Ombi kwa wahusika kuhusu ajira kwa wahitimu

jukiha

Member
Jan 9, 2017
72
27
Waheshimiwa viongozi mnaohusika na utoaji wa ajira naomba muwe na huruma juu ya vijana waliosomeshwa na wazazi maskini kwa kuuza Mali zao mbalimbali kwa kuamini vijana wao watawasaidia kupata ahueni ya Maisha wamalizapo masomo na kuajiriwa

Pasipokutegemewa hali imekuwa tofauti vijana wamehitim wapo tu mitaani wakizurura na vyeti vyao sekta binafsi kuomba kazi bila mafanikio

Kauli zinazidi kuwa nyingi za kuwashauri wajiajiri lakini ikumbukwe kujiajiri lazima mtaji uwepo na kama kujiajiri ilikuwa ndoto yao zile hela za wazazi zilizoishia shuleni pamoja na mda waliopoteza wangekuwa wamejiajiri na wangekuwa na Maisha mazuri , ila kujiajiri haikuwa kipaumbele

Imefikia mahali wasomi wanadharauliwa mana unakuta wale ambao hawakuendelea na masomo wanamaisha mazuri na wameshafikia malengo yao mengi ukilinfanisha na Hawa hahitimu , pia imekuwa ngum kuwashawishi hata waliopo mashuleni kuhusu faida ya elimu maana wanaona wahitim wamejazana mitaani wakiwa na Maisha magum kupita ambao hawakuendelea na masomo

Muwafikirie vijana kwa upya ili waweze kufikia malengo yao



#Simbachawene#
[HASHTAG]#Prof[/HASHTAG] Ndalichako#
 
Shida kubwa watoto wao hawana tatzo au uhtaj na ajira ndo maana wapo kimya kama hawaoni tatzo hili,

Wawe binadamu kuhurumia wengn nasio kujijua WENYEWE tu
 
Shida kubwa watoto wao hawana tatzo au uhtaj na ajira ndo maana wapo kimya kama hawaoni tatzo hili,

Wawe binadamu kuhurumia wengn nasio kujijua WENYEWE tu
Kweli aliyekuwa na shibe hamkumbuki mwenye njaa
 
Back
Top Bottom