Ombi kwa wanaJF kushiriki research yangu

Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,395
209
Hili ni ombi maalum kutoka kwangu binafsi kwenda kwenu wanaJF. Moderators naomba mnisaidie kuliweka mahali muafaka ambako wengi watalisoma.

Kama baadhi yenu mnavyofahamu, nafanya masomo ya PhD katika Social Policy. Nimeshafanya tafiti kadhaa, sasa kuna sehemu imebakia ambayo naamini watu wa humu JF wanaweza kuchangia kunipa data. Kifupi ni kwamba nakusudia kutengeneza discussion guide ya kukusanya some qualitative data, na ninaona hii forum itakuwa na participants wazuri sana wa hoja ninazohitaji zijadiliwe. Ninaomba kuuliza masuala kadhaa kabla sijaendelea na mpango huu:
1. Naomba moderators ama owners wa hii site mniambie kama mnakubali matumizi ninayotaka kufanya ya hii site
2. Kama mnayakubali, ni masharti gani mngependa niyafuate? Kama mnazo terms maalum za jambo kama hili, naomba kuzijua
3.Washiriki wa hii site, mna maoni gani kuhusu mie kukusanya kutoka kwenu data ambazo nitazitumia kwenye thesis yangu? Ni mambo gani mngependa niyazingatie katika kutumia data mtakazonipa?

Hata kama itahusisha gharama fulani fulani, niko tayari kulipa, muradi munipe tu utaratibu wa namna ya kukubaliana malipo na nani wa kumlipa, maana hii research inayo budget kidogo ya lengo hilo (lakini kama wengi mnavyojua, tafiti za masomo huwa hazina pesa nyingi, kwa hiyo naomba consideration kwa hilo), na hata mkiamua kujitolea taarifa kumsaidia mtanzania mwenzenu kama tunavyoshiriki mijadala mingine bila malipo nitashukuru zaidi.

Asanteni.

Brian J.Y. Kithuku
 
mm binafsi niko tayari kukusaidia kwa nitakaloliweza.

pia nnaona ni jambo zuri na la maana. ss watanzania tunayohaki ya kusaidiana kwa mengi ikiwemo hili.

nnategemea wenzangu na uongozi wa jf watafurahishwa na hili na kukuunga mkono
 
Mwenzetu, Binadamu, Mtanzania, anahitaji msaada fulani kutoka kwetu. Km uwezo tunao, sioni km kuna kikwazo chochote!

I THINK THAT'S ONE AMONG THE MANY THINGS WE'RE HERE, IN THIS WORLD AND IN THIS FORUM, FOR.

HAYO NDIYO MAONI YANGU.
 
Comrade Kithuku,
Mimi niko tayari pia kushiriki- as your countryman and JF member- unajua mchango wako pia hapa tunaupenda na haswa hii signature yako.

Wacha kwanza moderators watoe msimamo based on rules za JF!
 
Hili ni ombi maalum kutoka kwangu binafsi kwenda kwenu wanaJF. Moderators naomba mnisaidie kuliweka mahali muafaka ambako wengi watalisoma.

Kama baadhi yenu mnavyofahamu, nafanya masomo ya PhD katika Social Policy. Nimeshafanya tafiti kadhaa, sasa kuna sehemu imebakia ambayo naamini watu wa humu JF wanaweza kuchangia kunipa data. Kifupi ni kwamba nakusudia kutengeneza discussion guide ya kukusanya some qualitative data, na ninaona hii forum itakuwa na participants wazuri sana wa hoja ninazohitaji zijadiliwe. Ninaomba kuuliza masuala kadhaa kabla sijaendelea na mpango huu:
1. Naomba moderators ama owners wa hii site mniambie kama mnakubali matumizi ninayotaka kufanya ya hii site
2. Kama mnayakubali, ni masharti gani mngependa niyafuate? Kama mnazo terms maalum za jambo kama hili, naomba kuzijua
3.Washiriki wa hii site, mna maoni gani kuhusu mie kukusanya kutoka kwenu data ambazo nitazitumia kwenye thesis yangu? Ni mambo gani mngependa niyazingatie katika kutumia data mtakazonipa?

Hata kama itahusisha gharama fulani fulani, niko tayari kulipa, muradi munipe tu utaratibu wa namna ya kukubaliana malipo na nani wa kumlipa, maana hii research inayo budget kidogo ya lengo hilo (lakini kama wengi mnavyojua, tafiti za masomo huwa hazina pesa nyingi, kwa hiyo naomba consideration kwa hilo), na hata mkiamua kujitolea taarifa kumsaidia mtanzania mwenzenu kama tunavyoshiriki mijadala mingine bila malipo nitashukuru zaidi.

Asanteni.

Brian J.Y. Kithuku

Personaly nafikiri as long as its just a social matters/datas sioni tatizo lolote. Nafikii true responce itakuja wakati utakapokuwa umeweka the "exactly problem/asighnment yako kwetu" otherwise ..much welcome Sir!!Hakika Mimi sitahitaji mshiko wowote. Maana hatawatakaotaka kukamtishwa kitu kidogo sijui sijuiitakujwaje...etc
 
Kaka Kithuku.
Usijali nipo tayari kushiriki katika huo mchakto wako bila malipo yoyote kwani utakuwa msaada sana hapo baadae katika kuliendeleza hili libeneke.
 
Hakuna shida...we Nitumie tu kwenye Simu Yangu kama $ 2000 basi...Thesis Yako Itakua Funga kazi...
 
1. Naomba moderators ama owners wa hii site mniambie kama mnakubali matumizi ninayotaka kufanya ya hii site

Kithuku,

Tuwie radhi kwa kuchelewa kukujibu. Kifupi ni kuwa majukumu yanakuwa mengi hadi tunashindwa kusoma kila post. Katika pitia yangu nimekumbana na ujumbe huu na nimeonelea ni vema nikujibu haraka niwezavyo.

1. Ruksa kufanya tafiti zako kwa aidha kuuliza ama kufanya nama unayodhania ili mradi usikiuke sheria za JF. Katika tafiti zako tafadhali zingatia haya:
  • Ni kosa kubwa kuapa ama kuwaapisha wanachama wetu katika hoja zozote unazotaka wachangie katika kufanikisha tafiti zako.
  • Ni kosa kubwa kuandika jina ama majina halisi ya mmojawapo wa wanachama wetu bila hiari yake.
  • Katika tafiti zako hakikisha unasoma hoja kwa mapana na kuchambua yale yaliyo muhimu kwako. Kama hujaridhika na hoja husika omba maelezo ya ziada na chanzo cha habari ama hoja husika.
  • Si kila utakachopewa juu ya tafiti zako kitakuwa sahihi kwa asilimia 100 hivyo nakushauri kukifanyia utafiti wa ziada. Hii itakusaidia kufanya tafiti zilizo sahihi; tunakushauri uchambue hoja ama maelezo utakayopewa na tunaomba kukiri kuwa hayo yatakuwa ni mawazo ya watu na si msimamo wa JF Administration kwa ujumla wake. Hatutobeba lawama kwa kutochambua vema hoja za waliokushauri ama kukusaidia katika tafiti zako.
  • Kuomba hela ama kumlazimisha mwanachama kukuchangia ama kukutumia pesa ni kosa. Mwanachama atakayekusaidia hela atafanya hivyo kwa hiari yake (ama wewe kumtumia hela). JamboForums.com haitohusika na udanganyifu wa aina yoyote utakaofanyika katika mbadilishano wa fedha.
  • Jamboforums.com haitakuchangisha kiwango chochote cha fedha na ukifanya hivyo fanya kwa hiari yako na mapenzi yako kwa JF.
2. Utakapofungua mjadala husika tafadhali ufungue kwenye Jukwaa la Elimu ama tufahamishe kama kuna haja ya kuwa na sub-forum ya Tafiti. Tuko tayari kukusaidia katika hilo.

3. Kamwe hatutohusika (JF Administration) kwa namna yoyote katika kukwambia nani ni nani na yuko wapi. Tunasikitika endapo utakuwa na uhitaji wa hilo kwani haliwezekani kabisa.

JF haina sheria kali za kukubana katika kufanya tafiti zako kwakuwa inaheshimu mawazo ya kila mwanachama. Makosa makubwa sana ambayo tungeomba usifanye ni hayo niliyoainisha hapo juu.

Mwisho nakutakia kila la kheri katika tafiti zako na ukifanikiwa tafadhali tushirikishe. Sikukuu njema za mwisho wa mwaka.

Invisible
 
nitajitahidi kuchangia kadri ya ninavyofahamu ilikufanikisha utafiti wako,mimi nahitaji bata mzinga kwa ajili ya x mas.
 
Mkuu Kithuku,
Nakuheshimu. Nadhani umepata majibu mazuri kutoka kwa wana JF wenzangu na kwa Moderatorz, kwa hiyo hebu tuletee mada ya huo utafiti ili tuendelee kuumega na kuchangia kile kidogo tulichonacho, kama kawaida ya JF.
Binafsi nipo tayari kukusaidia kwa kila hali, kwani na mie ni mtafiti ingawa nafanya utafiti katika uwanja tofauti kabisa na wa kwako.

Karibu sana.
 
Back
Top Bottom