Ombi kwa wagombea Ubunge na Urais juu ya lugha ya kufundishia mashuleni kubadilishwa kutoka Kiswahili kuwa Kiingereza

CHEDU

Senior Member
Dec 24, 2015
150
250
Ombi kwa wagombea Ubunge na Urais juu ya lugha ya kufundishia mashuleni kubadilishwa kutoka kiswahili kuwa Kiingereza.

Mnapoelekea uchaguzi mkuu wagombea wote wa ngazi zote na kwa vyama vyote hasa wa chama tawala tafadhali tunaomba mchukue ajenda hii kwa upande wa elimu mkadilishe lugha ya kufundishia kutoka Kiswahili kuwa Kiingereza.

Hali ni mbaya sana kwa shule zetu za serikali wanafunzi wanahangaika sana pale wanapotoka shule za awali kujiunga na sekondar wanapata tabu sana kuyaelewa masomo kwa maana lugha inabadirika na wao wanafunzi awali walizoeshwa kutumia kiswahili katika kujifunza.

Hii imepelekea wanafunzi wengi kutoelewa wanachofundishwa na kuchukia shule, na hata hao wachache wanaofaulu bado shida ipo hasa katika kujieleza kwa lugha ya kiingereza hata baada ya masomo watu wanapata shida sana katika interview wakati wa kutafuta kazi hali ni mbaya sana.

Cha kushangaza viongozi wengi nchi hii wanakumbatia mfumo wa lugha kiswahili mashuleni wakati watoto wao wanawasomesha shule za private ambazo lugha za kufundishia ni za Kiingereza, hii ni roho mbaya na ubinafsi wa hali ya juu sana mnahalibu maisha ya watu.

Namaliza kwa kusema hii kitu ni rahisi kama watia nia na wagombea mkiichukua kama ajenda ili kuwanusuru vijana wetu huku mashuleni bado hamjachelewa, tukianza na chekechea darasa la kwanza hadi chuo kikuu naamini hata viwango vya ufaulu vitapanda.
 

Kishimbe wa Kishimbe

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
3,174
2,000
Kwa usalama wa Taifa, kwa masafa marefu, napendekeza mfumo wa kuanza kutumia kiingereza kwa masomo yote kuanzia darasa la tano urudishwe ... na bidii iongezwe kuifundisha, lugha hii muhimu sana kimataifa, katika ngazi za chekechea na madarasa ya awali!

NB: Wanasiasa wanaotaka kuua Kiingereza, na sio kukuza Kiswahili, wana nia ovu nyuma ya mapazia. TAFAKARI!
 

CHEDU

Senior Member
Dec 24, 2015
150
250
Kwa usalama wa Taifa, kwa masafa marefu, napendekeza mfumo wa kuanza kutumia kiingereza kwa masomo yote darasa la tano! Na bidii iongezwe kuifundisha, lugha hi muhimu sana kimataifa, katika ngazi za chekechea na madarasa ya awali!

NB: Wanasiasa wanaotaka kuua kiingereza, na sio kukuza kiswahili, wana nia ovu nyuma ya mapazia. TAFAKARI!
Lakin ilitakiwa kianze kufundishwa kuanzia chekechea au darasa la kwanza kama kweli tuna nia ya dhati kuiinua nchii.

Unajua tukifanya hivo itaongeza vijana kujiamini hata kama akifeli shule kale kalugha katamuongezea ujasiri hata wa kufanya biashara nje ya mipaka ya nchi hii.
 

CHEDU

Senior Member
Dec 24, 2015
150
250
Kwani mzee baba mwenyewe anajua kiingereza? Tuanzie hapo.
Yeye kujua au kutojua sio tatizo

Tatizo ni tuanze kuwaandaa watoto sasa hivi na kiswahili libaki kama somo moja tuh litakalofundishwa kwa madarasa yote.
 

Executivesister

JF-Expert Member
Aug 7, 2012
422
500
Sitasahau nilifaulu kutoka St kayumba kuingia Form One akaja mzungu mmoja kutufundisha sikuelewa hata neno moja kwa dk40 alizokaa darasani,wenzangu walivyokuwa wananitegemea ilibidi nijifanye naumwa kesho yake nisiulizwe homework,hili suala ni la muhimu Sana,liangaliwe kwa jicho la tano kabisa.Namshukuru Mungu nilitumia juhudi binafsi hadi kufika chuo nikawa nipo vizuri Sana kwenye lugha.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
45,685
2,000
Tatizo ni kuwa tuna walimu wachache wanaomudu lugha ya Kiingereza. Kwa kuanzia itabidi miaka mitano ya kwanza kuandaa walimu kwanza.
 

Mbogo nyeusi

Senior Member
Dec 27, 2019
169
500
Tatizo ni kuwa tuna walimu wachache wanaomudu lugha ya Kiingereza. Kwa kuanzia itabidi miaka mitano ya kwanza kuandaa walimu kwanza.
CHEDU,
Ina kera Sana watoto wa walala hoi ndio wanaambiwa wajifunze na kuenzi kiswahili huku watoto wa mabwenyenye wanasoma kwa kutumia lugha ya mabeberu,

Moja ya vipao mbele vya mgombea urais wa chadema"mtia nia",Nyalandu katika elimu ni kubadili lugha ya kufundishia kuwa kiingereza kwa shule zote toka awali ni vizuri Sasa likaingizwa kwenye ilani zao za chama,vile vile baadhi ya halimashauri na mikoa wameanza kujenga shule maalumu za serikali za mchepuo wa kiingereza ambazo zina ada ndogo,

Kwa waendesha shule binafsi hili swala ni mwiba itabidi wafunge shule zao
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,093
2,000
Tatizo ni kuwa tuna walimu wachache wanaomudu lugha ya Kiingereza. Kwa kuanzia itabidi miaka mitano ya kwanza kuandaa walimu kwanza.
SIO kweli vyuo vya ualimu hufundishwa masomo yote kwa Kiingereza sio Kiswahili

Pili serikali ina shule kibao za msingi za english medium mikoa mingi tu. SERIKALI NI KUAMUA TU KUBADILISHA LUGHA TU YA KUFUNDISHIA WALIMU WATAFUNDISHA BILA SHIDA YEYOTE HAWA HAWA WALIOPO
 

Makuku Rey

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
2,440
2,000
Lakin ilitakiwa kianze kufundishwa kuanzia chekechea au darasa la kwanza kama kweli tuna nia ya dhati kuiinua nchii.

Unajua tukifanya hivo itaongeza vijana kujiamini hata kama akifeli shule kale kalugha katamuongezea ujasiri hata wa kufanya biashara nje ya mipaka ya nchi hii
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
45,685
2,000
Ina kera Sana watoto wa walala hoi ndio wanaambiwa wajifunze na kuenzi kiswahili huku watoto wa mabwenyenye wanasoma kwa kutumia lugha ya mabeberu,

Moja ya vipao mbele vya mgombea urais wa chadema"mtia nia",Nyalandu katika elimu ni kubadili lugha ya kufundishia kuwa kiingereza kwa shule zote toka awali ni vizuri Sasa likaingizwa kwenye ilani zao za chama,vile vile baadhi ya halimashauri na mikoa wameanza kujenga shule maalumu za serikali za mchepuo wa kiingereza ambazo zina ada ndogo.

Kwa waendesha shule binafsi hili swala ni mwiba itabidi wafunge shule zao
Kwa muda mrefu watoto wa wapigiwa kura tu ndiyo wanaofaidi keki ya taifa. Watoto wetu wapiga kura wanaandaliwa kuwa wapiga kura wa miaka ijayo.

Tuna enzi Kiswahili lakini Kiingereza ni lugha ya dunia, lazima tuwe na uwezo wa kuwasiliana ki dunia katika maswala yote kuanzia biashara, uchumi, afya nk
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
45,685
2,000
SIO kweli vyuo vya ualimu hufundishwa masomo yote kwa kiingereza sio kiswahili
pili serikali ina shule kibao za msingi za english medium mikoa mingi tu.SERIKALI NI KUAMUA TU KUBADILISHA LUGHA TU YA KUFUNDISHIA WALIMU WATAFUNDISHA BILA SHIDA YEYOTE HAWA HAWA WALIOPO
Mimi mwenyewe ni mwalimu na sijui Kiingereza.
 

Makuku Rey

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
2,440
2,000
Lakin ilitakiwa kianze kufundishwa kuanzia chekechea au darasa la kwanza kama kweli tuna nia ya dhati kuiinua nchii...

Unajua tukifanya hivo itaongeza vijana kujiamini hata kama akifeli shule kale kalugha katamuongezea ujasiri hata wa kufanya biashara nje ya mipaka ya nchi hii

Acha kutukuza vya wageni!!aliyekwambia kujua kingereza kunainua nchi nan?!!hawa wasomi wa miaka hii sijui MNA nini vichwani mwenu!!!!!
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,093
2,000
Mimi mwenyewe ni mwalimu na sijui Kiingereza.
Una matatizo sekondari usome miaka minne kiingereza uende chuo usome Kiingereza kote ufaulu masomo uliyosoma kwa Kiingereza halafu mwisho wa siku useme hujui kiingereza hujielewi.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
45,685
2,000
una matatizo sekondari usome miaka minne kiingereza uende chuo usome kiingereza kote ufaulu masomo uliyosoma kwa kiingereza halafu mwisho wa siku useme hujui kiingereza hujielewi
Mwalimu wangu wenyewe hawakuwa wanaijua lugha si ajabu makosa niliyokuwa ninaandika Seko Dari na chuoni hawakuyaona na walinipa ufaulu.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,093
2,000
Mwalimu wangu wenyewe hawakuwa wanaijua lugha si ajabu makosa niliyokuwa ninaandika Seko Dari na chuoni hawakuyaona na walinipa ufaulu.
Haya walimu wakupe ufaulu na baraza la mitihani ambao hawakukufundisha nao wakupe ufaulu bado useme hujui kiingereza sio kweli mfano unafundisha two times two kweli unashindwa kusema is equal to four!! sio kweli

Kiingereza cha kufundishia huwezi shindwa
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
45,685
2,000
haya walimu wakupe ufaulu na baraza la mitihani ambao hawakukufundisha nao wakupe ufaulu bado useme hujui kiingereza sio kweli mfano unafundisha two times two kweli unashindwa kusema is equal to four!! sio kweli

kiingereza cha kufundishia huwezi shindwa
Sasa hiki ndiyo Kiingereza kinachomuandaa mtoto kuwa na umahiri wa lugha wa kuweza kuwasiliana na mataifa mengine?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom