Ombi kwa TFF kutumia marudio ya matukio ya Azam kama VAR kwenye matukio Tata

abdulhamis

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
1,436
2,292
Habar wadau wa michezo,

Baada ya kelele nyingi za muda mrefu kua Tanzania marefa wetu Hua wanaboronga mechi kutokana na kufanya maamuzi ambayo yanaleta utata nimeona ni Bora wawawekee waamuzi wetu screen ndogo ambayo inakua imeonganishwa moja kwa moja na kifurush cha Azam ili kama linatokea Tatizo Tata na linaitaji maamuzi refa anaweza kuangalia Marudio ya Azam TV kama tunavyo angalia sisi

Nimesema ivyo kwa sababu Mara nyingi hutokea Matukio ambayo refa na watu wote wanao angalia mechi kushindwa kulielewa Tukio kwa haraka mpaka pale tunapo angalia Marudio na Mara nyingi tunao angalia Marudio ni mshabik tu Tena tunao angalia nyumbani na baada ya kujua kua refa kafanya Makosa Hua Tunaanza kumlaum wakat hata sisi tumeona kosa baada ya video za Marudio.

Ivyo ningependa kushaur serikal kuwawekea marefa vi screen vidogo hata nje ya uwanja ili marefalii nao wapate faida ya marejeo Ya video ili kuwaondolea utata. Tusisubir mpaka nchi ziwe na uwezo wa VAR Kwan hata Marejeo ya video za Azam zinaweza kutusogeza sogeza.

Pia, kwa ili wazo nina iman tanzania tukiwa wa kwanza wengine watafata sababu ni wazo zuri.
 
naunga mkono hoja ....hasa matukio kama ya offside na fauls .........
Itasaidia Mimi naona kupunguza maamuzi tata wakati tukitafuta solution ya kudumu.....
 
Si rahisi Kama tufikiliavyo Kuna maswala ya patent right...uwezi kutumia idea ya mtu au kampuni Bila makubaliano maalum...
 
Back
Top Bottom