikali ichukue jukumu hili ili tupate walimu wengi wa masomo ya saayansi .
e16622d4cbc61c5ea70ee8f17599395d.jpg
5621c51de3e897208054dba66d98567d.jpg
3a082f716acc6140551410595ff16716.jpg
 
Back
Top Bottom