Hili ni ombi maalum kutoka kwangu binafsi kwenda kwenu wanaJF. Moderators naomba mnisaidie kuliweka mahali muafaka ambako wengi watalisoma.
Kama baadhi yenu mnavyofahamu, nafanya masomo ya PhD katika Social Policy. Nimeshafanya tafiti kadhaa, sasa kuna sehemu imebakia ambayo naamini watu wa humu JF wanaweza kuchangia kunipa data. Kifupi ni kwamba nakusudia kutengeneza discussion guide ya kukusanya some qualitative data, na ninaona hii forum itakuwa na participants wazuri sana wa hoja ninazohitaji zijadiliwe. Ninaomba kuuliza masuala kadhaa kabla sijaendelea na mpango huu:
1. Naomba moderators ama owners wa hii site mniambie kama mnakubali matumizi ninayotaka kufanya ya hii site
2. Kama mnayakubali, ni masharti gani mngependa niyafuate? Kama mnazo terms maalum za jambo kama hili, naomba kuzijua
3.Washiriki wa hii site, mna maoni gani kuhusu mie kukusanya kutoka kwenu data ambazo nitazitumia kwenye thesis yangu? Ni mambo gani mngependa niyazingatie katika kutumia data mtakazonipa?
Hata kama itahusisha gharama fulani fulani, niko tayari kulipa, muradi munipe tu utaratibu wa namna ya kukubaliana malipo na nani wa kumlipa, maana hii research inayo budget kidogo ya lengo hilo (lakini kama wengi mnavyojua, tafiti za masomo huwa hazina pesa nyingi, kwa hiyo naomba consideration kwa hilo), na hata mkiamua kujitolea taarifa kumsaidia mtanzania mwenzenu kama tunavyoshiriki mijadala mingine bila malipo nitashukuru zaidi.
Asanteni.
Brian J.Y. Kithuku