thetallest
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 8,256
- 9,085
Kumekuwa na wimbi la wanasiasa kujitafutia umaarufu kila linapotokea tukio lolote nchini, hasa majanga, wanasiasa hukimbilia kuita media na kutoa matamko ya kila aina kabla ya uchunguzi, ili mradi kutafuta attention kwa wananchi, hili si jambo jema, na Mara nyingi wanasiasa hawa huishia Kuumbuka baada ya uchunguzi wa kina (kitaalamu) kutoka.
Kuna msemo wa kiswahili usemao haraka haraka haina baraka.
Nawashauri wasiwe wepesi kutoa matamko, wasubiri taarifa ya serikali itoke ,hapo ndipo wanaweza kutoa maoni, matamko, na hisia zao dhidi ya serikali ya chama tawala. Wakiendelea hivi wanavyofanya wataumbuka Sana na kupoteza mvuto kwa wananchi ,ni maoni yangu ,hili watalifanyia kazi .
Mwisho,
siasa zetu ziwe za kujenga umoja wa kitaifa, si za kutugawa, siasa za kuichonganisha serikali na wananchi wake hazikubariki, si Tanzania Pekee, bali duniani kote. Nilitegemea kuona viongozi wa kisiasa wa vyama mbalimbali wakiungana na chama tawala kwenye msiba huu huko ukerewe, matokeo yake hamshiriki na mnatolea matamko mkiwa mbali na eneo la tukio ,mungu fariji nyoyo za wafiwa, amen