Ombi: Kwa Waandishi wa habari za uchunguzi!

Shomari

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,112
241
Wasalaam!
Hapa nilipo ninaandaa hadithi inayomhusu mwandishi wa habari za kichunguzi ( Investigative Journalist ). Binafsi sina uelewa wowote kuhusu uandishi wa habari , bali nina mapenzi na kuandika hadithi.
Mambo ninayotaka kujua ni haya :

1. Ni ipi miiko ya uandishi na ufuatiliaji wa habari za kichunguzi ?

2. Ni ipi mipaka inayotenganisha kati ya mwandishi wa habari za uchunguzi na Inspekta wa polisi?, sababu kuna kipindi mwandishi mmoja alipigwa risasi alipokua akifuatilia biashara za magendo katika mpaka wa Tanzania na Kenya.

3. Je? ni nani anayewapangia assignments za kufanya, Ni mhariri, ama ni nyinyi wenyewe huwa mnajiamulia mambo ya kufanyia uchunguzi?

4. Katika kufuatilia habari, huwa mnahitajika kuwa na kibali maalumu kutoka jeshi la polisi ama?

5. Ni Changamoto zipi mnakutana nazo katika kazi zenu za kila siku?

6. Kuna Fununu kwamba baadhi ya waandishi wa habari huwa ni wapelelezi , ama usalama wa Taifa , kuna ukweli wowote kuhusu hili?

Kwa leo naomba nikomee hapa . Tafadhali naombeni ushirikiano wenu. naandika hadithi hii si kwa sababu nataka kujifurahisha tu, bali kwa kuuona na kuuthamini mchango wa waandishi wa habari katika kuleta mabadiliko ya mtanzania. kifikra na kimaisha kwa ujumla. Kama unaona hautaweza kumwaga mtama katika kuku wengi, tafadhali usisite kunitumia Private message kadri iwezekanavyo.

P.S; Mods nawaomba msiifute haraka hii thread. iacheni ielee kwa muda.

Asanteni !
 
'Katika kuandika habari nahitaji kibali cha polisi', labda uwe wazi, habari gani unataka kuchunguza. Kama ni habari za mamantilie wa Temeke huhitaji kibali. Lakini kama ni habari kuhusu mahabusu ndani ya 'sello' za polisi nadhani lazima upate ridhaa yao. Ninachosema hapa, unataka kuchunguza habari zipi?
 
Wasalaam!
Hapa nilipo ninaandaa hadithi inayomhusu mwandishi wa habari za kichunguzi ( Investigative Journalist ). Binafsi sina uelewa wowote kuhusu uandishi wa habari , bali nina mapenzi na kuandika hadithi.
Mambo ninayotaka kujua ni haya :

1. Ni ipi miiko ya uandishi na ufuatiliaji wa habari za kichunguzi ?

2. Ni ipi mipaka inayotenganisha kati ya mwandishi wa habari za uchunguzi na Inspekta wa polisi?, sababu kuna kipindi mwandishi mmoja alipigwa risasi alipokua akifuatilia biashara za magendo katika mpaka wa Tanzania na Kenya.

3. Je? ni nani anayewapangia assignments za kufanya, Ni mhariri, ama ni nyinyi wenyewe huwa mnajiamulia mambo ya kufanyia uchunguzi?

4. Katika kufuatilia habari, huwa mnahitajika kuwa na kibali maalumu kutoka jeshi la polisi ama?

5. Ni Changamoto zipi mnakutana nazo katika kazi zenu za kila siku?

6. Kuna Fununu kwamba baadhi ya waandishi wa habari huwa ni wapelelezi , ama usalama wa Taifa , kuna ukweli wowote kuhusu hili?

Kwa leo naomba nikomee hapa . Tafadhali naombeni ushirikiano wenu. naandika hadithi hii si kwa sababu nataka kujifurahisha tu, bali kwa kuuona na kuuthamini mchango wa waandishi wa habari katika kuleta mabadiliko ya mtanzania. kifikra na kimaisha kwa ujumla. Kama unaona hautaweza kumwaga mtama katika kuku wengi, tafadhali usisite kunitumia Private message kadri iwezekanavyo.

P.S; Mods nawaomba msiifute haraka hii thread. iacheni ielee kwa muda.

Asanteni !

sijui kama wapo..
 
Back
Top Bottom