Ombi kwa Waziri Mkuu na Waziri wa TAMISEMI

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
31,829
33,224
Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu naamini ni wenye afya njema na mnaendelea kuwatumikia wananchi wa Tanzania vema kabisa, Naomba kuwasilisha kwenu mambo mawili na hasa katika wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi wa Mbunge na Madiwani.

Sisi wakazi wa Tungi Manispaa ya Morogoro tumesahaulika kwa kila kitu, tangu mwezi wa sita tumeshuhudia barabara za mitaa zikichongwa kwa kiasi cha kupitika vizuri kabisa lakini sisi wana tungi barabara zetu hazijatengenezwa na hivyo kufanya usafiri kuwa wa shida kabisa, wagonjwa wanasafirishwa kwa shida, wanafunzi wanachelewa kwenda shule na kurudi majumbani, watumishi wa serikali nao wanafika maofisini na kurudi nyumbani kwa taabu, na hata likitokea janga lolote huku nina uhakika jeshi la uokoaji halitafika kwa wakati sababu barabara ni mbaya kupindukia wakati RC, DC na DED wapo.

Kwakuwa njia ya kutoka Dodoma na kwenda Da es salaam inapita karibu sana na eneo hili, sisi wanatungi, tunaomba ikiwapendeza ninyi wawili mpite kwa kushitukiza kwenye eneo hili mshuhudie hali ilivyo hovyo, mwanzoni tulidhani TARURA ni mkombozi lakini kumbe wamekuwa ni tatizo juu ya tatizo, ushahidi upo kwenye barabara inayoanzia Mountfort karibu na Jordan University hadi Tungi imevurugwa vibaya kabisa kama vile haikuwa na injinia aliyesomea, njia hiyo haipitiki, fedha za walipakodi zimechezewa katika eneo hilo, inashangaza RC, DC na DED hawajatupia macho ubadhirifu huu wamekaa kimya kabisa wakati ubora wa kazi ni 0.

Naamini Rais naye anapita humu jukwaani, huenda akapita akajionea jinsi watendaji aliotupa wanavyofanya mambo kizembe. kwasasa njia mkombozi kama kuna dahrura ni ile inayotumiwa na wajenzo wa SGR ambayo tukitaka kuitumia lazima tuende hadi Kihonda VETA au Morogoro Junior Seminary ambayo ni ndefu na inatupeleka off-direction.

Natanguliza shukurani kwa kulichukulia suala letu seriously.
 
Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu naamini ni wenye afya njema na mnaendelea kuwatumikia wananchi wa Tanzania vema kabisa, Naomba kuwasilisha kwenu mambo mawili na hasa katika wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi wa Mbunge na Madiwani..
Hamieni CCM
 
Back
Top Bottom